Saturday, 31 December 2016

HARMONIZE ACHAGULIWA NA RAIS KIKWETE KWENDA KUWABURUDISHA NYUMBANI KWAO SIKU YA KUUAGA MWAKA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Hongera @harmonize_tz kwa kuchaguliwa kuburudisha katika hafla ya Kuukaribisha Mwaka Mpya Nyumbani kwa Mh Rais Mstaaf mh Jakaya Mrisho Kikwete, Msoga 31 dec 2016… Make us proud @harmonize_tz

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

Serikali Yapiga Marufuku Kuzungumzia Faru John.Fahamu zaidi hapa.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ramo Makani amesema kuwa hakuna mwenye Mamlaka ya kutoa tamko au ufafanuzi kuhusu faru John kwa sasa zaidi ya Waziri Mkuu kwa kuwa jambo hilo liko chini ya ofisi yake. kwaajili ya uchunguzi.

Ameyasema hayo Wilayani Ngorongoro katika ziara yake ya kikazi ya siku mbili wilayani humo kufuatilia changamoto za uhifadhi pamoja na utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu aliyo yatoa hivi karibuni akiwa Arusha.

“Ripoti hii ya uchunguzi ni mali ya Waziri Mkuu atakae weza kutoa ripoti hii nje kwaajili ya matumizi ya kila mmoja wetu kwa maana ya mamlaka, kwa hiyo hakuna mamlaka nyingine ya serikali yenye uhalali wa kutoa tamko au ufafanuzi wa jambo hili.”amesema Makani.

Hata hivyo, Makani amesema kuwa wanasubiri maagizo au maelekezo na mwelekeo wa sasa juu ya jambo hilo kutoka ofisi ya Waziri Mkuu.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

Waziri Mwigulu Nchemba akutana na mama yake Chid Benzi.Fahamu zaidi hapa.

Waziri Mwigulu Nchemba akutana na mama yake Chid Benzi "Nimekutana na kufanya mazungumzo na mama wa msanii Rashid Makwilo "Chid Benz" ambaye kwasasa amepatwa na tatizo la Dawa za kulevya.Inasikitisha na haivumiliki kuona nguvu kazi ya Taifa inapotea huku wauzaji wakinufaika kwa pesa haramu.Ifahamike wazi vita ya serikali dhidi ya magenge, wauzaji na wasambazaji wa madawa ya kulevya imeongezeka hasa katika awamu hii ya tano chini ya Mh.Rais J.P.Magufuli,hivyo anayejihusisha kwa namna yoyote ni vema akaamua kuachana nayo kabla hajakutwa na mkono wa dola.



Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

WACHINA WAKIWA KWENYE UBORA WAO, PEPE NAYE AFIKIRIA KWENDA ZAKE CHINA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Unaweza kusema Wachina wameleta mambo, maana beki wa kati wa Real Madrid, Pepe naye anafikiria kwenda China.

Hii ni sikh chache baada ya Carlos Tevez kukamilisha usajili wa kwenda China na atakuwa akipokea euro million 30 kila msimu.

Taarifa zinaeleza, Pepe anafikiria kwenda China na kujiunga na moja ya timu zinazoshiriki Super League.

Wachina wanaonekana kuanza kuwachanganya wachezaji mbalimbali kupitia fedha zao.


Klabu za China zimekuwa zikiwalenga wachezaji mbalimbali maarufu kutoka barani Ulaya wakiwemo wale wazaliwa wa Amerika Kusini ambao wanacheza barani Ulaya.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

Rose Ndauka: Sina mahusiano ya kimapenzi na MC Pilipili.Fahamu zaidi hapa.

Baada ya kuenea uvumi katika mitandao ya kijamii kuwa mchekeshaji MC Pilipili anatoka kimapeniz na Rose Ndauka, muigizaji huyo amekanusha uvumi huo.

Wiki chache zilizopita kupitia kipindi cha The Play List cha Times FM mchekeshaji huyo alidaiwa kukiri kutoka kimapenzi na muigizaji huyo.

Jana ijumaa muigizaji huyo amescreenshot ujumbe wa mtangazaji wa The Play List, Lilommy ambao ulidai huwenda wawili hao wakawa wanatoka kimapenzi na kuandaika

 “Jamaniii naomba niweke ili swala sawa sawa, mimi na MC Pilipili ni watu tunaofahamiana haswa kwenye kazi hatuna uhusiano wowote wa kimapenzi. NADHANI NTAKUWA NIMEELEWEKA”

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

Nicki Mbishi azungumza Ukweli...Adai Chidd Benz Hasaidiki na wala Hataki kuacha madawa.Fahamu zaidi hapa.

Hiki ndicho alichosema Nicki Mbishi azungumza Ukweli...Adai Chidd Benz ni mtu wa Kifo tuuu...Hasaidiki na wala Hataki kuacha madawa...watu kibao wamemshindwa...Hivyo Hakuna namna. ..!!!

TOA MAONI YAKO HAPA

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

Friday, 30 December 2016

HUU NDO MSHAHARA NA MADENI ANAYO DAIWA MBUNGE ZITTO KABWE.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Leo December 30, 2016 Mbunge Zitto Kabwe kutoka Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo) kupitia akaunti yake facebook ametoa taarifa kuhusu madeni anayodaiwa, kiwango cha mshahara wake wa mwaka, kiasi cha pesa kilichopo benki, posho pamoja na mali zote anazomiliki.

Hiki kimeandikwa na Zitto Kabwe leo.
 
Ndugu Watanzania, Kama mnavyofahamu kuwa ibara ya 132(4) na (5) na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Sheria namba 13 ya mwaka 1995 inataka viongozi wote wa umma kujaza fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni. Tamko hilo huwasilishwa Sekretariat ya Maadili ya Viongozi kabla ya mwisho wa kila mwaka. Kama nifanyavyo siku zote, nawajulisha rasmi kwamba nimetimiza matakwa hayo ya katiba na sheria kuhusu Maadili ya Viongozi.
 
Inafahamika kuwa Chama Cha ACT Wazalendo, kwa mujibu wa Katiba yake na Azimio la Tabora, kimeelekeza kuwa Viongozi wake wote waweke wazi kwa Umma Tamko la Mali, Madeni na Maslahi. Kwa kufuata masharti ya Katiba ya Chama Cha ACT Wazalendo natangaza rasmi fomu zangu nilizowasilisha Leo Sekretariat ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
 
Ni matumaini yangu kwamba itafikia wakati Daftari la Rasilimali na Madeni la Viongozi wa Umma litakuwa linawekwa wazi kwa Umma ili wananchi waweze kujua Mali, Madeni na Maslahi ya Viongozi wao na pale ambapo kiongozi ametoa habari zisizo sahihi au kuficha mwananchi aweze kutoa Taarifa kwenye Sekretariat na Baraza la Maadili liweze kufanya kazi yake ipsavyo.
 
Mfumo wa kuweka wazi Rasilimali na Madeni ya Viongozi wa Umma ni mfumo endelevu na muhimu kwenye vita vita dhidi ya ubadhirifu na ufisadi. Mataifa kadhaa duniani hutumia mfumo huu ( public disclosure of leaders’ assets and liabilities) kuwezesha mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi. Nchini Uingereza na Kanada kwa mfano, daftari la matamko ya Rasilimali na Madeni ya Viongozi lipo wazi kwa kila mwananchi kuona na huuzwa kwenye duka la vitabu la Bunge.
 
Namsihi Sana Rais John Pombe Magufuli kusaidia kufanya mabadiliko makubwa ya Sheria ya maadili ya Viongozi ili kurejesha na kuboresha Miiko ya Viongozi katika kuimarisha vita dhidi ya ufisadi nchini. Rais aliahidi kuweka wazi Mshahara wake alipokuwa anazungumza katika kipindi cha 360 cha Clouds TV. 
 
Ninamkumbusha afanye hivyo na pia aweke wazi Mali, Madeni na Maslahi yake ya Kibiashara ili awe mfano kwa Viongozi wengine Nchini.
 
Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto, Mb
Kigoma Mjini
30/12/2016

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

HUYU NDO KIJANA ALIYEMCHOMA MKUKI MKULIMA…AMEKAMATWA LEO.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Polisi Morogoro wafanikiwa kumkamata aliyemchoma mkulima mkuki mdomoni.Wafugaji wa kijiji cha Changalawe kata ya Masanze wilaya Kilosa mkoani Morogoro walioyakimbia makazi yao wakihofia kukamatwa na jeshi la polisi kufuatia tukio la mkulima Agustino Mtitu kuchomwa mkuki mdomoni na kutokea shingoni hatimaye wamerejea makazini kwao huku wakilalamikia baadhi ya mifugo yao kukatwa mapanga na watu wasiojulikana

Wakizungumza baada ya kurejea kutoka porini walikojificha kwa siku tano wafugaji hao wanawake kwa wanaume pamoja na watoto wamesema mtuhumiwa wa kosa la kumchoma mkuki mkulima wamemkabidhi kwenye mamlaka husika na hivyo wameliomba jeshi hilo kuwaacha huru wale wasiokuwa na hatia.

;Akithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei amesema hawatasita kuwakamata wafugaji wote wanaoendelea kusababisha uvunjifu wa amani katika wilya ya Kilosa.

Nao baadhi ya wakulima wamesema kijiji hicho kimekumbwa na hofu kubwa na kwamba familia ya ndugu Mtitu aliyechomwa mkuki nayo ilitoweka na kuomba hifadhi kwa wasamaria wema.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

Kilichosababisha bondia Francis Cheka kufungiwa kucheza ngumi.Fahamu zaidi hapa.

Leo December 30, 2016 Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini (TPBC) imetangaza kumfungia kwa miaka miwili Bondia wa ngumi za kulipwa, Francis Cheka kufuatia kitendo chake cha kugoma kupanda ulingoni kupigana na Bondia Abdallah Pazi “Dullah Mbabe”.

Pambano hilo ilikuwa lifanyike Desemba 25 mwaka huu, katika Ukumbi wa PTA Saba saba jijini Dar es salaam, lililoandaliwa na Promota Siraju Kaike kupitia kampuni yake ya Kaike Promotion.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Katibu Msaidizi wa Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini (TPBC), Chatta Michael amesema kuwa Kamisheni yake ilitoa kibali cha kufanyika kwa mpambano huo baada ya kujiridhisha kuwa taratibu zote zimefuatwa na mabondia wameridhia na kukubaliana na muandaaji, Ila wameshangwaza na Bondia Francis Cheka kugoma kupanda ulingoni kwa madai ya malipo wakati alishasaini mkataba na muandaaji ulioonyesha kuwa ameshachukua kiasi cha shilingi milioni tatu (3,000,000) na baada ya mpambano alitakiwa kupewa kitita chake cha milioni sita.

Amesema kitendo kilichofanywa na Cheka kinaweza kupoteza uaminifu baina ya mabondia na waandaaji wa mapambano, kujiondoa kwa waandaaji katika mchezo huo kwa kuona hakuna uaminifu na pia kinaweza sababisha uvunjifu wa amani kwa watazamaji, iwapo wataendelea kudanganywa uwepo wa mapambano hewa.

Hivyo Kamati ya utendaji ya Kamisheni hiyo iliyokaa Desemba 27, na kupitia kanuni za mchezo huo, imemkuta Bondia Francis Cheka na makosa ya kimakubaliano na kutangaza kumfungia kujihusisha kwa namna yeyote na mchezo huo na kutakiwa kupipa faini ya shilingi laki tano (500,000).


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

Picha : Hali ya mwanamuziki Chid Benz yazidi kuwa mbaya.Fahamu zaidi hapa.

Watu wengi walionyesha kusikitishwa baada ya habari kuenea kuwa mwanamuziki Rashid Mkwiro maarufu Chid Benz ametoroka kwenye nyumba ya matibabu (Sober house) alipokuwa akipatiwa matibabu kutokana na kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya.

Kwa kadiri picha zake zinavyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii inaonyesha dhahiri kuwa mwanamuziki huyo hali yake inazidi kuwa mbaya tofauti na alivyotoka kwenye nyumba ya matibabu ambapo aliweza kurekodi wimbo na pia kutumbuiza katika matamasha kadhaa ya muziki.

Babu Tale aliyekuwa amejitolea kumsaidia awali alisema hawezi kumsaidia tena kwani alishafanya hivyo ikashindikana na kusema Chid Benz ni sikio la kufa.

Licha ya kuwa inadaiwa kuwa hataki kupatiwa matibabu lakini ni dhahiri kuwa kwa hali yake ilivyo sasa anahitaji msaada tena wa haraka zaidi kuweza kuyanusuru maisha yake.

Hapa chini ni picha za hali ya mwanamuziki huyo kwa sasa.



Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

EWURA yakubali ongezeko la bei ya umeme.Fahamu zaidi hapa.


Bei za umeme zimepanda kwa 8.5% badala ya 18.19% iliyopendekezwa na TANESCO.

Ongezeko la bei ya huduma za umeme limetokana na kuzidi kwa gharama za uzalishaji wake.

Shirika la umeme Zanzibar (ZECO) ambalo linanunua umeme wa jumla kupeleka Zanzibar limeongezewa 5.7% ya bei ya umeme.

Ongezeko hilo halitaathiri wateja wa majumbani ambao matumizi yao hayazidi uniti 75 kwa mwezi.

Kundi la TIb linalohusisha viwanda vidogo,mabango na minara ya mawasiliano litakua na tozo ya mwezi ya shilingi 5,520.

Bei hizo zitaanza kutumika Januari Mosi mwaka 2017.

TANESCO inatarajia kufanya maboresho ya msongo wa umeme na kutekeleza miradi mipya ya kuunganisha wateja ili kuboresha huduma za umeme.

IMEANDALIWA NA IDARA YA HABARI (MAELEZO).

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

Urusi Yaapa Kulipiza Kisasi Baada ya Marekani Kuwatimua Wanadiplomasia wa Urusi.Fahamu zaidi hapa.

Urusi imeonya kwamba italipiza kisasi hatua ya rais wa Marekani Barrack Obama ya kuwatimua wanadiplomaisa 35 wa Urusi kufuatia tuhuma kwamba Urusi iliingilia maswala ya uchaguzi wa Marekani kwa njia ya udukuzi wa mitandaoni.

Obama amesema Urusi pia imekuwa ikiwadhalilisha maafisa wa Marekani.

Kwa upande wake, rais mteule Donald Trump ambae mara kwa mara amekuwa akizipuuzilia taarifa hizo za udukuzi, sasa amesema atakutana na wakuu wa kiintellijensia wa Marekani ili kupata undani zaidi wa swala hilo.

Msemaji wa rais Vladmir Putin amesema kuwa hatua zitakazochukuliwa na Urusi zitaiathiri Marekani.

Hatahivyo amesema kuwa Urusi itasubiri hadi rais mteule Donald Trump ambaye amepinga tuhuma hizo za udukuzi atakapochukua mamlaka.

Urusi imekana madai yoyote ya udukuzi na kuvitaja vikwazo hivyo vya Marekani kama visivyo na msingi.

Siku ya Alhamisi, Idara ya maswala ya kigeni nchini Marekani ilitangaza kwamba mabalozi hao 35 kutoka Urusi pamoja na wasaidizi wao huko San Fransisco hawatakiwi  Marekani na kuwapatia wao na familia zao muda wa saa 72 kuondoka nchi humo.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

AFUNGWA Jela Maisha Kwa Kuiba Simu ya Sh 110,000 na Kujeruhi.Fahamu zaidi hapa.

Kesi ya wizi wa simu aina ya Tecno iliyochukua takriban miaka miwili mahakamani, imefika tamati kwa mtuhumiwa kufungwa maisha jela.

Hukumu hiyo ilifikiwa jana katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, baada ya mtuhumiwa Kassim Salum (18) kukutwa na hatia kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia nguvu wa simu yenye thamani ya Sh110,000.

Mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo Januari 28, mwaka jana katika Mtaa wa Ghana Magenge eneo la Buguruni jijini Dar es Salaam.

