Kwa mujibu wa sheria za Urais Marekani, ili mgombea athibitishwe kuwa mshindi wa kiti cha Urais inabidi apate sio chini ya kura 270 kutoka kwa wajumbe hao 538 ambao huamua mshindi kwa namna watu walivyopiga kura katika majimbo mbalimbali.
Wakati wa uchaguzi wa mwaka 2012, Barrack Obama alipata ushindi baada ya kuchaguliwa kwa kura zaidi ya Milioni 65 za raia wa nchi hiyo huku mpinzani wake Mitt Romney akipata zaidi ya Milioni 60 ambapo baada ya kura za Wajumbe kupigwa, Obama alipata ushindi wa Wajumbe 332, Romney 206.
Wakati kura zimeshaanza kupigwa nchini humo inaelezwa kuwa kuna majimbo ambayo ni ngome ya chama cha Republican sawa na Democratic lakini kuna majimbo mengine kama Florida, Pennsylvania na Ohio ambayo hayana mshindi wa jumla, hayo ndio majimbo ambayo yataamua mshindi.
Pamoja na kumchagua Rais siku ya leo Jumanne raia wa Marekani wanapiga kura kuwachagua wawakilishi 435 watakaofanya kazi kwa muda wa miaka miwili.
0 comments:
Post a Comment