TAARIFA KWA UMMA
KUKANUSHA TAARIFA KWAMBA BODI HAINA FEDHA
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kukanusha taarifa za upotoshaji zinazoenezwa kwa sasa kwamba haina fedha.
Si kweli kwamba Bodi haina fedha, ila ni kweli kwamba kumekuwa na
ucheleweshaji wa kufikisha fedha za wanafunzi vyuoni kutokana na zoezi
la kuhakiki wanafunzi wanaonufaika na mikopo linaloendelea vyuoni hivi
sasa.
Hata hivyo, maandalizi ya malipo hayo yameshafanyika na ‘pay sheets’
zimeshapelekwa vyuoni tayari kwa wanafunzi wanaonufaika na mikopo
kusaini.
Bodi inatarajia wakati wowote wiki ijayo baada ya zoezi la uhakiki kukamilika; itapeleka fedha hizo vyuoni.
IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
TAREHE 2 JULAI 2016
0 comments:
Post a Comment