Ushahidi uliotolewa na mashahidi watano uliiwezesha mahakama kukubaliana na madai ya mlalamikaji Lutifia Mohamed.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Flora Haule alisema, “Baada ya kusikiliza mashahidi wote watano wa upande wa jamhuri, mahakama inaona wamethibitisha mashtaka dhidi ya mshtakiwa.”

Akipitia ushahidi huo, hakimu Haule alisema mshtakiwa alimsukuma mlalamikaji na kuangukia katika karai la mafuta ambalo lilikuwa jikoni.

Mashahidi hao waliieleza jinsi mshtakiwa alivyomvamia mlalamikaji akimtaka atoe simu aliyokuwa nayo na katika purukushani hizo, alimpiga ngumi tumboni hali iliyosababisha kuishiwa nguvu.

Ilielezwa kuwa kutokana na kupigwa, mlalamikaji aliirusha simu upande wa pili ambapo kulikuwa na muuza chipsi, hivyo Salum aliamua kumuachia mlalamikaji ili aende kuifuata.

Hata hivyo, wakati mlalamikaji anajaribu kuokota simu yake, Salum alimsukuma akaangukia katika karai la mafuta ya moto na kumsababishia kuungua eneo lote la mgongoni. Inadaiwa baada ya hapo Salum alichukua simu hiyo na kutoweka nayo.

Wakili wa Serikali, Sylvia Mitanto aliomba mahakama impe adhabu kali Salum ili aweze kujifunza kwa kuwa amemtia mlalamikaji ulemavu wa kudumu.

Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo, mahakama ilitoa nafasi kwa mshtakiwa kujitetea na Salum aliomba isimpe adhabu kali akisema si yeye aliyechukua simu hiyo, bali ni chuki binafsi za mitaani wanakoishi.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

WCB Watembelewa na Waziri wa Mambo ya Ndani.Fahamu zaidi hapa.

Katika kile kinachoonekana viongozi wa serikali kuvutiwa na jinsi Diamond na lebel yake WCB wanavyoibadilisha tasnia ya muziki wa Tanzania kuwa fursa ya kibiashara na kazi rasmi, Mh. Waziri wa wizara mambo ya ndani, Mwigulu Lameck Nchemba ametembelea ofisi za WCB na kukutana na baadhi ya wafanyakazi na wasanii wa label hiyo ili kuwapa moyo na kuwahakikishia kuwa serikali ipo pamoja nao katika kuhakisha kazi zao zinalindwa kwa mujibu wa sheria. Pia kawaambia kuwa serikali haitasita kuwapa msaada pale watakapokwama na kuhitaji usaidizi wa serikali.

Binafsi nimeona ni jambo jema hasa ukizingitia wameshatembelea viongozi na mawaziri kadhaa. Rai yangu kwa wasanii wengine kuiga mfano wa WCB katika kuwa na ofisi maalumu na kuzipa thamani kazi zao.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

Thursday, 29 December 2016

#BREAKING NEWS>>>>BASI LA ABIRIA LAPATA AJALI SINGIDA MUDA HUU.FAHAMU ZAIDI HAPA.

zinasemekana kwamba watu watatu wamefariki dunia  akiwemo Dereva wa bus hilo


Katika maelezo niliyo yapata mke wa Dereva nae alikuwa ndani ya hilo bus ila yey kasalimika.

Lakini amemlilia mume wake mno baada ya kujua amefariki.


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

HII ndiyo Simu ya Milioni 16.5 Anayotumia Bilionea Alhaj Dangote.Fahamu zaidi hapa.

Inasemekana hii ndio simu anayotumia Bilionea Alahaji Aliko Dangote. Inaitwa Nokia Vertu Signature. Bei yake ni kati ya $5000 hadi $7500. Ukibadilisha kwa pesa ya madafu ni kama milioni 16.5Tsh hivi. Alhaji sio mtu wa ki-spoti spoti

Mfanyabiashara huyu raia wa Nigeria anamiliki kampuni tanzu ya mafuta inayofahamika kama Dangote Group yenye makao yake makuu nchini Nigeria.

Kufikia June mwaka 2016 kwa mujibu jarida la Forbers, alitajwa kuwa na ukwasi unaokadiriwa kufikia kiasi cha dola bilioni 15.1 akiwa amewekeza kwenye nchi mbalimbali barani Afrika ikiwemo Tanzania ambapo anamiliki Kiwanda cha kutengeneza ‘Cement’ kilichopo mkoani Mtwara.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

ALIYECHOMWA MKUKI MDOMONI ASIMULIA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

MKAZI wa kitongoji cha Upangwani, Kijiji cha Dodoma Isanga, Kata ya Masanze, wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro, Augustino Mtitu, aliyechomwa mkuki mdomoni na kutokea shingoni, amemshukuru Mungu, madaktari, uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Kilosa na wananchi wa kijiji hicho kwa kuwezesha kunusuru maisha yake.
 
Mkuki huo ulimjeruhi na kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kufanyiwa upasuaji na kufanikiwa kuondolewa mkuki huo na kuokoa maisha yake.
 
Mtitu (42) ambaye ni mkulima alisema hayo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi akiwa wodi namba moja, inayolaza wagonjwa wa majeraha ya ajali katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro.
 
Mkulima huyo na wengine wanane walijeruhiwa katika vurugu zilizohusisha jamii ya wafugaji wa kimasai na wakulima wa kijiji hicho kilichopo katika wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro.
Tukio hilo lililotokea saa 5:00 asubuhi Desemba 25 mwaka huu.
 
Alisema licha ya sasa kuendelea vizuri, alipata maumivu makali kuanzia muda wa kuchomwa mkuki huo na kulazimika kuushikilia mkononi mkuki kuanzia muda huo hadi saa 10:00 jioni ya siku hiyo alipofikishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro na madaktari kumfanyia upasuaji na kuutoa.
 
“Namshukuru Mungu, pia Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen, Mganga Mkuu wa Mkoa, Dk Frank Jacob waliofika kuniona na kunifariji na leo (jana) amenitembelea Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule na baadhi ya ndugu zangu wa kijijini Dodoma Isanga,” alisema.
 
Hata hivyo, hakuweza kuzungumza mwa muda mrefu kutokana na sehemu ya jeraha bado ikiletea maumivu, ingawa alisema si kama yaliyokuwa siku ya kwanza baada ya upasuaji.
 
Katika wodi hiyo, wananchi waliokuwa wakienda kuwaanglia ndugu zao waliolazwa walikuwa wakimiminika eneo la kitanda chake wakimjulia hali na kumpa pole kwa mkasa huo wa aina yake.
 
Naye Stanley Andrea, ndugu wa Mtitu, ambaye yupo katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro akimuunguza nduguye, alisema hali yake inaleta matumaini ya kupona na kwamba kwa sasa anaweza kula vyakula laini.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

MAKUBWA Yafichuka Faru John.Fahamu zaidi hapa.

Maofi sa wa Wizara ya Maliasili na Utalii, wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA), wafanyakazi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na maofi sa Taasisi ya Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) wakiwamo madaktari, wakifanya uchunguzi wa Faru John baada ya kufa katika eneo la Sasakwa Grumeti.


SAKATA la kutoweka kwa faru John lililoibuliwa wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika mikoa ya Arusha na Manyara linazidi kuchukua sura mpya kila kukicha.

Taarifa zilizolifikia MTANZANIA baada ya kufanya uchunguzi wa sakata hilo kwa wiki kadhaa sasa, zinaonyesha kwamba uamuzi wa kumhamisha faru huyo kutoka Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro ulihusisha mamlaka za kitaifa za Serikali.

Habari kutoka vyanzo vya kuaminika zinaeleza kwamba mchakato wa kuhamishwa kwa faru John kutoka Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro kwenda Grumeti, ulianza katika eneo la Nyasirori ndani ya Hifadhi ya Serengeti Aprili 17, 2015.

Uamuzi huo kwa mujibu wa vyanzo vya uhakika serikalini, ulianza siku hiyo hiyo wakati wa tukio la kuwafungulia mbwa mwitu waliokuwa wamehifadhiwa katika eneo maalumu huko Nyasirori.

Vyanzo vya uhakika vya habari vinaeleza kwamba mjadala kuhusu kuhamishwa kwa faru John ulifanyika wakati watendaji wakuu wa taasisi za uhifadhi za Serikali zinazounda Kamati Maalumu ya Kuwalinda Tembo na Faru (National Elephant and Rhino Steering Committee) wakiwapo.

Miongoni mwa watendaji wanaotajwa kuwapo wakati wa mjadala kuhusu kuhamishwa kwa faru huyo kutoka katika Bonde la Ngorongoro kutokana na sababu za kitaalamu, ni Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Bonde la Ngorongoro (NCAA), Dk. Fadhili Manongi na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi.

Wengine ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Wanyamapori (TAWIRI), Dk. Simon Mduma na mwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori aliyefahamika kwa jina la Alex Choya.

Taarifa kuhusu kuwapo kwa haja ya kuhamishwa kwa faru huyo zilipelekwa hadi Wizara ya Maliasili na Utalii.

Kufikishwa kwa suala hilo wizarani kulifuatiwa na hatua ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Adelhem Meru, kuwaandikia barua watendaji wa Mamlaka ya Bonde la Ngorongoro kutekeleza uamuzi huo ifikapo Desemba 31, 2015.

Alipoulizwa kuhusu uwapo wa barua hiyo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, alisema ni kweli barua hiyo ipo kwenye kumbukumbu za wizara.

“Ni kweli hiyo document ipo, lakini hili suala la faru John linafanyiwa kazi na vyombo vya dola. Nadhani si vizuri kulijadili kwa undani sasa, tusubiri matokeo ya uchunguzi,” alisema Waziri Maghembe.

Wahifadhi kadhaa waliozungumza na gazeti hili kutoka Serengeti na Ngorongoro juu ya sakata hilo, walieleza kwamba kiini cha kufikiwa kwa uamuzi huo kulitokana na mabadiliko makubwa ya kitabia aliyokuwa nayo faru John tangu mwaka 2002.

“Faru John alizaliwa ndani ya Ngorongoro, na alianza kuonyesha tabia za ukorofi dhidi ya faru wengine madume mwaka 2002,” alieleza mhifadhi mmoja anayefanya kazi Ngorongoro.

Mhifadhi mwingine alimweleza mwandishi wetu kwamba hali hiyo ilisababisha Mamlaka ya Bonde la Ngorongoro kufanya mawasiliano na TAWIRI kuhusu hatua za kuchukua.

Alisema kuwa hali ilizidi kuwa mbaya na mwaka 2005 kiliitishwa kikao kingine kujadili matatizo ya faru John ambaye tabia yake ya kuwapiga faru wengine ilisababisha wanyama hao kutoka ndani ya Ngorongoro na hivyo kusababisha ugumu wa kuwalinda.

