Tuesday 1 August 2017

LIPULI YAMNASA BUSUNGU KUIMARISHA SAFU YAKE YA "KUCHANA" NYAVU.

Baada ya kumnasa Ditram Nchimbi kutoka Mbeya City ili kuimarisha safu yake ya ushambulizi, Lipuli ya Iringa imemnasa Malimi Busungu.

Busungu amejiunga na Lipuli kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Mshambuliaji huyo alikuwa hatari wakati akiwa Mgambo FC ya Tanga hadi alipojiunga Yanga.

Msimu wa kwanza akiwa Yanga alionyesha cheche lakini kuanzia katikati mambo yalibadilika mwisho akapotea mwelekeo.


Hata hivyo, Busungu aliwahi kufanya mahojiano na SALEHJEMBE na kusema angependa kuondoka Yanga na kwenda kuanza upya na anajiamini atafanya vema.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment