Tuesday 13 December 2016

KATIKATI YA LA LIGA, BARCELONA YATUA QATAR, YAITWANGA AL AHLI YA SAUDI ARABIA 5-3 NA KURUDI NYUMBANI USIKU.FAHAMU ZAIDI HAPA.

FC Barcelona imeitwanga Al Ahli ya Saudi Arabia kwa mabao 5-3 katika mechi ya kirafiki iliyomalizika hivi punde huko Doha, Qatar.
Katika mechi hiyo ya kirafi, Luiz Suarez, Lionel Messi na Neymar kila mmoja alifunga bao moja kabla ya wote watatu kutolewa katika dakika ya 32.
Kocha Luis Enrique aliwatoa wakali wake hao kwa kuwa wana mechi ngumu ya La Liga Jumapili dhidi ya Espanyol ambayo hujulikana kama Catalan Derby.

Barcelona iliongoza kadi kwa mabao 5-1 baada ya  Paco Alcacer na Rafinha kila mmoja kufunga katika kipindi cha pili.

Lakini Al Ahli nao walijitutumua na kupata mabao hayo matatu kupitia kwa Omar Abdulrahman ambaye ni mwanasoka bora wa Bara la Asia,  na Muhannad Assir aliyepiga bao mbili.


Barcelona ilitua Qatar jana, leo imecheza mechi na baada ya hapo, wachezaji wake wameingia kwenye ndege kurejea Barcelona.




Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

 

0 comments:

Post a Comment