Vilio na simanzi zimetawala katika kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu 2
pamoja na dereva mmoja waliopoteza maisha kwa ajili ya gari Jumamosi
hii huko mkoani Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan yuko mjini Arusha muda huu ambapo anaongoza wananchi wa mkoa huo pamoja na mikoa ya jirani katika kuuaga miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili pamoja na dereva Mmoja wa shule ya Lucky Vincent iliyopo mkoani humo.
Wanafunzi na walimu hao walipata ajali hiyo wakati wanaenda kwenye shule iitwayo Tumaini kwa ajili ya kufanya mitihani wa ujirani mwema baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kutumbukia korongoni kwenye eneo la Rhotia wilayani Karatu.
Mama akisaidiwa na watu wa msalaba mwekundu baada ya kuanguka.
Ni simanzi na vilio.
Baadhi ya wazazi wakisadiwa.
Baadhi ya viongozi wakiwa katika msiba huo.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment