Hadithi ya Tanzania na Argentina inaweza
ikawa moja ila tofauti ikawa wahusika. Wakati Messi akiachana na Timu
ya Taifa ndio muda mwafaka kwa Tanzania kuthamini mchango wake kwa
taifa.
Mengi yatazungumzwa lakini ukweli wa
mambo ni maelewano hafifu yaliyopo kati ya viongozi wa Shirikisho la
Soka Argentina AFA na Timu ya Taifa. Muda mfupi kabla ya timu kwenda
Marekani wachezaji walitaka kugoma kwa madai kwamba AFA haipo upande wao
na imekuwa ikifanya mambo kwa maslahi binafsi na sio kwa faida ya mpira
na taifa.
Hapa ndipo tunarejea nyuma wakati
Samatta na Ulimwengu wanacheza TP Mazembe. Kuna wakati walikuwa majeruhi
lakini Watanzania waliwasakama kuwa hawana mapenzi na taifa. Lakini pia
kuna wakati walicheza na Timu ya Taifa haikufanya vizuri wakaambiwa
wanacheza chini ya kiwango.
Siamini kama Samatta anaweza kuvumilia
haya ipo siku atavaa viatu vya Messi na kuamua kuachana na Timu ya
Taifa. Mfano mzuri alivyokosa penati kwenye mechi na Misri alisakamwa
kwa katuni na misemo ya kila aina ikiwemo msemo wa uliovuma wa “Penati ya Mwendokasi”.
Mchezaji kama Messi hawezi kuyumbishwa
na matokeo lakini akikosa ushirikiano ndio pale anapoamua kujiweka kando
huku moyoni akidhamiria kuonyesha pengo lake kwa wanaobeza uwepo wake
ndani ya kikosi cha taifa.
0 comments:
Post a Comment