Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imewajibu rasmi Simba
SC juu ya sakata lao la kupokwa pointi tatu za mezani walizopewa baada
ya rufaa yao dhidi ya Kagera Sugar wakidai kumcheza mchezaji Mohamed
Fakhi akiwa na kadi tatu za njano.
Kwa mujibu wa barua kutoka katika Bodi ya Ligi zimesema kuwa Fakhi
hakuwa na kadi tatu za njano wakati akicheza mchezo dhidi ya Simba
uliofanyikia uwanja wa Kaitaba, Bukoba Aprili 2 mwaka huu.
"TFF ambayo ndiyo yenye dhamana ya usimamizi wa mpira nchini na ambayo
ndiyo iliyokaimu madaraka kwa TPLB kuendesha ligi kuu iliitisha kikao
cha Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ambayo ilichunguza kwa undani
sakata hili na baada ya uchunguzi wao ambao walihoji watu mbalimbali,
walituandikia kutujulisha kuwa wamebaini mchezaji Mohamed Fakhi
anayelalamikiwa na Simba hakuwa na kadi 3 siku ya mchezo wa Kagera
Sugara dhidi ya Simba hivyo alikuwa halali kucheza mchezo huo". Ilisema
barua hiyo.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza HapaFollow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment