Friday 16 December 2016

#EXCLUSIVE>>>>HATIMAYE YAMETIMIA, NGASSA AMWAGA WINO KUKIPIGA MBEYA CITY.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Baada ya vuta nikuvute ya hapa na pale, hatimaye mshambuliaji Mrisho Ngassa ametua Mbeya City.


Ngassa amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea Mbeya City, maana yake itakuwa naye katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.

Blog hii ya SALEHJEMBE ilianza kukuletea hatua kwa hatua kuanzia safari ya Ngassa kutoka jijini Dar es Salaam kwenda Mbeya kufanya mazungumzo na uongozi wa Mbeya City, baadaye makubaliano na jana usiku jina lake lilivyotumwa kuwahi dirisha dogo la usajili kabla halijafungwa na mwisho usajili wake.

Ngassa anatokea Fanja ya Oman ambayo alijiunga nayo baada ya kuvunja mkataba wake na Free State Star ya Afrika Kusini.

Hata hivyo, Fanya ameichezezea si zaidi ya mechi tatu akafunga bao moja lakini akaumia, baadaye akalazimika kurejea Tanzania na baadaye amesaini Mbeya City.


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

 

0 comments:

Post a Comment