Matajiri wa Ufaransa, Klabu ya soka ya Paris Saint-Germain yaweka mezani
dau la Euro Milioni 70 kwa klabu ya Borussia Dortmund ili wapate
saini ya mshambuliaji wa kimataifa wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang.
Taarifa kutoka ndani ya PSG zinakanusha habari hizo zilizoandikwa na
gazeti la Bild la nchini Ujerumani kwamba mzaliwa huyo wa Ufaransa,
ambaye amefunga jumla ya mabao 35 msimu huu, tayari amekutana na
Mkurugenzi wa Soka wa PSG, Patrick Kluivert mjini Paris.
Aubameyang, mwenye umri wa miaka 27, kama dili hilo litafanikiwa,
atakuwa anaingiza kitita cha Euro Milioni 14 kwa msimu akitua PSG, pato
ambalo ni mara mbili ya mshahara wake wa sasa.
Taarifa zinasema kuwa Dortmund inajipanga kupokea ofa ya PSG msimu
utakapomalizika baada ya fainali ya Kombe la Ujerumani Mei 27 dhidi ya
Eintracht Frankfurt.
Kwa upande wa mchezaji huyo mara kwa mara amesikika akisema kuwa anataka
kujiunga na kikosi cha Mfaransa, Zinedine Yazid Zidane,”Zizou” , kocha
wa klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment