Wednesday, 2 November 2016

#MICHEZO>>>>SAFARI YA MWISHO YA SIMBA ASIYEFUGIKA, BURIANI THOMAS MASHALI.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Kila mwanadamu ataonja mauti, kila mwanadamu ana safari yake ya mwisho.

Safari ya mwisho ya bondia Thomas Mashali ilikuwa leo alipozikwa kwenye makabuli ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Mashali alifariki dunia baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana.

Hadi anafariki dunia, Mashali alikuwa ni bondia namba mbili kwa viwango baada ya Francis Cheka lakini ikiwa ni miezi kadhaa baada ya kumtwanga Cheka.

Alikuwa na mikanda minne ya ubingwa katika mashirikisho mbalimbali likiwemo lile la UBO.


Mashabiki wengi walijitokeza leo kumuaga kwenye Viwanja vya Leaders kabla ya kumzika kwenye makaburi hayo ya Kinondoni.

#MICHEZO>>>TUMBA SUED VS DONALD NGOMA ILIKUWA SI MCHEZO PALE SOKOINE LEO.FAHAMU ZAIDI HAPA.



Beki Tumba Sued wa Mbeya City yeye aliamua kula sahani moja na mshambuliaji Donald Ngoma wa Yanga.

Mbeya City imeitwanga Yanga kwa mabao 2-1 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, leo.
Tumba alikuwa busy na Mzimbabwe huyo kokote aliko na kweli akafanikiwa kumbana vilivyo.


Angalia taswira walivyokuwa wakipambana, haikuwa kazi rahisi.

#YALIYOJIRI>>>>Taarifa Kuhusu taharuki ya Moto uliolipuka kwenye bandari ya Dar es salaam.Fahamu zaidi hapa.

Jana Nov 1 2016 katika Bandari ya Dar es salaam kulitokea moto ambao ulizua taharuki kwa baadhi ya wafanyakazi na watu wengine waliokuwa eneo hilo la bandari. 
Moto huo ulilipuka kwenye makontena na kuteketeza kontena tatu zilizokuwa na matairi ya magari na kudumu kwa muda wa dakika 30.

Mkuu wa mawasiliano wa mamlaka ya Bandari, Peter Mlanzi ametoa ufafanuzi kuhusu moto huo kwamba uliandaliwa makusudi kwa ajili ya kukipima kikosi cha zima moto…
"Tukio hili tumelitengeza kwa makusudi ili tuone namna ambavyo  kikosi kazi cha zimamoto na uokoaji kinavyoweza kukabilana na majanga mbalimbali" Alisema Mlanzi

Aidha kwa upande wake mkuu wa kikosi cha zimamoto bandari ya Dar es salaam, Mussa Biboze, alisema' "kwa zimamoto moto uko kwenye madaraja, huu moto wa matairi ni moto wa daraja A ambao unazimwa tu na maji ya kawaida"

#YALIYOJIRI>>>>>Serikali yavipa siku mbili vyuo vikuu ambavyo havijatuma matokeo ya wanafunzi Bodi ya Mikopo (HESLB).Fahamu zaidi hapa.

Serikali kupitia Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Maimuna Tarish imevitaka vyuo vikuu 14 ambavyo havijatuma matokeo ya wanafunzi wao ya mwaka uliopita kwa Bodi ya Mikopo kutuma mara moja ili kuwapatia mikopo kwa walio katika utaratibu wa kupata mkopo wa serikali.

Taarifa ambayo imetolewa na Tarish imevipa vyuo hivyo 14 siku mbili pekee kuhakikisha vinatuma majina kwa Bodi ya Mikopo na kuagiza viweke mfumo mzuri ambao utawawezesha kutuma matokeo kwa haraka.

#MICHEZO>>>>SIMBA YATAKATA KAMBARAGE SHINYANGA MBELE YA STAND UNITED.FAHAMU ZAIDI HAPA.

MPIRA UKWISHAAAAA
-Mnyate anaachia shuti la chinichini hapa lakini ni goal kick
-Mpira unateleza na unaonekana kuwasumbua wachezaji wengi
-Simba wanaonekana kuosha kila mpira unaokwenda langoni mwao
DAKIKA 6 ZA NYONGEZA
Dk 89, Simba wanapata kona na inakwenda kuchongwa Bukungu, kipa Frank Muonge anajitahidi kudaka vizuri kabisa
SUB Dk 88, Ibrahim Ajibu anaingia kuchukua nafasi ya Mavugo
Dk 88, mvua imeanza kunyesha uwanjani hapa na mashabiki wengi wanakimbia kutoka majukwaani
Dk 87, Angban yuko chini baada ya kuumia wakati akijaribu kuudaka mpira wakati wa shambulizi lililoelekezwa langoni mwake

Dk 82, kipa Muhonge anatoka na kumuwahi Mavugo aliyekuwa anakaribia kufunga. Lakini anampiga na mguu tumboni wakati akiokoa
Dk 81, Mavugo anapokeza nafasi mujarab ya kufunga kwa kuwa kipa wa Stand alikuwa ametoka langoni, likiwa wazi MAvugo amepiga nje
SUB 80, Moussa Ndusha ambaye ITC yake imekuja, anaingia kuchukua nafasi ya Kazimoto
SUB Dk 75 Kichuya anatoka na nafasi yake inachukuliwa na Jamal Simba Mnyate

DK 70, Wanachofanya Simba, wote wamerudi nyuma na wanafanya mashambulizi kwa kuwatumia watu watatu waende mbele kushambulia ambao ni Kichuya, Mavugo na Mwinyi Kazimoto tu
Dk 67, Kiemba anafanya yake hapa, anamtoka Bukungu na Juuko na kutoa pasi safi

Dk 64, Mo Ibrahim anaingia vizuri, ananyoshaa, unapita juu kidogo
DK 60, Selembe anapiga kichwa safi mbele ya mabeki wa Simba, goal kick
Dk 58, Stand wanapata kona inachongwa na Angban anaidaka kwa ulaini kabisa
Dk 56, Job analazimika kufanya kazi ya ziada kuokoa pasi nzuri ya Kichuya iliyokuwa inakwenda kwa Mo Ibrahim. Inakuwa inachongwa lakini haina faida
Dk 53, Stand wanafanya shambulizi kwa mpira wa adhabu, lakini juuuu
Dk 50, Stand wanaonekana kwenda taratibu na zaidi wanamtumia Amri Kiemba ambaye yuko vizuri
Dk 47, mpira umeanza kwa kasi na Stand United wanaonekana wamepania kusawazisha bao


DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 45, Kichuya anapaa kama mkizi na kuunganisha kichwa mpira wa adhabu lakini unatoka sentimeta chache kwenye lango la Stand
Dk 43, hakuna shambulizi kali zaidi ya kila timu kupiga pasi nyingi, Stand wakionekaan kufika zaidi kwenye lango la Simba
Dk 42 sasa, Stand wanaonekana kuongeza mashambulizi mengi zaidi ya Simba ambao wanafanya mashambulizi ya kushitukiza tu
Dk 35, Stand wanapata kona baada ya kusukuma mashambulizi mfululizo kwenye lango la Simba
]Dk 33, GOOOOOOOOO Kichuya aaukwamisha mpira wavuni
Dk 31, PENAAAAAAAT...MAVUGO Anaangushwa na Adeyum
Dk 30, Stand wanafanya shambulizi kali hapa, piga nikupige lakini Simba wanaokoa
KADI Dk 29, Mwanjale analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Sabato
Dk 27, mpira unaendelea lakini ni taratibu kutoka kila upande kama vile hakuna timu yenye haraka
Dk 26 sasa, mpira umesimama, kuna mchezaji wa Stand United anatibiwa pale uwanjani
Dk 23, Mo Ibrahim anapoteza nafasi nzuri hapa ya kufunga akiwa amebaki na lango, mpira unamzidi nguvu
Dk 22, mpira unaonekana kuchezwa zaidi katikati ya uwanja na hakuna mashambulizi makali kwenye milango
DK 19, Bukungu anafanya kazi ya ziada kuokoa krosi ya Kelvin Sabato
Dk 13, Stand wanaonekana ni wengi zaidi nyumba huku wakifanya mashambulizi ya kushitukiza
Dk 10, mpira unaonekana kuwa wa juu zaidi na hata milango haina kashkash sana, kila timu iko makini kwenye ulinzi
Dk 5 sasa, bado mpira unaonyesha kuchangamka lakini timu zote mbili si bora katika umaliziaji
Dk 1, mechi inaanza na Simba wanakuwa wa kwanza kushambulia. Lakini Mavugo anacheza faulo na mwamuzi anasema mpira uelekezwe Simba

#MICHEZO>>>>"YANGA" yala kipigo mbele ya "MBEYA CITY" goli 2 kwa 1.Fahamu zaidi hapa.

Dakika ya 6, Hassan Mwasapili anapiga mpira unaojaa moja kwa moja wavuni baada ya kumshinda kipa Dida Munishi.

Wakati kipindi cha kwanza kikielekea mwishoni Mbuyu Twite analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Ally Ramadhani
DAKIKA 4 ZA NYONGEZA 
Dk 44, hakuna matumaini kama Yanga wanaweza kusawazisha dhidi ya Mbeya City kwa kuwa hakuna shambulizi kali
Dk 42, mwamuzi anasema lile ni bao lililofungwa na Kenny Ally dak ya 36, hivyo Mbeya City wanaongoza kwa mabao 2-0.


MAPUMZIKO
Ngoma anaunganisha krosi ya Msuva vizuri hapa na kuandika bao moja kwa Yanga.
 

Mahakama Yamtia Hatiani Lady Jaydee.Yamwamuru Amuombe Radhi Ruge wa Clouds Media.Fahamu zaidi hapa.

Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni imemkuta na hatia mwanamuziki Judith Wambura maarufu Lady Jaydee kumkashifu Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga pamoja na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba.

Hukumu hiyo imesomwa mahakamani hapo kufuatia kesi iliyokuwa imefunguliwa na viongozi hao wawili wa Clouds Media Group wakimtuhumi Judith Wambura kuwakashifu na kuwaharibia taswira zao na kampuni yao katika jamii.

Awali mahakama hiyo ilipanga kusoma hukumu ya kesi hiyo ya madai Oktoba 13 mwaka huu lakini Hakimu Lyamwike aliiahirisha hadi Novemba 2 mwaka huu kwa maelezo kuwa hakuwa amemaliza kuiandikia hukumu.

Katika kesi ya msingi, Joseph Kusaga na Ruge Mutahaba waliiomba mahakama itamke kuwa maneno yaliyotolewa na Judith Wambura kubitia blog yake ni kashfa na yanaathiri taswira yao katika jamii, pia mahakama imuamuru aombe radhi kupitia vyombo vya habari na alipe fidia kutokana na madhara ya jumla kwa jinsi mahakama itakavyoona inafaa.

Judith Wambura aliandika waraka katika blog yake na kwenye baadhi ya magazeti uliokuwa na kichwa cha habari “Wosia wangu ikitokea nimetangulia kufa kabla ya Ruge na Kusaga.”

Wakati akijibu shtaka hilo, Wambura ambaye alikuwa mtetezi pekee wa upande wake alikiri kuandika waraka huo, hivyo mahakama imemtaka aombe radhi kwenye chombo cha habari chenye coverage kubwa hapa  nchini na ikiwezekana duniani pia

Tuesday, 1 November 2016

Wema Sepetu Atangaza Kupumzika Instagram Kwa Muda...Maneno Maneno Yamkimbiza.Fahamu zaidi hapa.

Maskini Watu wanaingilia life ya Wema Sepetu mpaka ametangaza kujitoa Insta kwa muda....Chaaa!!!! Waliokuwa Marafiki zake na Timu Wema hali si shwari, Munalove na Hope wanashutumiana kumsengenya Wema na kumuendea kwa mganga....

Toa maoni yako kwake kuhusu wanaomuingilia life yake

#YALIYOJIRI>>>> EWURA yatangaza bei mpya ya mafuta.Fahamu zaidi hapa.

Mamlaka ya udhibiti wa hudumaza nishati na maji EWURA imetangaza bei mpya za bidhaa ya mafuta ambazo zitaanza kutumika kesho Jumatano huku bei ya Petrol ikiongezeka kwa shilingi 33, Diesel imeongezeka kwa Shilingi 21 na mafuta ya taa yakiongeka kwa Shilingi 11.

#YALIYOJIRI>>>Boniface Jacob(CHADEMA) ashinda Umeya wa Manispaa ya Ubungo.Fahamu zaidi hapa.

Diwani wa Kata ya Ubungo kwa tiketi ya CHADEMA, Boniface Jacob ameshinda nafasi ya Umeya Manispaa ya Ubungo katika uchaguzi uliofanyika leo baada ya ule wa awali kuhairishwa.

Amepata jumla ya kura 16 za UKAWA na kura 2 CCM huku Naibu Meya akishinda kwa kura 15 dhidi ya kura 3.

#MICHEZO>>>>WANACHAMA YANGA WANUSURIKA KATIKA AJALI MBAYA YA GARI WAKIWA NJIAJI KUIFUATA MBEYA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Baadhi ya wanachama wa Yanga, wamepata ajali mbali ya gari.

Bahati nzuri, wote wamefanikiwa kutoka salama katika ajali hiyo iliyotokea katika eneo la Mwidu, wakiwa njiani kwenda Mbeya kuiwahi mechi kati ya Yanga dhidi ya Mbeya City, kesho.
Baadhi ya viongozi waliokuwa katika gari hilo dogo aina ya Suzuki Vitara ni kamati ya mashindano na ya Utendaji ya Yanga, Omary Said, Bakili Makele na Seif Chuma walikuwa ndani ya gari hilo.
Makele amethibitisha wao kupata ajali hiyo na kusema wameamua kuahirisha safari.
“Tunashukuru Mungu sana, tumetoka salama ingawa ajali ilikuwa mbaya sana. Sasa tunarejea Chalinze ambako tutafanya taratibu nyingine,” alisema.
Hebron Malele, inatoa pole kwa wanamichezo hao kwa ajali mbaya iliyowakuta. Mungu awape nguvu zaidi.

