Home »
Habari Moto
» #YALIYOJIRI>>>>Mchina Anyongwa Ndani ya Gari Dar es Salaam.Fahamu zaidi hapa.

Mfanyabiashara
raia wa China aliyetambulika kwa jina la Luo Dongpeng (32), maiti yake
imekutwa ndani ya gari lenye namba za usajili T145 DFY Machi 28, mwaka
huu maeneo ya Kijitonyama, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar,Uwazi
linakupasha.
Taarifa
zilizopatikana kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo wanaoishi maeneo
aliyokutwa Mchina huyo zinaeleza kuwa, gari la marehemu huyo walianza
kuliona hapo tangu alfajiri ya siku hiyo lakini kadiri muda ulivyokuwa
ukienda ndivyo walivyozidi kulitilia shaka maana hakukuwa na mtu
aliyetoka ama kuingia.
Waliendelea
kusema kwamba ilipofika saa 10.00 jioni walilazimika kulisogelea na
kuchungulia ndani ndipo walipomuona mtu akiwa amelala kiti cha nyuma,
walipomwamsha hakuamka wala kujigeuza ndipo waliwaarifu polisi wa Kituo
cha Mabatini Kijitonyama.085A9757
Moja ya msumali uliokuwa umetegwa kwenye gari hilo.
Mashuhuda
hao walidai kuwa huenda Mchini huyo aliuawa kisha kutelekezwa na gari
lake maeneo hayo kwani alikuwa na michubuko mikononi na shingoni.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Alphonce Fuime alipohojiwa na
gazeti hili wiki iliyopita ofisini kwake alikiri kutokea kwa mauaji
hayo.
“Huyu
marehemu inaonekana alikuwa akitoka casino na uchunguzi wa awali
unaonesha aliuawa sehemu nyingine na akutupwa hapo.Tunaendelea na
uchunguzi kuwasaka watu aliokuwa nao casino kwa mara ya mwisho,” alisema
Kamanda Fuime aliyefafanua kuwa mwili huo ulipelekwa kuhifadhiwa
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Related Posts:
Breaking News>>>Mwanamuziki PAPA WEMBA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKA JUKWAANI.Fahamu zaidi hapa.
Mwanamuziki
nguli wa Congo Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba maarufu kama Papa
Wemba amefariki dunia huko Abidjan, Ivory Coast, usiku wa kuamkia leo.Habari
zilizotufikia hivi punde zinasema marehemu Papa Wemba amefia … Read More
#YALIYOJIRI>>>Serikali Yapangua Hoja Moja ya UKAWA.Fahamu zaidi hapa.
SIKU
moja baada ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kususa kuchangia hotuba
za bajeti, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Florence Mwanri,
amesema serikali haikukosea kuipa Wizara ya Ujenzi fedha zaidi ya
zilizok… Read More
#YALIYOJIRI>>>>NAPE AZINDUA TAMASHA LA KIMATAIFA LA FILAMU MJINI ARUSHA.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Waziri wa
Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akifunua pazia
kuashiria uzinduzi wa Tamasha la kimataifa la filamu la Tanzanite mjini
Arusha.
Waziri wa
Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nap… Read More
#YALIYOJIRI>>>RAIS MAGUFULI AWASHTUA WENGI,STAILI YAKE YA KUIBUKA MTAAANI YAWAPA HOFU KUBWA.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Rais John Pombe Magufuli akiwasalimia walemavu.Stori: Ojuku Abraham, Risasi JumamosiDAR
ES SALAAM: Staili inayotumiwa na Rais John Pombe Magufuli kuibuka
katika maeneo mbalimbali mitaani pasipo kutarajiwa, inaonekana kuw… Read More
DIAMOND NA ZARI WAWA KIVUTIO AFRIKA KUSINI KATIKA UZINDUZI WA VIDEO YA MAFIKIZORO.FAHAMU ZAIDI HAPA.
You
become powerful when you don't let people steal your joy &
happiness or let negativity affect you or your life. Stay unbothered and
you'll stay happy
When
she's got your back like that after your perf… Read More
0 comments:
Post a Comment