Msanii wa filamu, Steve Nyerere, amedai wasanii wa filamu wanashindwa
kufanikiwa kutokana na kukosa ushirikiano huku akidai kuna baadhi yao
wanajifanya wao ni mungu watu.
Muigizaji huyo amedai hakuna mtu wa nje ambaye ataweza kuja kuikomboa tasnia yao ya filamu isipokuwa wao wenyewe.
“Leo hatupo katika umoja, kwanza ili tuweze kufanikiwa mafanikio hayapo
ya mmoja mmoja, mafanikio yote duniani yalipita kwa watu ndiyo wewe
ukafanikiwa kwa hiyo lazima tukubaliane, tupendane na nyoyo zetu ziwe
zimefunguka kwa kufanya vitu vizuri,” Steve alikiambia kipindi cha Enewz
cha EATV.
Aliongeza, “Kuna ma-director wazuri zaidi lakini leo wote hawapo,
wanachokikosa ni ushirikiano, tunao ma-director wazuri tu, wanaweza
wakafanya kitu kizuri tu ‘site’ lakini ushirikiano hawana, kuna watu
wanakuwa Mungu watu haiwezekani, haiwezekani kuwa Mungu mtu jamani Mungu
ni mmoja tu,”
Muigizaji huyo amekuwa akipingana na wasanii wenzake wa filamu
walioandamana mwezi mmoja uliopita wakiishinikiza serikali kuzifungia
filamu za nje ambazo hazilipi kodi kwa madai zinawaharibia soko lao la
filamu za ndani.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment