Nahodha Msaidizi wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC,
Himid Mao ‘Ninja’, anaendelea na majaribio yake kwenye kikosi cha
Randers FC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Denmark.
Himid tayari ameshafanya mazoezi mara kadaa mpaka sasa toka awasili ndani ya kikosi hiko cha Randers.
Kwa mujibu wa mtandao wa klabu hiyo, umeeleza kuwa kiungo huyo nyota
mkabaji wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, 24, yuko tayari kwa
mara ya kwanza kucheza soka la kulipwa na kulipa kisogo soka la nyumbani
kwa kuhakikisha anapata mkataba wa kusajiliwa na Randers.
Nyota huyo ambaye atafanya majaribio ndani ya timu hiyo kwa siku 10,
aliondoka nchini Jumatatu iliyopita baada ya pande zote mbili za timu
hizo kufanya makubaliano kuhusu mchezaji huyo,
Mara baada ya kumaliza zoezi hilo atarejea mara moja Azam FC kabla ya
taratibu nyingine kufuata kama watakuwa wamevutiwa na huduma yake.
Habari njema ni kuwa mbali na kufanya mazoezi na Randers, pia anatarajia
kucheza mchezo mmoja akiwa na kikosi cha wachezaji wa akiba wa Randers
kitakachocheza na AC Horsens Jumanne ijayo kwenye Ligi ya Wachezaji wa
Akiba ndani ya Ligi Kuu ya Taifa hilo ‘Danish Superliga’.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment