Wizkid anakabiliwa na kifungo cha miaka 11 jela, baada ya mahakama ya Uganda kutoa hati ya kukamatwa kwake na meneja wake, Sunday Aare.
Wizkid alishindwa kutokea kwenye show iliyokuwa ifanyike December 3
mwaka huu mjini Kampala. Kampuni iliyomlipa, Face TV, kupitia
mwanasheria wake, Fred Muwema, imepata kibali cha kumkamata muimbaji
huyo kwa kuchukua dola $60,000 na kushindwa kutokea kwenye show. Gharama
zingine walizotoa ni brokerage fee, $5,000 na per die, $3,000 kwa muda
ambao Wizkid angekaa Uganda.
Muimbaji huyo alidaiwa kushindwa kusafiri na ndege toka Marekani kwenda nchini humo kwa show hiyo.
“Between 29th August 2016 and 29th November 2016, our client (Face
TV) paid to Mr. Sunday Are, Wizkid’s manager the full performance fee of
US$60,000, a brokerage fee of US$5,000 and US$3,000 being per diem for
the days they were going to stay in Uganda,” yanasomeka maelezo ya
mlalamikaji.
Zaidi ya watu 25,000 walikuwa wamenunua tiketi kwaajili ya show
hiyo. Maelezo yaliyowasilishwa mahakamani yameeleza kuwa mwandaaji wa
shiw hiyo amekula hasara ya zaidi ya $300,000 kutokana na maandalizi
aliyofanya.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
0 comments:
Post a Comment