Umoja
wa Vijana CCM (UVCCM) umeingia katika mvutano mkubwa na Baraza la
Vijana wa Chadema (BAVICHA) kuhusu Mkutano Mkuu Maalum wa chama hicho
tawala uliopangwa kufanyika Julai 23 mwaka huu mjini Dodoma.
UVCCM
wameionya BAVICHA kuhusu mpango wao wa kutaka kukusanyika mjini Dodoma
siku hiyo kwa lengo la kuzuia mkutano huo kwa madai kuwa unakiuka amri
halali ya polisi ya kupiga marufuku kufanyika kwa mikutano yote ya
kisiasa nchini.
Onyo
hiyo limetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamda Shaka
ambaye aliwaambia waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuwa
watawakabili kwa nguvu zote BAVICHA endapo wataamua kuendesha siasa
zinazolenga kuvuruga amani na kuleta hofu katika jamii na kutishia
maisha.
Alisema umoja huo hautaona shaka kutumia mbinu zilizotumiwa na wapiganaji wa Maumau miongo kadhaa iliyopita nchini Kenya.
“Hatutaona
muhali kupita njia zilizotumiwa na wapiganaji wa Maumau wa Kenya ili
kukihami chama, kulinda viongozi wake na kupigania hadhi na heshima
yetu,” alisema Kaimu Katibu Mkuu huyo wa UVCCM.
CCM
inatarajia kufanya mkutano mkuu maalum Julai 23 mwaka huu ambapo Rais
John Magufuli atakabidhiwa rasmi uenyekiti wa chama hicho kutoka kwa
mtangulizi wake, Dk. Jakaya Kikwete.
0 comments:
Post a Comment