Mbunifu huyo wa mavazi ameiambia Bongo5 kuwa kwa sasa yeye na Wema Sepetu ni kama kaka na dada na sio meneja wake tena.
“Mimi kum-meneji Wema nimemaliza kama miaka miwili iliyopita, mkataba uliishia hapo, lakini tukasimama kama mtu na kaka yake,” alisema Martin. “Kwa hiyo umeneja ule wa ukaka na udada upo mpaka tunaingia kaburini lakini kama umeneja wa mkataba uliisha na ukabaki ule umeneja wa imani baada ya kuaminiana,”
“Tuliona hakuna umuhimu wa kuwa na mikataba kwa sababu tayari tumeshaaminiana, kwa sababu sasa hivi mimi Wema nimeshamchukulia kama ndugu yangu na yeye kama kaka yake. Kwahiyo kugombana kupo lakini baadaye mnawekana sawa na maisha yanaendelea,”
Aliongeza,
“Ukaribu wa mimi na Wema umepungua kwa sababu mimi kwa sasa nafanya mambo yangu na yeye anafanya mambo yake kwa sababu zamani Wema alikuwa anafanikiwa sana nakuniacha mimi nikiwa pale pale, kwa hiyo sasa hivi kila mtu anafanya mambo yake hatuwezi kuwa tunajenga kwake halafu kwangu kunaungua,”
Katika hatua nyingine mbunifu huyo wa mavazi amewataka mashabiki wake wa fashion kusubiria mambo mazuri kutoka kwake.
0 comments:
Post a Comment