Friday, 4 August 2017

Tarime: John Heche(Mb), Akamatwa na Polisi Kwa Tuhuma za Kuhamasisha Bangi na Uvamizi wa Mgodi.

Polisi wamefika Nyumbani kwa Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche,
sasa Hivi wa naomba kuchukua simu zake zote na wanamueleze Kuwa anatuhumiwa kwa kuchochea wananchi kuvamia Mgodi wa ACIACIA. Kosa la Pili analotuhumiwa nalo ni Kuhamasisha Kilimo cha bangi. Alipokuwa kwenye Mkutano wa hadhara Silali, aliwaambia wananchi kwamba atapeleka Hoja binafsi bungeni ili bangi iwe zao la Biashara. Kwa sasa yupo chini ya Ulinzi.

=> Polisi Wamechukua simu moja na Ipad ila kakataa kuwapa Password.

=> Vilevile Polisi Wamemtaka Esther Matiko Mbunge wa CHADEMA Tarime Mjini, Kujisalimisha Polisi aunganishwe kwenye kesi ya Heche kwani na yeye alikuwepo kwenye Mkutano wa Silali.


UPDATES;1630hrs

Hatimaye Mbunge John Heche aachiwa kwa dhamana. "Wamemwachia Heche ila wamechukua simu zake zote na kumtaka afike polisi Jumatatu kwa mahojiano. Leo amekataa kuchukuliwa maelezo yoyote kwa kuwa hakuwa amekwenda Polisi kwa mambo hayo bali kushughulikia kukamatwa kwa Katibu wake, hivyo amejidhamini na kuondoka ila simu zimebaki Polisi"


Source:Jamii Forums


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Related Posts:

  • Polisi Wakamata Machungwa Yaliyoibiwa. Polisi wa huko jijini Seville nchini Hispania wakamata watu watano jana baada ya kufukuzana nao kwa kasi na ndipo hapo polisi waligundua tani hizo za machungwa zilizoibiwa ambazo watuhumiwa walikuwa wameyajaza ndani ya m… Read More
  • Hii Ndio Gharama ya Passport za Kielektroniki. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt.  Mwigulu Nchemba amesema kuwa gharama mpya ya hati ya kusafiria ya kielektroniki itakuwa Sh. 150,000. Dk Nchemba amesema hayo leo  wakati wa uzinduzi wa Hati ya kusafiria y… Read More
  • Kampuni ya TTCL Yafutwa. Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Makame Mbarawa, amesema kuwa anamshukuru sana Rais Magufuli kwa kuona umuhimu wa kuona wa kuwa na shirika la mawasiliano madhubuti kwa ajili … Read More
  • TANZIA: Mzee Kingunge Ngombale Mwiru Afariki Dunia. Mzee Kingunge Ngombale–Mwiru amefariki dunia alfajiri ya leo.Tupo hapa na masikitiko makubwa.Poleni sana sana wafiwa na kijana wake Kinje (Mama yake alifariki 4/1/2018 na Baba yake leo)May his soul Rest in Eternal Peace. D… Read More
  • TCRA Yafafanua Matuzi ya Alama za Vidole Kwenye Usajili wa Laini. “Ndugu mteja katika kuboresha usajili wa laini za simu alama za vidole zitatumika kuanzia Februari 5, 2018. Kwa mawasiliano zaidi tembelea maduka yetu,” ni ujumbe ambao watumiaji mbalimbali wa mitandao ya simu nchi wamet… Read More

0 comments:

Post a Comment