Thursday 15 December 2016

DILI LA MBUYU TWITE KWENDA MAJIMAJI LABUMA, YAELEZWA AMEPATA OFA NJE.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Usajili wa beki Mbuyu Twite kwenda Majimaji ya Songea umeingia ruba baada ya kukwama katika hatua za mwisho.

Majimaji ilifikia hatua nzuri ya mazungumzo na Twite, lakini baadaye katika hatua za mwisho suala hilo likashindikana.

Hadi saa sita na dakika moja usiku, Majimaji haikuwa imetuma jina la Twite katika majina yake ya usajili.

Imeelezwa, imeshindikana baada ya Twite kupata ofa hiyo ya nje ya nchi ingawa bado haijawa wazi ni nje wapi.

Twite raia wa DR Congo, ameachwa na Yanga ili nafasi yake aichukue Justice Zulu, kiungo mkabaji kutoka nchini Zambia.



Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

 

0 comments:

Post a Comment