Benchi
la ufundi la Simba chini ya Kocha Mkuu, Joseph Omog, limeridhishwa na
kiwango cha kiungo Mghana, James Kotei ambaye amepewa mwaka mmoja.
Kiungo
huyo maarufu kama Mzima Swichi, anamudu kucheza nafasi ya kiungo
mkabaji, nafasi anayocheza nahodha, Jonas Mkude, hivyo kuzua sintofahamu
ya nani aanze kwenye nafasi hiyo.
Omog
amezima maswali hayo kwa kusema kuwa licha ya wote kucheza nafasi moja,
bado anaweza kuwatumia kwa pamoja, muhimu ni kucheza na aina ya mfumo
kulingana na mechi husika.
Hata
hivyo, Mcameroon huyo tangu atue Simba amekuwa akitumia mfumo wa 4-4-2
au 4-5-1 lakini hajawahi kutegemea viungo wawili wakabaji, jambo ambalo
litaonekana kwa Mkude na Kotei iwapo atawatumia wote.
“Kweli
Kotei naye ni kiungo mkabaji, lakini nafasi ya Mkude kama nahodha ipo
palepale, awali sijui nini kilitokea kati yake na uongozi hadi
akachelewa kambini lakini bado Mkude ana nafasi yake.
“Pia
wanaweza kucheza wote katika mechi moja kulingana na mfumo
nitakaoutumia. Siwezi kuutaja maana hiyo ni sawa na kumpa silaha adui,
lakini ukweli bado wanaweza kucheza kwa pamoja,” alifunguka kocha huyo
wa zamani wa Azam FC kwenye mahojiano maalum.
Wakati huohuo, Kocha
Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja ‘Mia Mia’, amesema hawatishiki na
rekodi mbovu za watani wao, Yanga kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona wa
Ndanda ambako hawajawahi kushinda.
Amesema hayo wakati Simba ikitarajiwa kucheza dhidi ya Ndanda, keshokutwa Jumapili katika Ligi Kuu Bara.
“Sisi
hatuchezei rekodi, muhimu ni kuandaa timu kuhakikisha inashinda katika
mazingira yoyote, haijalishi ugenini ama nyumbani.”
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
Bonyeza Hapa CLICK HERE
0 comments:
Post a Comment