Monday, 7 September 2015

#YALIYOJIRI>>>IKULU:Rais Jakaya Kikwete akiwapa pole wagonjwa waliokuwa wamelazwa wodi moja na majeruhi leo.Jionee Picha hapa.


Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimpa pole  mmoja wa majeruhi Bi Flora Maduka akiwa kitandani pake hospitalini hapo baad ya kujeruhiwa katika msongamano huo.
Mmoja wa majeruhi Bw. Kokoliko Ramadhani akiwa kitandani pake hospitalini hapo akiuguza bega la kuume aliloumia kwenye msongamano huo.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya  Mkoa wa Morogoro Dkt. Ritha Lyamuya alipokwenda kuwapa pole majeruhi walioumia katika msongamano mkubwa uliotokea katika mlango wa kutokea nje baada ya mkutano wa kampeni wa CCM katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana Septemba 6, 2015. Watu wawili walipoteza maisha, akiwemo mvulana wa miaka 12 aliyejulikana kwa jina la Ramadhani Abdallah na mwanamama Grace George (42), ambapo jumla ya watu 17 walijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini hapo. Hadi jioni hii majeruhi saba walikuwa wameruhusiwa
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Kaimu Mganga Mku wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro Dkt. Samson Tarimo alipokwenda kuwapa pole majeruhi walioumia katika mlango wa kutokea nje baada ya mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana Septemba 6, 2015.
  Rais Kikwete akimpa pole  mmoja wa majeruhi Bw. Kokoliko Ramadhani akiwa kitandani pake hospitalini hapo akiuguza bega la kuume aliloumia kwenye msongamano huo.
  Rais Kikwete akimpa pole  mmoja wa majeruhi Bi. Jalia Mohamed akiwa kitandani pake hospitalini hapo akiuguza bega la kuume aliloumia kwenye msongamano huo.
IKULU:Rais Jakaya Kikwete akiwapa pole wagonjwa waliokuwa wamelazwa wodi moja na majeruhi leo. 
  Picha za zaidi.
Toa maoni yako hapa.

0 comments:

Post a Comment