1.
Moja kati a viambato vilivyopigwa marufuku kutumika kama kipodozi ni aina ya
“steroids” ambazo kimsingi ni dawa, mfano wa viambato hivi ni pamoja na
“Clobetasol” na “Betamethosone” zinazopatikana katika dawa aina ya MOVATE,
BETACIRT-N, DIPROSON, GENTRISONE, n.k
2. Bidhaa hizi zinaendelea kutumika kama dawa za cheti (prescription only medicine) na lazima zitolewe kwa wagonjwa wa ngozi kwa kufuata maelekezo ya kidaktari na mfamasia. Hata hivyo, haziruhusiwi kutumika kama vipodozi.
3. Dawa nyingine zilizopigwa marufuku kutumika kama vipodozi nizile za kuongeza makalio na maziwa. Hii ni kutokana na kusadikiwa kuwa huleta madhara kwa watumiaji ikiwa ni pamoja na kuhatarisha kupata ugonjwa wa kansa.
4. Kutokana na madhara hayo ya kiafya na kiuchumi yanayoweza kusababishwa na matumizi ya mikorogo na vipodozi vyenye viambato sumu, TFDA imeweka mifumo ya kiuthibiti wa vipodozi ili kuhakikisha kuwa vipodozi vinatumiwa na wananchi ni bora na salama. Hii ni kwa kuhakikisha kuwa vipodozi hivi havina viambato vyenye sumu vinavyoweza kudhuru afya ya mtumiaji.
5. Mifumo ya uthibiti wa vipodozi inajumuisha usajiri wa vipodozi, udhibiti katika uingizaji, ukaguzi na ufuatiliaji na utoaji wa vibali vya biashara ya vipodozi kama ilivyoainishwa.
MADHARA YATOKANAYO NA
MATUMIZI YA VIPODOZI VYENYE VIAMBATO VYENYE SUMU
1. BITHIONOL
Kupata mzio wa ngozi/allergic na athari kwenye ngozi ikiwa itapata mwanga wa jua.
2. HEXACHLOROPHENE
- Inapenya kwenye ngozi na kuingia kwenye ishipa ya fahamu na kusababisha ugonjwa wa mishipa ya fahamu hasa kichwani.
- Pia inasababisha ugonjwa wa ngozi na kuathirika kwa ngozi pindi unapokuwa kwenye mwanga wa jua.
- Kwa watoto wachanga husababisha uhalibifu kwenye ubongo
- Vile vile ngozi inakuwa laini na kusababisha kupata ugonjwa kama fangasi kwenye ngozi au maambukizi ya vimelea vya maradhi.
3. ZEBAKI (MERCURY)
- Husababisha madhara ya ngozi, ubongo, figo na viungo, mbalimbali vya mwili
- Zebaki inapopakwa kwenye ngozi kuweza kupenya taratibu ndani ya mwili na kusababisha sumu yake kuingia kwenye damu na kusababisha madhara mwengi mwilini.
- Mama mjamzito akitumia vipodozi vyenye zebaki mtoto huathirika akiwa akiwa bado tumboni na huzaliwa akiwa na mtindio wa ubongo.
- Husababisha ngozi kwa laini na kuwa na mabaka meusi na meupe
- Husababisha mzio/ allergic wa ngozi na muwasho
- Sumu iingiapo kwenye mishipa ya fahamu husababisha ugonjwa wa mishipa ya fahamu.
- Sumu ya zebaki ikiingia mwilini kwa kiwango kikubwa husababisha madhara maka upofu, uziwi, upotevu wa fahamu wa madhara mara kwa mara.
4. VINYI CHLORIDE
- Inasababisha kansa ya maini, ubongo, mapafu na mfumo wa damu
- Sumu pia husababisha kuumwa kichwa, ksikia kizunguzungu na kupoteza fahamu
5. ZIRCONIUM
Husababisha kansa ya mapafu na ngozi
6. HALOGENATED SALICYLANILIDE
Husababisha kansa ya mapafu na ngozi
6. HALOGENATED SALICYLANILIDE
- Husababisha mzio wa ngozi mara inapopata mwanga wa jua
- Husababisha ugonjwa wa ngozi
7. CHLOROQUINONE
- Kundi zima la vipodozi vya CHLOROQUINONE hutumika kutengenezea vipodozi lakini kiambato ambacho kinachotumika ziaid ni kiambato cha Hydroquinone.
8. HYDROQUINONE
- Husababisha muwasho wa ngozi, mzio wa ngozi, kansa, kuchubuka kwa ngozi na kusababisha mabaka meusi na meupe.
9. STEROIDS
- Steroids ni kundi la homoni, homoni hizi hutenganezwa kwenye miili ya binadamy na wanyama. Pia zinaweza kutengenezwa nje ya mwili wa binadamu yaani bandia (artificial). Katika kundi hili, corticosteroids ndizo hutumika sana kama viambato kwenye vipodozi.
- Steroids zikitumika kwa muda mrefu husababisha madhara mbalimbali kaam, ugonjwa wa ngozi na kutokwa na chunusi kubwa. Pia ngozi huwa nyembamba sana na laini na endapo ngozi itapata jeraha au kufanyiwa upasuaji kidonda hakitapona. Pia husababisha magonjwa ya moyo.
10. CHLOROFORM
- Husababisha kansa ya utumbo mpana na kibofu cha mkojo
- Husababisha ugonjwa wa akili na ugonjwa wa mishipa ya fahamu
- Kwenye ngozi, chloroform husababisha ngozi kuungua, maumivu makali, ngozi kuwa nyekundu sana na kutokwa na vipele.
11. CHLOROFLUOROCARBON (HALOGENATED CHLOROFLUOROALKANES)
- Husababisha madhara kwenye mishipa ya katikati ya fahamu na hivyo kusababisha mtu kutopumua vizuri
- Husababisha kichefuchefu, kutapika, kuumwa na kichwa, kusikia usingizi na kusikia kizunguzungu.
12. METHYLENE CHLORIDE
- Husababisha satarani/kansa (cancer)
- Husababisha madhara kwenye mishipa ya kati ya fahamu, kwenye maini na kwenye mishipa ya moyo.
Pamoja
na madhara ya kiafya yaliyotajwa hapo juu pia kuna madhara mengine ya kiuchumi
yanayoweza kuambatana na matumizi ya vipodozi visivyo na ubora na usalama kwa
mtumiaji.
- Kwanza ni gharama za matibabu pale mtu anapopata madhara
- Lishe kwa watoto na familia kwa ujumla hupungua kwa sababu pesa nyingi hutumiak kununua vipodozi au mikorogo.
Mamlaka
ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), inapenda kuwaasa watumiaji wa vipodozi na
wananchi kwa ujumla kujiepusha na matumizi ya vipodozi vilivyopigwa marufuku
kwani huleta madhara ya afya kwa mtumiaji.
0 comments:
Post a Comment