RAIS WA TFF, JAMAL MALINZI
Kuonyesha kweli Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) haliko makini, ni baada ya kuipangia mechi ya Yanga dhidi ya JKT Ruvu kuchezwa kesho Jumatano, halafu ndani ya saa tatu, likaahirisha tena na kutoa taarifa itachezwa keshokutwa Alhamisi.
Mechi
hiyo ya mwisho ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara ilikuwa kiporo,
TFF ikaipangia kuchezwa Jumatano na ikatoa taarifa kwa vyombo vya habari
saa 9:31 Alasiri.
Lakini ilipofika Saa 12:33 ikiwa ni saa 3 na dakika 3, TFF ikatangaza kwamba mechi hiyo sasa itachezwa Alhamisi.
Hii
ilikuwa ni baada ya JKT inayomilikiwa na Jeshi, kutia mkwara na kusema
haitacheza mechi hiyo na TFF ikagundua iliboronga na kuufyata.
Soma taarifa zote...
TAARIFA YA LEO SAA 12:33 JIONI
Wakati
michezo miwili ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ikifanyika kesho
Jumatano Novemba 9, 2016, mchezo kati ya Young Africans na Ruvu Shooting
utafanyika Alhamisi Novemba 10, 2016 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es
Salaam, imefahamika.
Mchezo
huo umesogezwa mbele kwa siku moja kwa sababu Ruvu Shooting imechelewa
kutoka Bukoba mkoani Kagera ambako Jumapili iliyopita ilicheza na Kagera
Sugar katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limejiridhisha kuwa Ruvu Shooting
imechelewa kuingia kituo cha Dar es Salaam, ndiyo maana mchezo dhidi ya
Young Africans umesogezwa mbele.
Michezo
mingine ya kesho Jumatano inahusisha timu za Mwadui ya Shinyanga na
Azam FC ambayo ilipewa jina la Mechi Na. 57 itachezwa Uwanja wa Mwadui
wakati Simba itasafiri hadi Mbeya kucheza na Tanzania Prisons katika
mchezon Na. 60 Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine.
Mechi
zilipangiwa ratiba, lakini tarehe zake hazikupangwa (TBA). Tayari Bodi
ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), imewasiliana na wahusika kuhusu mabadiliko
hayo.
Sababu
ya kuvuta nyuma michezo hiyo ni kutoa nafasi ya maandalizi ya kambi ya
timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayotarajiwa kusafiri Ijumaa wiki hii
kwenda Harare Zimbabwe kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa
unaotarajiwa kufanyika Novemba 13, maka huu.
TAARIFA YA LEO SAA 9:31 ALASIRI
Zile
mechi tatu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara za raundi ya Nane Duru
la Kwanza, sasa zitafanyika kesho Jumatano Novemba 9, 2016.
Michezo
hiyo inahusisha timu za Mwadui ya Shinyanga na Azam FC ambayo ilipewa
jina la Mechi Na. 57 itachezwa Uwanja wa Mwadui wakati Simba itasafiri
hadi Mbeya kucheza na Tanzania Prisons katika mchezon Na. 60 Uwanja wa
Kumbukumbu ya Sokoine.
Mchezo
mwingine utazitanisha Young Africans ya Dar es Salaam itakuwa mwenyeji
wa Ruvu Shooting ya Pwani kwenye Uwanja wa Uhuru jijini katika mchezo
Na.59.
Mechi
zilipangiwa ratiba, lakini tarehe zake hazikupangwa (TBA). Tayari Bodi
ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), imewasiliana na wahusika kuhusu mabadiliko
hayo.
Sababu
ya kuvuta nyuma michezo hiyo ni kutoa nafasi ya maandalizi ya kambi ya
timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayotarajiwa kusafiri Ijumaa wiki hii
kwenda Harare Zimbabwe kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa
unaotarajiwa kufanyika Novemba 13, maka huu.
0 comments:
Post a Comment