“Tatizo jingine lililotokana na ubabe wa faru John, ni gharama kubwa za ulinzi wa faru waliokimbia vipigo, na kutawanyika hadi kwenye mashamba ya watu.

“Faru wana tabia moja, pindi wanapopigana, yule aliyeshindwa huondoka eneo husika,” alieleza mhifadhi mwingine aliyezungumza na MTANZANIA.

Taarifa kutoka Ngorongoro zinaeleza kuwa mwaka 2013 tatizo la faru John lilizidi kuwa baya zaidi pale kreta, baada ya faru huyo kuua wenzake wawili.

Katika tukio hilo, faru John anatajwa aliua ndama (jike) kwa kumchoma na pembe na kisha akaua dume mwenzake katika mapigano.

Mhifadhi huyo aliliambia gazeti hili kwamba faru John ndiye aliyekuwa na watoto wengi katika Bonde la Ngorongoro kuliko faru mwingine yeyote.

Tukio la faru John kumuua ndama kwa pembe lilitokea wakati alipokuwa akijaribu kumpanda mama yake.

“Faru John alianza kuwapanda watoto wake, jambo ambalo kitaalamu si salama kwa uhai wa faru, hivyo kuendelea kumwacha pale kreta lilikuwa jambo la hatari.

“Baada ya matukio hayo ya 2013, kikao kilikaa tena ambapo TANAPA pia walihudhuria, swali kubwa likiwa ni wapi ambako faru John alipaswa kupelekwa?” alisema mhifadhi mwingine.

Kwa mhifadhi huyo, uamuzi wa kwanza ulikuwa ni kumtoa faru John na kumpeleka katika Hifadhi ya Mkomazi ambako kuna makazi maalumu ya faru (rhino sanctuary).

Hifadhi ya Mkomazi ambako hata hivyo uamuzi huo ulikwama, iko chini ya uendeshaji wa mwekezaji Tony Fitz John.

Kukwama kwa uamuzi huo wa kwanza pia kunaelezwa kulisababishwa na taarifa kwamba katika Hifadhi ya Mkomazi kulikuwa na uwiano sawa kati ya faru madume na majike.

Taarifa nyingine zinasema mwaka huo huo wa 2013, ulifikiwa uamuzi mwingine wa kumkata pembe faru huyo kama njia ya kupunguza madhara aliyokuwa akisababisha katika hifadhi, jambo ambalo lilifanyika.

Wakati wahifadhi wakiumiza vichwa kuhusu nini kifanyike, faru wawili waliokuwa Grumeti, waitwao Limpopo (dume) na Laikipya (jike) walipoteza maisha.

Taarifa zinasema Limpopo aliuawa wakati akipigana na tembo, wakati sababu za kifo cha Laikipya hazikutajwa.

Upungufu huo wa faru wawili ndiyo sababu ambayo baadaye ilisababisha kuzaliwa kwa hoja ya faru John kupelekwa Grumeti kupanda na kuzalisha majike.

Hali hiyo inatajwa kuwa ndiyo iliyosababisha uongozi wa Grumeti inayomilikiwa na tajiri wa Marekani, Paul Tudo Jones, waandike barua ya kuomba faru dume kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori, jambo ambalo lilifanyika.

Vyanzo vya habari kutoka serikalini vinaeleza kuwa baada ya maombi hayo, kilikaa kikao cha Kamati ya Tembo na Faru mjini Dodoma ambacho kilitoa mapendekezo yake kuwa faru John anafaa kwenda Grumeti.

Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni pamoja na usalama wake, gharama kubwa za kumhamisha na suala zima la siasa kuhusu hatua hiyo.

Kwa hiyo taratibu zikaanza, ikiwamo kutafuta madaktari watakaoshiriki kumkamata, ambao miongoni mwao walikuwa kutoka Kenya.

Hatua ya kwanza ya kumhamisha kwa mujibu wa taarifa za wataalamu wa uhifadhi, ilikuwa ni kujengwa kwa banda maalumu ambalo faru John aliingizwa Novemba 7, 2015.

“Unajua kuna taratibu za kuhamisha faru, hamuwezi kumdunga sindano ya usingizi na kumbeba, unaweza kumjeruhi na hata kusababisha kifo, kwa hiyo tulimuacha azoee lile banda kwanza kwa kumuwekea miwa, wanapenda sana miwa.

“Kwa kawaida mkishabeba banda alimo na kuliingiza kwenye gari maalumu, ndipo mnamdunga sindano.

“Kwenye banda hilo alikuwa akiingia na kutoka kwa mwezi mmoja, ilipofika Desemba 8, 2015, ndipo akapelekwa eneo la Sasakwa, Grumeti,” alieleza mmoja wa wahifadhi aliyeshiriki kumhamisha faru huyo.

Mhifadhi huyo alilieleza gazeti hili kwamba kazi ya kumhamisha faru John ilifanywa na watu 56 na magari 15, na baada ya kumfikisha, timu ya madaktari ilibaki Sasakwa kwa siku saba kufuatilia maendeleo yake.

“Kule Sasakwa kwanza aliwekwa kwenye eneo dogo ili iwe rahisi kumfuatilia, lakini ilipofika Januari 8, mwaka huu, alifunguliwa na kuachwa kwenye eneo kubwa la wazi, na afya yake ilikuwa vizuri na alikuwa na mahusiano mazuri na faru jike aliyekuwa eneo hilo,” alieleza mhifadhi mwingine.

Hata hivyo, inadaiwa kuwa faru John alianza kuonekana amezubaa tofauti na uchangamfu wa awali na ilipofika Agosti 20, mwaka huu, hali yake ilibadilika na kuwa mbaya kiasi cha kusimama kwa shida, jambo linalotajwa kuwashtua hata madaktari waliokuwa wakimwangalia.

Inadaiwa alipoteza maisha usiku wa kuamkia Agosti 21.

Mhifadhi huyo alisema kuwa faru John alikufa akiwa na umri wa miaka 38, miaka mitatu zaidi ya wastani wa maisha ya faru ambao ni miaka 35.

Alisema kuwa baada ya kifo chake uchunguzi wa kitaalamu kubaini sababu za kupoteza kwake maisha ulifanyika na kuhudhuriwa na madaktari kadhaa na wanafunzi zaidi ya 50 kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA).

Miongoni wa madaktari wanaotajwa kushiriki ni Dk. Morris Kilewo (TANAPA), Dk. Ernest Mjingo (TAWIRI), Dk. Emmanuel Macha (TANAPA), Dk. Justin Samanche (TAWIRI) na Profesa Donald Mpanduji wa SUA.

Taarifa nyingine zinasema kuwa baada ya uchunguzi huo, pembe mbili za faru John zilikabidhiwa kwa Mhifadhi wa Ikorongo-Grumeti, ambaye ni mtumishi wa wizara ili kuzipeleka Dar es Salaam ambako nyara za Serikali zinahifadhiwa katika jengo la Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii (Mpingo House).

Pia pembe kubwa ya faru John ilikuwa imewekwa kifaa maalumu cha utambuzi (transponder), ambacho hadi sasa kipo ndani ya pembe hiyo, na kinachotakiwa ni kuweka betri na kupata taarifa kuhusu faru huyo, njia ambayo inatajwa kuwa bora kuliko vipimo vya vinasaba (DNA).

Baadhi ya wahifadhi ambao wamehojiwa na kikosi kazi maalumu kilichoundwa na Serikali kuchunguza kile kinachotajwa kuwa “utata kifo cha Faru John”, walisema suala hilo lilipaswa kufanywa na wataalamu wa wanyamapori.

“Jamani hili suala ni la kitaalamu zaidi, sasa tulitarajia iundwe timu ya wataalamu waliobobea katika masuala ya wanyamapori ifanye kazi kwanza, kisha kama kutaonekana kuna kosa la jinai, sasa kikosi kazi kingeingia kazini kuchunguza,” alisema mmoja wa wahifadhi waliohojiwa.

Desemba 6, mwaka huu akiwa ziarani mkoani Arusha, Waziri Mkuu aliuagiza uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, umletee nyaraka zote zilizotumika kumhamisha faru John kutoka hifadhi hiyo ifikapo Alhamisi, Desemba 8.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo alipotembelea ofisi za Makao Makuu ya NCAA zilizopo wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha na kuzungumza na watumishi wa mamlaka hayo pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafugaji, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo.

Saa 7 usiku Desemba 9, Waziri Mkuu alipokea taarifa inayoelezea utaratibu uliotumika kumhamisha faru John kutoka Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Sasakwa Black Rhino Sanctuary iliyoko katika Hifadhi ya Grumeti.

Akizungumza katika kikao kilichofanyika nyumbani kwake Oysterbay, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Maghembe na baadhi ya watendaji wa wizara yake, Waziri Mkuu alisema taarifa hiyo itafanyiwa kazi na wataalamu wa ofisi yake.

Akisoma taarifa hiyo mbele ya Waziri Mkuu, Profesa Maghembe alisema hadi kufikia Desemba 2015 wakati faru John anahamishwa, alikuwa na watoto 26 (sawa na asilimia 70.2) ya faru wote waliokuwapo ndani ya kreta.

“Kati ya faru 37 waliokuwapo ndani ya kreta, watoto wake walikuwa 26 sawa na asilimia 70.2. Uamuzi wa kumwondoa John ulikuwa ni muhimu, ili kuwezesha kuongezeka kwa faru weusi na kupunguza tatizo la ‘inbreeding’ ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro.”

Baada ya kuhamishiwa Sasakwa, Waziri Maghembe alisema Julai 10, mwaka huu afya ya faru John ilianza kudorora na alikufa Agosti 18, mwaka huu. Taarifa hiyo iliandaliwa na Kamati ya Taifa ya Kuwalinda Tembo na Faru.

Akikabidhi pembe za faru huyo mbele ya Waziri Mkuu, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Kupambana na Ujangili wa Wanyamapori, Robert Mande, alimweleza kwamba pembe kubwa ya faru John ilikuwa na uzito wa kilo 3.6 na ndogo ilikuwa na uzito wa kilo 2.3.

Mbali ya Waziri Mkuu kupokea ripoti na pembe za faru huyo, lakini siku tatu baada ya agizo hilo, maofisa watano wa NCAA wanaotuhumiwa kushiriki kumwondoa faru John kutoka katika kreta hiyo walikamatwa kwa mahojiano, ili kujua ukweli kuhusu mazingira ya kupotea kwake.

Pia Waziri Mkuu aliituhumu menejimenti na wafanyakazi wa NCAA kuwa imejaa vitendo vya rushwa na wizi na asingeweza kuvumilia sakata la faru John, ambaye alisema kuwa aliuzwa kwa Sh milioni 200 kwenye Hoteli ya Grumeti iliyo Hifadhi ya Serengeti na kuwa walipokea fedha za awali Sh milioni 100.

