Ukimya wa aliyekuwa mgombea wa Urais wa UKAWA,Edward Lowassa
umezua mjadala kwenye mkutano wa Kamati Kuu ya CCM.Kikao cha Kamati Kuu
kimefanyika jana hapa Dodoma.
Mjadala ulianza pale Mwenyekiti Kikwete alipochagiza maelezo
yake ya chama kuendelea kufanya maandalizi ya chaguzi zijazo na
kutobweteka. Mwenyekiti alisema kuwa Lowassa bado ana uungwaji mkono na
nguvu ya kisiasa na hutumia ukimya kujijenga zaidi.
Mwenyekiti alionya kuwa Lowassa hakufika mwisho na chama
chapaswa kuutazama ukimya wake wa kuchangia na kutoa hoja juu ya
Serikali ya Rais Magufuli kwa jicho la tatu. Wajumbe wote wa KK
walikubaliana na Mwenyekiti Kikwete.
Wakati huohuo,Rais Magufuli ameaswa kuwa ‘mpole kiasi’
atakapoukwaa uenyekiti wa taifa wa CCM mnamo mwezi Juni mwaka huu.
Imesemwa kuwa wanachama wa chama cha siasa hutendewa mambo kwa upole ili
wabaki chamani na kukijenga chama. KK imeunga mkono hatua za Rais na
Serikali yake kutumbua majipu!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
0 comments:
Post a Comment