Ndoto za Barcelona kutetea taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya
msimu huu kimepotea baada ya jana kukubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa
Atletico Madrid katika mchezo mkali wa robo fainali uliochezwa katika dimba la
Vincent Calderon,Madrid Hispania.
Mabao yote mawili ya Atletico Madrid yalifungwa na Antoine Griezmann aliyeipeleka
timu yake nusu fainali ya ligi ya mabingwa kwa ushindi wa jumla ya mabao 3-2.
Licha ya Barcelona kutawala mchezo huo waliishia kutengeneza
nafasi chache tu kutokana na ukuta imara wa vijana wa Diego Simeone ambao
walikaba timu nzima nan a kufanya mashambulizi
ya kushtukiza mara kwa mara kitu ambacho kilikiweka kwenye wakati mgumu
kikosi cha Luis Enrique.
Atletico Madrid walipa bao lake la kwanza katika dakika ya
36 ya mchezo mfungaji akiwa Griezmann ambaye alimalizia kwa kichwa krisi safi
ya “Outer” iliyopigwa na kiungo wa kihispania Saul na kumuacha kipa wa Barcelona
Marc-Andre ter Stegen akiwa hana la kufanya.
0 comments:
Post a Comment