Saturday, 6 May 2017

CHADEMA watuma salamu za rambirambi kufuatia vifo vya Wanafunzi 32.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema wametuma salamu za rambirambi kufuatia kutokea kwa ajali mbaya iliyotokea leo na kusababisha vifo vya watu 32.

Katika salamu zao cha CHADEMA wamesema wamepokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa kwani taifa limepoteza watu muhimu ambao wangelitumikia taifa katika siku zijazo.

"Tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za ajali mbaya Iliyotokea Leo tarehe 6 Mei,2017 Mkoani Arusha, Wilaya ya Karatu na kusababisha vifo vya wanafunzi 33 (watoto wa kike 16 na watoto wa kiume 17) waliokuwa wanafunzi wa Shule ya Lucky Vicent ya Mkoani Arusha.....Hakika taifa limepoteza watoto wake na vijana wa Kesho ambao wangelitumikia taifa letu siku zijazo". Alisema Mrema

Aidha, chama cha CHADEMA pia wametoa pole kwa familia ya wafiwa, uongozi wa shule ya Lucky Vicent pamoja na wananchi kwa ujumla.
 
"Kwa majonzi makubwa tunatoa salamu za pole kwa wazazi, wanafunzi wa Shule ya Lucky Vicent,  uongozi wa Shule hiyo pamoja na wananchi wote wa Tanzania kwa msiba huu mkubwa na wenye kutia simanzi na huzuni kubwa...CHADEMA tutakuwa pamoja na familia za Marehemu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo , tunawataka wanachama na watanzania wote bila kujali imani zetu tuwakumbuke wafiwa katika Sala /Dua ili Mwenyezi Mungu awatie ujasiri wafiwa katika kipindi hiki kigumu". Alisema Mrema

Pamoja na hayo, CHADEMA wamelitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina juu ya chanzo cha ajali hiyo mbaya ili matokeo ya uchunguzi huo yatumike katika kuzuia ajali nyingine  isije kutokea katika siku zijazo.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa 

Related Posts:

  • Mmiliki wa Facebook Mark Zuckerberg akabidhiwa shahada ya heshima.Mwanzilishi wa Facebook na CEO Mark Zuckerberg amefanikiwa kupata shahada ya heshima kutoka katika chuo kikuu cha Havard, Marekani. Bosi huyo ambaye ni miongoni mwa matajiri wakubwa duniani kwa mujibu wa Forbes, aliwahi k… Read More
  • Njiwa Aliyetumika Kusafirisha Dawa za Kulevya, Akamatwa. Polisi wa Kuwait wamemkamata njiwa aliyekuwa amebeba dawa za kulevya aina ya Ketamine ambaye alikuwa amenasa kwenye bati la jengo la forodha katika Bandari ya Abdel iliyopo mpakani mwa Kuwait na Iraq. Katika taarifa iliy… Read More
  • Serikali kuongeza viwango vya pango la ardhi.Waziri wa Ardhi, Nyumba Maendeleo na Makazi, William Lukuvi amesema kuwa Serikali itaendelea kuongeza hazina ya ardhi kwaajili ya matumizi mbalimbali ikiwa ni pamoja na uwekezaji mkubwa katika sekta ya viwanda. Waziri Luk… Read More
  • Soma Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Leo. Bonyeza Links Zifuatazo: Job Opportunity at CVPeople Africa, Senior Business Advisor Job Opportunity at BBC World Service Job Opportunity at ABT Associates, Finance & Administrative Assistant Job Opportunities at F… Read More
  • Kagame atangaza kung'atuka. Kuelekea uchaguzi mkuu nchini Rwanda unaotarajiwa kufanyika Agosti 3 mwaka huu, Rais wa Rwanda Paul Kagame ameeleza kinaga ubaga kuwa ukomo wake wa kutawala ni mwaka 2024. Rais Kagame amethibitisha taarifa hizo kupitia … Read More

0 comments:

Post a Comment