VIONGOZI zaidi ya 20 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ngazi ya kata na
matawi Jijini Arusha wamesimamishwa uongozi kwa tuhuma za kufuja mali za
chama.
Kata ambazo viongozi wake wamesimamishwa kwa tuhuma hizo za
ubadhirifu ni Unga Limited, Themi, Sekei, Sombetini na Daraja Mbili.
Viongozi hao ni wenyeviti, makatibu, wachumi na makatibu wenezi.
Katika kata ya Unga Limited, mbali ya viongozi wa kata kuchukuliwa
hatua pia viongozi wa matawi wa wamesimamishwa kwa madai ya kushindwa
kusimamia ipasavyo mali za chama.
Mbali ya tuhuma za kufuja mali za chama, baadhi ya viongozi hao pia
wanatuhumiwa kufanya hujuma katika chaguzi zilizopita, ikiwa ni pamoja
na kuficha fomu kwa wanachama wanaotaka kuwania uongozi ili wao waweze
kuwania tena nafasi hizo na kupita bila ya kupingwa ama kuwa na wagombea
dhaifu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana, Katibu wa
Uenezi na Itikadi wa CCM, Humphrey Pole pole alisema na kutoa salamu kwa
watendaji wote wa chama hicho kote nchini kuhakikisha wanatunza mali na
kuzitumia kwa uaminifu na uadilifu mkubwa.
Polepole alisema katika baadhi ya maeneo mali za chama zinatafunwa
kama mchwa na viongozi mbalimbali hivyo msako unaendelea kote nchini
kuwasaka na bila ya kuonea mtu.
Katibu huyo alisema chama hakiwezi kuwavumilia viongozi wanaofuja
mali kwa sasa chini ya uenyekiti wa Rais John Magufuli. “Wote
watachukuliwa hatua kali,” alisema.
“Kuna baadhi ya maeneo mali za chama zinatumika vizuri sana… kuna
baadhi ya maeneo mengine viongozi wanafuja vibaya lakini wameachwa.
“Kwa sasa hilo halipo.
“Heri kuwa na viongozi wachache waaminifu na waadilifu wenye
kufuata katiba ya chama kuliko kuwa na utitiri wa viongozi wezi na
wasiokuwa waaminfu. Hilo haliko kwa sasa chini ya uongozi wa (Rais)
Magufuli.”
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza HapaFollow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment