Monday 11 July 2016

#YALIYOJIRI>>>Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan awataka wanawake kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.Fahamu zaidi hapa.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan amesema ukuosefu wa fedha, taarifa pamoja na ujuzi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ni vikwazo vinavyoendelea kuongeza umaskini nchini ambapo wanawake ndio waathirika wakubwa.

Mama Samia aliyasema hayo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizindua mradi wa Green Voices ambao unakusudia kuwasaidia wanawake katika kupambana na mabadiliko ya tabia nchi ambapo wamegeuza changamoto kuwa fursa.

“Wote tumeshuhudia jinsi Bara la Afrika linavyopoteza mabilioni ya shilingi kila mwaka kutokana na mabadiliko ya tabia nchi”. Alisema Mama Samia.
 
Awali Rais wa Mfuko wa Wanawake Afrika Mama Maria Terezo la Vega Fernandes alisema atahakikisha anatimiza dhamira yake ya kuendelea kuwasaidia wanawake wa Tanzania na Afrika katika maeneo ya kilimo, afya, Amani na haki za binadamu.

“ Miradi ya Green Voices imeanzishwa katika nchi mbalimbali duniani kwa lengo la kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi na kujiletea maendeleo yao”. Alsema Mama Tereza.

Naye mjumbe wa Bodi ya ushauri wa mradi huo Balozi Getrude Mongela alimpongeza mama Tereza kwa juhudi zake za kuwaunganisha wanawake katika kuleta maendeleo na ukombozi wao kwa ujumla.

“Mradi wa Green Voices umenikumbusha maazimio ya mkutano wa Reo De Jenairo uliofanyika mwaka 1992, mkutano wa Cairo na Beijing ambayo ilizingatia ushirikishwaji wa wanawake katika suala zima la mazingira”. Alisema Balozi Mongela.

Naye mratibu wa mradi huo nchini Bi.Sechelela Balisydia amesema wanawake 15 kutoka Tanzania walipata mafunzo ya jinsi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na uongozi nchini Spain.

Aliongeza kuwa baada ya mafunzo hayo wameweza kutoa kutoa mafunzo kwa wenzao 250 kwa kuwashirikisha katika miradi ya ufugaji nyuki, mitambo ya kukaushia mboga inayotumia nishati ya jua na kilimo cha uyoga.

Miradi hiyo ipo katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Kigoma, Mwanza, Morogoro na Kilimanjaro ambapo mradi huo mpaka sasa umetimiza mwaka mmoja

0 comments:

Post a Comment