Waziri Mkuu alisema anataka kumwona faru huyo, nyaraka za kumhamisha na kama amekufa basi apelekewe hata pembe ofisini kwa kuwa anajua pa kuzipeleka.

Alisisitiza kuwa ikibainika kuna ambao wamekiuka taratibu watawajibika.
Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

VIDEO: Mchungaji Mtikila Aonekana Akiwa Hai Msukule.

VIDEO: Mchungaji Mtikila Aonekana Akiwa Hai Msukule
Bonyeza kuangalia Video:


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

Viongozi Chadema Arusha Wakamatwa Na Polisi.Fahamu zaidi hapa.

JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha linawashikilia watu 12, wakiwemo viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Arusha.

Viongozi hao walikamatwa kwa amri ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo wakituhumiwa kuhusika kuchoma moto mashine za kuvuta maji kutoka kwenye chanzo cha Kangdet wilayani Karatu kwa madai kwamba wanatekeleza agizo la Serikali, hatua ambayo imeelezwa kuwa haikufuata utaratibu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Arusha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo, aliwataja waliokamatwa kuwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Karatu, Moshi Darabe ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Barai, anayedaiwa kuhamasisha wananchi kuchoma moto mashine hizo zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 16.

Wengine waliokamatwa ni Diwani wa Kata ya Mang’ola, Lazaro Emanuel, viongozi wa vijiji vya kata hizo pamoja na baadhi ya wananchi.

Kamanda Mkumbo alisema kuwa msako wa kuwakamata watuhumiwa wengine waliohusika na tukio hilo bado unaendelea na uchunguzi utakapokamilika watafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria.

Desemba 27, mwaka huu, kundi la wananchi wa vijiji vinne vya  kata hizo waliandamana, wakang’oa na  kuchoma moto mashine za kuvuta maji katika chanzo cha  maji cha Kangdet, kinachotegemewa na  vijiji vingine vya Kata ya Barai.

Kutokana na tukio hilo, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ikiongozwa na mwenyekiti wake ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Gambo, walitembelea eneo la tukio na baada ya viongozi kueleza kilichotokea, aliagiza kukamatwa kwa watu wote waliohusika na uharibifu huo.

“Sheria lazima ichukue mkondo wake kwani agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa lilikuwa wazi na halikusema wananchi wachukue sheria mkononi, jambo hili ni kinyume cha sheria,” alisema Gambo katika mkutano huo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Jubilate Mnyenye (Chadema), amesema kuwa yeye, mbunge wa jimbo hilo, Willy Qambalo na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mang’ola, Jacob Pius, wametakiwa kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi jijini Arusha leo asubuhi kwa mahojiano kuhusu tukio hilo.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

Washitakiwa Wanne Mauaji wa Dr. Mvungi Waachiwa Huru.Fahamu zaidi hapa.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru washitakiwa wanne kati ya 10 waliokuwa wanakabiliwa na mashitaka ya mauaji ya bila  kukusudia ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk Sengondo Mvungi.

Washitakiwa walioachiwa ni Masunga Makenza (40), mkazi wa Tabata Darajani, Zacharia Msese (33), Ahmad Kitabu (30) mkazi wa Mwananyamala na John Mayunga (56).

Waliachiwa kwa mujibu wa Kifungu Namba 91 Kifungu kidogo cha kwanza cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA). Wakili wa Serikali, Pamela Shinyambala alidai mbele ya Hakimu Mkazi Thomas Simba kuwa upande wa mashitaka umeshasajili jalada hilo Mahakama Kuu.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Mshitaka Nchini (DPP), hakuwa na nia ya kuendelea kuwashitaki washitakiwa hao kwa mujibu wa kifungu hicho. Awali, Shinyambala alidai kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutolewa maelezo ya mashahidi baada ya upelelezi wa kesi hiyo kukamilika.

Hakimu Simba alisema anawaachia washitakiwa hao, kama walivyoomba upande wa mashitaka. Alisema kwamba washitakiwa sita, ndio watakaosomewa maelezo hayo ya mashahidi.

Washitakiwa hao ni Longishu Losingo (29), Paulo Mdonondo (30) mkazi wa Tabata Darajani, Mianda Mlewa (40) Mkazi wa Vingunguti, Juma Kangungu (29) mkazi wa Vingunguti, Msungwa Matonya (30), mkazi wa Vingunguti na Masenga Mateu.

Hata hivyo, Hakimu Simba aliutaka upande wa mashitaka, kuhakikisha kwamba wanaleta cheti cha kifo cha mshitakiwa wa kwanza, Chibago Magozi (32), mfanyabiashara mkazi wa Vingunguti Machinjioni.

Pia alieleza kuwa kesi hiyo ikienda mahakama kuu, bila ya kupelekwa mahakamani hapo cheti cha kifo, itakwama kwa kuwa hawawezi kusoma maelezo hayo hadi kwa mtu aliyekufa.

Aliwataka kuhakikisha katika tarehe ijayo ambapo washitakiwa sita watasomewa maelezo, wawe wamewasilisha cheti cha kifo.

Hata hivyo, Wakili Shinyambala alikubaliana na maelezo hayo na kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasomea washitakiwa waliobaki maelezo ya mashahidi. Kesi imepangwa Januari 10, 2017.

Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram