Kampuni ya michezo ya kubahatisha
SportPesa imezinduliwa leo na moja kwa moja imemwaga Sh milioni 50
kuisaidia timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti
Boys.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema ni jambo zuri kwa SportPesa
kuonyesha wanajali kwa kiasi kikubwa na Serengeti Boys inahitaji msaada
wa wadau kama ambavyo imefanya kampuni hiyo kutoka Kenya.
Serengeti Boys italiwakilisha taifa la Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho itakayofanyika nchini Gabon.
Uzinduzi wa kampuni maarufu ya michezo
kubahatisha ya SportPesa uliofanyika leo jijini Dar es Salaam,
uliwakutanisha wadau mbalimbali wa michezo na burudani.
Kampuni hiyo imeahidi kusaidia mambo mbalimbali katika udhamini wa michezo hapa nchini ikiwa ni sehemu ya kusaidia mabadiliko.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment