JENGO la makao makuu ya Klabu ya Yanga lililoko makutano ya mtaa wa
Jangwani na Twiga Kariakoo jijini Dar es Salaam, liko hatarini kupigwa
mnada kutokana na deni la Sh. milioni 300 ambalo klabu hiyo inadaiwa,
imefahamika.
Taarifa zilizopatikana jana jijini zinaeleza kuwa Kampuni ya Udalali ya Msolopa ndiyo imepewa mamlaka ya kusimamia mnada huo.
Akizungumza jana jioni, Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa,
alithibitisha kuwapo kwa deni hilo na kueleza kuwa uongozi umeanza
utaratibu wa kulifanyia kazi suala hilo.
Mkwasa alisema kuwa deni hilo limetokana na malimbikizo ya ada ya
jengo la kiwanja kinachomilikiwa na klabu hiyo, lakini wanaamini
watalilipa kabla ya mchakato huo wa kunadi jengo hilo la makao makuu
haujafanyika.
“Ni kweli kesi iko katika Mahakama ya Ardhi na tumeshaanza
kuifanyia kazi,” alisema kwa kifupi Mkwasa, kocha na mchezaji wa zamani
wa timu hiyo.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment