WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe,
amesema kikosi cha Everton FC kitatua nchini Julai mwaka huu kukipiga
dhidi ya Simba au Yanga katika mechi maalum zilizoandaliwa na serikali
ili kutangaza vivutio vya utalii nchini.
Mwakyembe alisema uongozi wa timu hiyo inayoshika nafasi ya saba katika
msimamo wa Ligi Kuu ya England (EPL) ikiwa na pointi 58 baada ya mechi
35, umeweka sharti kwamba utacheza dhidi ya timu itakayoibuka mshindi
katika mechi maalum ya kirafiki kati ya Simba na Yanga.
Waziri huyo aliyasema hayo bungeni mjini hapa jana alipowasilisha hotuba
yake kuhusu utekelezaji wa bajeti ya wizara yake kwa mwaka huu wa fedha
na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka ujao wa fedha.
Alisema ili kuimarisha michezo na kuvitangaza vivutio vya utalii
vilivyopo nchini, mwaka ujao wa fedha wizara yake kwa kushirikiana na
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, itahakikisha
inawasiliana na Balozi zilizopo Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Italia,
Uholanzi, Ubelgiji, Urusi, China, Japan, Jamhuri ya Korea, Canada na
Marekani kwa lengo la kuzikaribisha klabu kubwa za soka za nchi hizo
kuja nchini.
"Tayari tuna uzoefu wa ziara ya wachezaji wa kimataifa wastaafu wa timu
ya mpira wa miguu ya Real Madrid ya Hispania ambao walicheza na
wachezaji wastaafu wa timu yetu ya Taifa jijini Dar es Salaam mwaka 2014
na kupata fursa ya kutembelea vivutio vyetu vya utalii," alisema.
"Ziara ya timu hiyo ilitangazwa dunia nzima kupitia vyombo mbalimbali vya habari ikiwa ni pamoja na CNN, BBC na Supersport.
Alisema ujumbe wa timu hiyo tayari umeshakuja Tanzania mara mbili ndani
ya mwaka huu, mara ya kwanza kujadiliana na wizara na kukagua Uwanja wa
Taifa na miundombinu yake na mara ya pili kujiridhisha kuhusu ubora wa
nyasi za uwanja huo.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment