Katibu wa
NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza mbele ya Waandishi wa habari
(hawapo pichani) mapema leo asubuhi,katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM
Lumumba jijini Dar es Salaam kuhusiana na uteuzi wa kamati ya Kampeni kwa
ajili ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 2015,ambayo itaongozwa na Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Wajumbe Kamati Kuu ya Halmashauri
Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa jana Agosti 17, 2015 katika kikao chake
cha siku moja kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba
jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dokta Jakaya Mrisho
Kikwete imekamilisha kazi ya uteuzi wa Wagombea Ubunge katika majimbo mawili ya
Singida Mashariki na Kiteto. Wagombea ubunge walioteuliwa kupeperusha bendera
ya CCM katika majimbo hayo ni pamoja na Ndugu Jonathan Njau (Singida Mashariki)
na Ndugu Emmanuel Papian John (Kiteto). Aidha Kamati Kuu imefanya uteuzi wa
Kamati ya Kampeni kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015 ambayo itaongozwa
na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. Wajumbe wa Kamati hiyo ni kama
ifuatavyo;- 1. KAMATI YA KAMPENI YA CHAMA CHA MAPINDUZI 1. Ndugu Abdulrahman
Kinana - Mwenyekiti 2. Ndugu Rajab Luhwavi - Makamu Mwenyekiti - Bara 3. Ndugu
Vuai Ali Vuai - Makamu Mwenyekiti - Z'bar 4. Ndugu Sofia Simba 5. Ndugu Mohamed
Seif Khatib 6. Ndugu Asha-Rose Migiro 7. Ndugu Samwel Sitta 8. Ndugu Nape
Nnauye 9. Ndugu Mwigulu Nchemba 10. Ndugu Harrison Mwakyembe 11. Ndugu January
Makamba 12. Ndugu Amina Makillagi 13. Ndugu Christopher Ole Sendeka 14. Ndugu
Stephen Wasira 15. Ndugu Abdallah Bulembo 16. Ndugu Hadija Aboud 17. Ndugu
Mohamed Aboud 18. Ndugu Lazaro Nyalandu 19. Ndugu Issa Haji Ussi 20. Ndugu
Waride Bakari Jabu 21. Ndugu Mahmoud Thabit Kombo 22. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha
23. Ndugu Maua Daftari 24. Ndugu Stephen Masele 25. Ndugu Pindi Chana 26. Ndugu
Shaka Shaka 27. Ndugu Makongoro Nyerere 28. Ndugu Bernard Membe 29. Ndugu
Sadifa Juma Khamis 30. Ndugu Antony Diallo 31. Ndugu Livingston Lusinde 32 . Ndugu
Ummy Mwalimu Imetolewa na:- Nape Moses Nnauye, KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA
TAIFA, ITIKADI NA UENEZI 18/08/2015
0 comments:
Post a Comment