#MICHEZO>>>>MASHALI KUAGWA LEADERS CLUB KESHO SAA TANO ASUBUHI.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Shughuli za mazishi ya bondia Thomas Mashali zitaanza kesho saa tano asubuhi kwenye Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.

Kamati ya mazishi iliyokutana leo na kuongozwa na Japhet Kaseba, Rashid Matumla, Emmanuel Mlundwa, Juma Mbizo na wengine, imefikia uamuzi huo kuwa Mashali ataagwa Leaders na mazishi ni makaburi ya Kinondoni.
Mashali ameuwawa na watu wasiojulikana na bado polisi haijaeleza nini hasa imepata.
 
Lakini taarifa zinasema alishambuliwa hadi kupasuliwa kichwa katika eneo la Tabata karibu kabisa na Kimara Bonyokwa.
 
Alikimbizwa katika Hospitai ya Palestina, lakini ikashindikana. Akahamishiwa Muhimbili ambako alipoteza maisha usiku wa kuamkia juzi.

#YALIYOJIRI>>>>Serikali Yahakiki Vyeti vya Ndoa, Walimu Wajiandaa Kugoma.Fahamu zaidi hapa.

Gazeti la Tanzania Daima limeripoti kuwa Serikali imeanza uhakiki wa vyeti vya ndoa kwa watumishi wa umma. Hatua hiyo ambayo imewashtua watumishi wengi wa umma, imeelezwa kuwa ni mwendelezo wa harakati za Serikali ya Rais John Magufuli kuhakiki watumishi wa umma ili kuondokana na watumishi hewa.

Wakati Serikali ikianza na uhakiki wa vyeti vya ndoa, kazi ya uhakiki wa watumishi hewa na vyeti vyao vya elimu inaendelea sehemu mbalimbali nchini.

Kwa muhibu wa Gazeti hilo, habari ambazo limezipata zinasema kuwa serikali imeanzisha uhakiki huo nchi nzima kwa madai kuwa baadhi ya watumishi wa umma wamekuwa wakitoa taarifa za uongo kwamba wana ndoa ili kupata nauli na stahiki zingine za likizo wakati hawana ndoa.

Habari zaidi zinasema kuwa walimu wakuu wa shule zote za Wilaya ya Ilala wamepewa siku mbili kutekeleza agizo hilo kwa walimu wao.

Mmoja wa walimu hao ambaye ameomba jina lake lihifadhiwe, alilithibitishia Tanzania  daima kuwa ametoa siku mbili kwa walimu wa shule yake wenye vyeti vya ndoa waviwasilishe kwake.

"Kweli tumepewa agizo hilo leo manispaa ya Ilala na tumetakiwa kuwasilisha vyeti hivyo kesho na tayari baadhi ya walimu wangu wamefanya hivyo leo na kesho zoezi hilo linakamilika"

Alipoulizwa sababu ya kuwepo kwa zoezi hilo, mwalimu huyo alisema hajui lakini anahisi lina lengo la kudhibiti taarifa za uongo za watumishi wakati wa kuomba likizo.

Wakati walimu wa shule za Ilala wakitakiwa kuwasilisha vyeti vyao vya ndoa, wilaya nyingine za Temeke, Kinondoni, Ubungo na Kigamboni hawana taarifa hizo.

Mmoja wa walimu kutoka Manispaa ya Ilala alisema kuwa uhakiki huo una lengo la kutaka kuchelewesha zaidi malipo na stahiki za walimu za likizo ambazo hazijalipwa kwa miaka mingi.

#MICHEZO>>>MTITI MWINGINE WA LIGI KUU BARA KESHO HUU HAPA.FAHAMIU ZAIDI HAPA.

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea kesho kwa viwanja sita ambako kwa mara ya kwanza timu zote za Dar es Salaam zitakuwa mikoani kupambana kutafuta nafasi bora katika ligi hiyo iliyoanza Agosti 20, 2016 kabla kufifikia ukomo wa mzunguko wa 15, Novemba 12, mwaka huu.
 
Vinara ligi hiyo kwenye msimamo msimu wa 2016/17, Simba SC watakuwa wageni wa Stand United kwenye Uwanja wa CCM Kambarage wakati mabingwa watetezi wa taji hilo Young Africans itakaribishwa na Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
 
Africans Lyon pia ya Dar es Salaam itakuwa mkoani Pwani kucheza na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani wakati Maafande wengine kutokea mkoani humo – JKT Ruvu watakuwa wageni wa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Majimaji ilihali Ndanda itawakabiri Ndanda FC kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara huku Toto African ikiwakaribisha Azam kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
 
Ligi hiyo itaendelea Alhamisi Novemba 3, mwaka huu kwa michezo miwili ambayo itafanyika mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa Mwadui kuialika Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mwadui Complex huko Shinyanga huku Mbao Fc ikiwa na kibarua kigumu dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.
 
Wakati ligi hii ikiingia ukiongoni kwa nusu msimu, TFF inatoa wito kwa timu kuajiandaa na dirisha dogo la usajili linalotarajiwa kuanza Novemba 15, mwaka huu kusajili wachezaji mahiri ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwendelezo wa ligi hiyo nusu ya msimu uliobaki utakaoanza baadaye Desemba.
 
Wakati wa usajili wa dirisha dogo ndipo michuano ya hatua ya awali ya kuwania Kombe la Shirikisho la Azam 2016/2017 inatarajiwa kuanza Novemba 19, mwaka huu ambako pia imepangwa kuzindua michuano hiyo hukop mkoani Mara.

Safari hii timu shiriki zimeongezwa mabingwa wa mikoawa mwaka jana hivyo kufikisha idadi itakayofika 86 badala ya 64 za msimu ulioipita. Imechukuliwa mikoa 22 baada ya ile mitano, kupanda Daraja kucheza Ligi Daraja la Pili msimu huu ambayo imeanza kushika kasi.

Linah Adai Amejaribu Kumweka Sawa Recho Lakini Ameshindwa.Fahamu zaidi hapa.

Msanii wa muziki Linah Sanga amedai kuwa amejaribu kuzungumza na msanii mwenzake Recho ili kumrudisha kwenye nafasi yake lakini ameshindwa.
Linah na Recho

Akiongea katika kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds TV wiki hii, Linah amesema tayari ameshamfuata Recho mara kadhaa ili amweleze kinachomsibu lakini amekuwa msiri.

“Sisi wasanii tulilelewa kwa kushirikiana kwa kila hali na tulipenda kwa sababu kuna wakati tunaishi pamoja, tunatungiana nyimbo,” alisema Linah “Kwahiyo kwa upande wangu mimi na niseme ukweli namfutilia sana Recho, shoga yangu vipi? Mbona kimya, fanya hivi lakini huwezi kujua kwanini yupo vile na kwanini anashindwa kubadilika,”

Muimbaji huyo ambaye aliwahi kufanya vizuri na wimbo ‘Upepo’ amekuwa kimya kwa muda mrefu bila kuweka wazi kitu kinachomsibu.

#YALIYOJIRI>>>Taarifa kutoka Ikulu: Rais Magufuli na Rais Kenyatta wazindua barabara ya Southern By-pass.Fahamu zaidi hapa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta leo tarehe 01 Novemba, 2016 wamezindua barabara ya Southern By-pass iliyojengwa kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Nairobi nchini Kenya.

Sherehe ya uzinduzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 28 na inayounganisha maeneo mbalimbali ya Jiji la Nairobi imefanyika katika eneo la Karen nje kidogo ya Jiji la Nairobi.

Akizungumza katika sherehe hiyo Rais Magufuli amempongeza Rais Kenyatta na Serikali yake kwa kujenga barabara hiyo ambayo sio tu itawasaidia wananchi wa Kenya bali pia itawasaidia wananchi wa Afrika Mashariki wanaotumia barabara zinazopitia Nairobi.

Rais Magufuli pia ameishukuru Serikali ya China kupitia benki yake ya Exim ambayo imetoa mkopo wa kujenga barabara hiyo, kwa kuendelea kuziamini nchi za Afrika Mashariki na kuzikopesha mikopo inayosaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara.

“Wananchi wanahitaji maendeleo na haya ndio maendeleo, barabara hii itasaidia kuinua uchumi na itasaidia masuala ya kijamii” amesema Rais Magufuli.

Dkt. Magufuli amesema viongozi wa Afrika Mashariki wameamua kufanya kazi ya kuharakisha maendeleo na kuinua maisha ya wananchi, na kwamba ili kufanikisha hilo wamedhamiria kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa barabara zinazounganisha nchi wanachama na kujenga vituo vya pamoja vya utoaji wa huduma za mpakani (One Stop Border Post).

Kwa upande wake Rais Kenyatta amesema kujengwa kwa barabara hiyo kumesaidia kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Nairobi na pia kutaboresha shughuli za maendeleo ya wananchi.

Mhe. Kenyatta amemshukuru Rais Magufuli kwa kuungana nae kuzindua barabara hiyo na amesema Kenya itaongeza juhudi katika utekelezaji mradi wa ujenzi wa barabara zinazounganisha Kenya na Tanzania zikiwemo barabara ya Malindi kupitia Saadani hadi Bagamoyo nchini Tanzania na barabara ya Voi – Taveta- Horiri-Arusha.

Sherehe za uzinduzi wa barabara ya Southern By-pass zimehudhuriwa na Naibu Rais wa Kenya Mhe. William Ruto.

Kabla ya kuzindua barabara hiyo Rais Magufuli ametembelea kiwanda kidogo cha kusindika maziwa cha Eldoville kilichopo katika eneo la Karen ambacho kinamilikiwa na familia ya mkulima Bw. James Karuga.

Familia hiyo ilianzisha kiwanda cha kusindika maziwa mwaka 1985 kwa uzalishaji wa chini ya lita 1,000 kwa siku na hivi sasa imefikia uzalishaji wa lita 5,000 kwa siku na inatarajia kuongeza uzalishaji hadi lita 70,000 katika mwaka mmoja ujao baada ya kuongeza kiwanda cha pili.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Nairobi
01 Novemba, 2016

Mkenya Aibuka Mshindi wa Maisha Plus.Fahamu zaidi hapa.

Olivie Kiarie wa Kenya ameibuka mshindi wa shindano la Maisha Plus. Fainali za shindano hilo zilifanyika mwishoni mwa wiki.
Ushindi huo umempa Olive kitita cha shilingi milioni 30 za Kitanzania.
Shindano la Maisha Plus lilishirikisha nchi za Afrika Mashariki.

#YALIYOJIRI>>>>Mtihani wa Kidato cha Nne kuanza leo..NECTA Yatoa Onyo.Fahamu zaidi hapa.

Watahiniwa 408,442 wamesajiliwa na Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne unaotarajia kuanza leo hadi Novemba 18, mwaka huu.

Akizungumzia maandalizi ya mtihani huo, Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde alisema kati ya watahiniwa waliosajiliwa wa shule ni 355,995 na wa kujitegemea ni 52,447. Mwaka 2015, waliosajiliwa kufanya mtihani ni 448,382, hivyo kuwapo na upungufu wa watahiniwa 39,940.

Dk Msonde alisema kati ya watahiniwa wa shule 355,447 waliosajiliwa, wavulana ni 173,423 ambao ni asilimia 48.72 na wasichana ni 182,572 sawa na asilimia 51.28. Watahiniwa 59 ni wasioona na wenye uoni hafifu ni 283.

Alisema kati ya watahiniwa wa kujitegemea 52,447 waliosajiliwa, wanaume ni 25,529 sawa na asilimia 48.68 na wanawake ni 26,918 sawa na asilimia 51.32.

Pia watahiniwa wa kujitegemea wasioona wako saba, wanawake watatu na wanaume ni wanne. Mwaka jana watahiniwa wa kujitegemea walikuwa ni 54,317.

Kuhusu watahiniwa waliosajiliwa kufanya Mtihani wa Maarifa (QT), Dk Msonde alisema baraza limesajili 20,634 ambao wanaume ni 7,819 sawa na asilimia 37.89 na wanawake ni 12,815 sawa na asilimia 62.11. Mwaka jana, idadi ya watahiniwa wa QT walikuwa 19,547.

“Maandalizi yote kwa ajili ya mtihani huo yamekamilika ikiwa ni pamoja na usambazaji wa mtihani, vitabu vya kujibia na nyaraka zote muhimu zinazohusu mtihani huo katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani,” alieleza Dk Msonde.

Aidha, baraza limewaasa wanafunzi, walimu kutojihusisha na vitendo vya udanganyifu wa mtihani kwani watakaobainika kufanya hivyo watachukuliwa hatua kali zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kufutiwa matokeo yote.

Katika matokeo ya darasa la saba yaliyotangazwa wiki iliyopita, wanafunzi 238 kutoka shule sita walifutiwa matokeo yao yote kutokana na udanganyifu wa mtihani.

Dk Msonde alizitaka Kamati za Mitihani za Mikoa na Halmashauri, kuhakikisha kuwa taratibu zote za uendeshaji mitihani ya Taifa zinazingatiwa ipasavyo, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa mazingira ya vituo yapo salama, tulivu na kuzuia mianya yote inayoweza kusababisha udanganyifu. Pia Dk Msonde alitoa mwito kwa wasimamizi wote kufanya kazi yao kwa umakini na uadilifu wa hali ya juu.

“Wasimamizi wanaaswa kujiepusha na vitendo vya udanganyifu kwani baraza litachukua hatua kali kwa yeyote yule atakayebainika kukiuka taratibu za uendeshaji wa Mitihani ya Taifa,” alieleza.

Barua ya Tupac Kuuzwa Shilingi Milioni 378.Fahamu zaidi hapa.

Ni miaka 20 tangu afariki rapper mkongwe, Tupac. Na sasa barua ambayo aliiandika, mwenyewe inatarajiwa kuuzwa kwa kiasi cha $172,750 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 378 za kibongo.

Kampuni ya Goldin Auctions, imesema barua hiyo iliyondikwa na Tupac Shakur ni moja ya vitu kumi vilivyokuwa vikimilikiwa na rapper huyo ambavyo vyote vitauzwa kwa mtonyo wa $206,625.

#YALIYOJIRI>>>>‘Makonda’ Feki Awatapeli Wachina Mil 22.8.Fahamu zaidi hapa.

Dar es Salaam. Raia wa China wametapeliwa fedha taslimu Sh 22.8 milioni wakidai kuwa sauti waliyoisikia kwenye simu ya kiganjani iliyotumiwa na tapeli ilifanana na ya  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro alisema jana ofisini kwake kuwa Oktoba Mosi, mwaka huu mfanyakazi wa Kampuni ya Group Six ambaye  ni raia wa China, Marco Li (24) alipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni Makonda.

Sirro alisema tapeli huyo alimtaka raia huyo atoe Dola 3,500 za Marekani kwa ajili ya msaada wa kumsomesha mwanafunzi aliyechaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Manilla kilichopo nchini Ufilipino.


“Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Jensen Hung (39) alikubali ombi la mkuu wa mkoa huyo feki na kumtuma msaidizi wake, Marco Li aende ofisini kwake kwa ajili ya kujiridhisha,” alisema Sirro.

#YALIYOJIRI>>>>Paul Makonda Amezindua Nembo ya I love Dar (Naipenda Dar).Fahamu zaidi hapa.

Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda amezindua nembo ya I love Dar (naipenda Dar) inayobeba dhana nzima ya utalii wa ndani hususan mkoa wa Dar es Salaam.

Tukio hilo lilotokea juzi usiku majira ya saa saba huku likishuhudiwa na mamia ya watu waliojitokeza kwenye uzinduzi huo uliofanyikia katika baa ya Element iliyopo Oyster bay.

Akizungumza baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa nembo hiyo Makonda alisema kuwa ni hatua nzuri kwa wadau binafsi kujitokeza na kuendeleza mazuri kwa Mkoa wa Dar es Salaam.

Alisema kuwa kwa kupitia nembo hiyo ya I love Dar inahamasisha kuendeleza uzuri wa Mkoa wa Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kutangaza kila aina ya kivutio chake.

Alisema, vipo vitu vya asili ambavyo vinatumiwa kama utalii hasa kuanzia majengo ya kizamani hasa maeneo na mjini, makumbusho za taifa zenye kuhifadhi historia ya Mkoa pamoja na mengineo.

Alisema kuwa nembo hiyo inaenda mbali hadi kuhamasisha masuala ya kimaendeleo ya Dar es Salaam likiwamo suala zima la usafi pia.

“Najua I Love Dar ni nembo ambayo inamaana kubwa sana kwa wananchi kwa ujumla kuipenda Dar ni pamoja na kufanya mazuri kwa ajili ya Mkoa huu hapo ikiwa ni suala zima la kutangaza vivutio, kuzingatia usafi na mengine yote mazuri” alisema Makonda.

Kwa upande wake Meneja wa Baa ya Element, Mackenzie alisema kuwa katika kuhakikisha kuwa inaunga mkono sera ya kuendeleza utalii wa ndani imeamua kuanzia kwa kubuni nembo hiyo.

Alisma hata katika majiji makubwa duniani kama vile New York ina nembo ya I love New York na kwa hapa nchini kuandika I love Dar ni mwanzo wa kuliendeleza jiji la Dar kwa kuanzia kwenye Utalii.

#YALIYOJIRI>>>>Wahariri wamuangukia Rais Magufuli.......Wamtaka Amshughulikie Serukamba Kwa Kuvuruga Muswada wa Habari.Fahamu zaidi hapa.

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limemwomba Rais John Magufuli kumshughulikia Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Peter Serukamba kwa maelezo kuwa ni ‘jipu’ ambalo limevuruga mjadala wa Muswada wa Huduma za Habari.

Hayo yalibainishwa jana Dar es Salaam wakati wahariri wa vyombo vya habari walipokuwa wakijadili vipengele vya Muswada huo ambavyo vinatakiwa kufanyiwa mabadiliko kabla ya kupitishwa kuwa sheria kwa kuwa si rafiki kwa tasnia ya habari nchini.

Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari Limited, Absalom Kibanda alisema Serukamba ni ‘jipu’ na kumwomba Rais aamini hivyo, akibainisha kwamba kipindi cha aliyekuwa Waziri wa Habari, Fenella Mukangara walipeleka hati ya dharura kutaka Muswada huo ujadiliwe vizuri, lakini alikataa huku akiunga mkono kama ulivyo.

“Kuna sauti ilisikika ikitembea katika mitandao, nikajiuliza ameongea kama Waziri, Ofisa Habari wa Serikali au mtu binafsi?” Alihoji Kibanda.

Kibanda alimwomba Rais aangalie ni nani wasemao ukweli kati ya wadau wa habari (wahariri na waandishiwa habari) na mamlaka nyingine za Serikali kuhusu namna nzuri ambayo Muswada huo unaweza kujadiliwa na kuwa sheria kwa maslahi ya Taifa bila kukwaza upande.

Aidha, alibainisha kuwa kuna watendaji wa Serikali ambao wamekuwa wakimsukuma Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, ili aridhie mahitaji yao kwa maslahi binafsi.

Alisema kwa sasa waandishi wa habari wanafananishwa na wahalifu na kusema hivi karibuni walichapisha habari kwenye gazeti lao na walikuja kuomba radhi baada ya kupokea vitisho.

Aliongeza kuwa Muswada huo ulitakiwa uwekwe vipengele vinavyowachukulia hatua watu wanaoingilia kazi za vyombo vya habari, kwa kuwa makosa mengi vinayotupiwa vyombo vya habari vyanzo huwa ni wanasiasa.

Mjumbe wa TEF, Jesse Kwayu alisema wana wasiwasi na msimamo wa Serukamba, kwa kuwa anashindwa kutimiza majukumu yake ya kuisimamia Serikali na badala yake anakuwa kama ni ofisa wa Serikali.

“Wakati akiusoma Muswada huu kwenye Kamati, akihitimisha alisema hakuna uhuru usio na mipaka,” alisema Kwayu.

Alibainisha kuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo aliyepita, alisikiliza vizuri mapendekezo ya wadau wa habari na kuyafikisha bungeni yajadiliwe tofauti na wa sasa ambaye si msikivu.

Alisema wakati wakiujadili hivi karibuni Dodoma ilifika mahali kukawa na mvutano mkali kati ya Serukamba na Zitto Kabwe kwa kuwa alikuwa hajaridhishwa na namna Muswada huo ulivyojadiliwa, kwa sababu wadau wa habari wahusika hawajahusishwa kikamilifu.

Alisema asilimia 80 ya waandishi wa habari wako mikoani ambako waandishi hao pia hawajajadili na kupata mwafaka wa Muswada huo.

Naibu Mhariri Mtendaji wa Jamhuri, Manyerere Jackton aliwataka Serukamba na Mkurugenzi wa Idara ya Habari, MAELEZO, Hassan Abbas wasijisahau na kupitisha Muswada huo eti kwa kuwa wako serikalini, bali wajue kuwa kuna wakati watarudi na kukabiliwa na sheria hiyo.

Mwenyekiti wa TEF, Theophil Makunga alisema Muswada huo usipobadilishwa vipengele hivyo na ukapitishwa kuwa sheria, waandishi wa habari watakuwa kwenye shida kubwa kwa kuwa watakuwa wakipambana na kitu kibaya sana.

Wema Sepetu Amuandikia Ujumbe Miss Tanzania Mpya.Fahamu zaidi hapa.

Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu amedai mshindi wa shindano la Miss Tanzania 2016, Diana Edward alistahili kuchukua taji hilo.

Kupitia Instagram, Wema ameandika:

When You Nailed that question Properly, I knew that The Crown was Yours…. Congratulations mdogo wangu… You deserve it… And I have a very good feeling about Your performance in the Miss World Beauty Pageant…. You will do Tanzania Proud… @dianaflave @dianaflave @dianaflave @dianaflave … #GoodMorningWorld

Faraja Nyalandu aliyewahi kushika taji hilo naye amekuwa miongoni mwa watu waliompongeza mshindi huyo

#YALIYOJIRI>>>>Lowassa, Sumaye Waibukia Bungeni Dodoma.Fahamu zaidi hapa.

Aliyekuwa Mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa na Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye leo asubuhi wamehudhuria Bungeni ambapo kimeanza kikao cha kwanza cha mkutano wa tano wa Bunge la 11, mjini Dodoma.

Mawaziri hao wastaafu walioihama CCM na kuhamia CHADEMA walikwenda mjini Dodoma kutoa somo kwa wabunge wa UKAWA jinsi ya kukabiliana na wabunge wa CCM wakiwa ndani ya ukumbi wa Bunge.

Hamisa Mobetto Afunguka Kuhusu Tetesi za Bifu Lake na Zari Hassan.Fahamu zaidi hapa.

Hamisa Mobetto amefunguka juu ya mahusiano yake na first lady wa Madale, Zari The Bosslady baada ya tetesi za kutoka na Diamond.

Mrembo huyo amemuambia mtangazaji wa kipindi cha The Playlist cha Times FM, Omary Tambwe aka Lil Ommy kuwa hajawahi kuwa na urafiki na Zari na wala hawana uadui wowote.

“Unajua huwezi kusema kuwa mimi na Zari tuko sawa au hatupo sawa kwa sababu hatujawahi kuwa marafiki, na mimi nimemjua kwa sababu ‘Kazaa’ na bosi wangu [Diamond Platnumz],” amesema Hamisa.

Malkia huyo wa video ya Salome ameongeza kuwa amewahi kuonana na Zari mara moja pekee ambapo ilikuwa ni kwenye 40 ya Tiffah mwaka jana.