Ofisi kuu ya Rais wa Nigeria imethibitisha kuwa wanafunzi 82 wa shule ya
wasichana wa Chibok, waliotekwa nyara na wanamgambo wa kiislamu wa Boko
Haram mnamo mwaka wa 2014, wameachiwa huru.
Maafisa wanasema kuwa waliachiwa huru, kufuatia majadiliano ya muda
mrefu na ubadilishanaji washukiwa wa Boko Haram, waliokuwa wamezuiliwa
na wakuu wa nchi hiyo.
Wasichana hao ni miongoni mwa zaidi ya wanafunzi wanafunzi 270
waliotekwa nyara kutoka shule ya malazi katika mji wa Chibok ulioko
kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Wasichana hao wote 82 kwa sasa wanalindwa na jeshi la Nigeria mahali
salama, baada ya kuletwa kwa barabara kutoka maeneo ya ndani kabisa
vijijini, hadi katika kambi ya jeshi ya Banki, karibu na mpaka na
Cameroon, hayo ni kwa mjibu wa mwaandishi habari wa BBC Stephanie
Hegarty kutoka Lagos.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment