Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inampongeza
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kupiga
marufuku matumizi ya Shisha na uvutaji wa Sigara hadharani kama afua ya
kupunguza madhara ya tumbaku na madawa ya kulevya katika jamii.
Uchunguzi
wa kitalaam uliofanyika umebaini kuwa Shisha ina madhara kwa afya ya
watumiaji hasa vijana na watoto. Watumiaji wa Shisha wanatumia kiwango
kikubwa cha tumbaku kwa muda mfupi, hali inayoongeza madhara yatokanayo
na tumbaku kama vile: – Saratani, Magonjwa ya Mapafu, Kibofu cha mkojo,
Tezi dume, Koo, Mdomo na Kiywa, Ngozi, Ini, Ubongo.
Pia
imebainika kwamba matumizi ya Shisha huambatana na kuongezewa dawa
nyingine za kulevya na hivyo hufanya watumiaji wa Shisha kupata uraibu
wa dawa za kulevya. Matumizi ya dawa hizo za kulevya ni kosa la jinai.
Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inapenda kurejea
na kusisitiza agizo lake la tarehe 12 Machi 2015 la kuzuia matumizi ya
sigara na matumizi ya bidhaa za tumbaku katika maeneo ya umma
Inakumbushwa
kwamba agizo hili limezingatia utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa
Bidhaa za Tumbaku, Sura ya 121 T.L 2002, ya Sheria za Tanzania kipengele
cha 12 (1) ambacho kinakataza matumizi ya Tumbaku katika Maeneo ya
Umma.
Madhumu
ya Agizo hili ni kuilinda Jamii kwa ujumla kutokana na madhara
yatokanayo na moshi wa sigara. Wizara inawakumbusha wananchi wanaotumia
bidhaa za tumbaku kupunguza au kuacha kabisa matumizi ya tumbaku. Aidha,
agizo hili linaijumuisha jamii yote katika kubaini madhara ya tumbaku
na umuhimu wa kuzuia matumizi ya tumbaku katika maeneo ya kazi na maeneo
yote ya umma.
Agizo hili linawahusu wananchi wote nchini wanaopata huduma katika maeneo ya umma kama ilivyotafsiriwa na sheria husika.
Matumizi
ya tumbaku hayaruhusiwi katika maeneo yote ya umma. Maeneo haya
yanajumuisha ofisi zote za Serikali na tasisi zake zote, watu binafsi,
vyuo, vituo vya huduma za Afya zikiwemo Hospitali, vituo vya Afya na
zahanati, vituo vya usafiri wa Anga, Mabasi, bandari na treni, sehemu za
mikutano, mapumziko, bustani na fuko za
maji,sherehe,michezo,masoko,maduka makubwa pamoja na sehemu za
kuabudu.Na kwa mtu yeyote anayeendesha shughuli katika maeneo ya umma
analazimika kutenga eneo maalum kwa ajili ya wavuta sigara.
Kwa
kuwa Mhe. Waziri mwenye dhamana na masuala ya Afya nchini ameona hatari
hii ya Uvutaji wa sigara na utumiaji wa bidhaa za tumbaku kwa afya ya
Wananchi, kuanzia leo tarehe 4/7/2016 matumizi ya Shisha nchini
yamepigwa marufuku kwa wote wanaojihusisha na matumizi hayo, na kwa
wafanyabiashara wote wanaojihusisha na upatikanaji wa Shisha nchini
Hivyo
basi, kwa agizo hili katika maeneo yote nchini ambako matumizi ya
Shisha hufanyika ni marufuku matumizi hayo kuendelea kutumika.
Aidha vyombo vya Dola na mamlaka husika vinahimizwa kusimamia kwa ukamilifu katazo hili.
0 comments:
Post a Comment