Home »
Habari Moto
» #YALIYOJIRI>>>Mhasibu Mkuu wa Jeshi la Polisi Asimamishwa Kazi Kwa Kosa la Kulipa Malipo Hewa .Fahamu zaidi hapa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira amemsimamisha kazi Mhasibu Mkuu
wa Jeshi la Frank Charles Msaki kutokana na makosa ya kufanya malipo
hewa yaani kulipa posho ya chakula kwa watu ambao si askari.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizarani hapo ambayo nakala tumeipata, Mhasibu Mkuu huyo Bw. Frank Msaki anasimamishwa kazi kwa kufanya malipo ya kiasi cha
sh. 305,820,000 kama posho ya chakula kwa watu ambao sio askari kwa
kipindi cha kuanzia mwaka wa fedha 2013/2014 hadi 2015/2016.
Meja
Jenerali Rwegasira amesema kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za
Kijeshi anayetakiwa kulipwa posho ya chakula yaani ‘ration allowance’
ni askari peke yake na si mtu mwingine yeyote yule.
Meja
Jenerali Rwegasira amesema anamsimisha kazi Mhasibu Mkuu huyo tangu leo
tarehe 9 Julai, 2016 ili kupisha uchunguzi ufanyike juu ya tuhuma
zinazomkabili.
Katibu Mkuu huyo amesema baada ya jalada la
uchunguzi kufunguliwa na Ukaguzi Maalumu kufanywa na Mkaguzi wa Ndani wa
Jeshi la Polisi imebainika kuwa mbinu mbalimbali zimetumika ili
kufanikisha malipo hayo hewa.
Related Posts:
#YALIYOJIRI>>>>ACT-Wazalendo walaani kauli ya Serikali kutowajengea wananchi......Wadai kauli hiyo ni fedheha kwa waathirika na Wadau.Fahamu zaidi hapa.
Watanzania
wanakumbuka kuwa mnamo tarehe 10 Septemba, 2016 lilitokea tetemeko la
ardhi katika eneo la Kanda ya Ziwa na hususan Mkoa wa Kagera.
Tetemeko hilo lilisababisha athari mbalimbali zikiwemo vifo, majeruhi,
uhari… Read More
#YALIYOJIRI>>>TB Joshua Afunguka 'issue' ya kumtabiria Clinton Ushindi Marekani Ambao Uligonga Mwamba.Fahamu zaidi hapa.
Mhubiri mashuhuri raia wa Nigeria TB Joshua amevunja kimya baada ya
utabiri wake kuwa mgombea urais nchini Marekani Hillary Clinton
angeshinda, kugonga mwamba.
Mhubiri huyo alikejeliwa kwenye mitandao ya kijamii wakati u… Read More
#YALIYOJIRI>>>Kulikoni Ikulu, Serikali na CCM Wanachelewa Kutoa Majibu ya Tuhuma za Msingi Kama Hizi?..Fahamu zaidi hapa.
Ndugu wapendwa, kumezuka tuhuma nyingi wiki iliyopita...kwanza ilikuwa
ya mhe. Mbowe bungeni, ya wabubge hupewa ten M, akanyamazishwa.
Tukasubiri tamko la chama tawala kimya, serikalini kimya, ikulu kwa rais kimya hadi le… Read More
#YALIYOJIRI>>>Rais Dkt. Magufuli Akutana Na Kufanya Mazungumzo Na Rais Mstaafu Wa Afrika Kusini Thabo Mbeki Ikulu.Fahamu zaidi hapa.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Thabo Mbeki mara baada ya
kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Ta… Read More
#YALIYOJIRI>>>>Wadaiwa Sugu Bodi ya Mikopo wapewa siku 30.Fahamu zaidi hapa.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa
bodi hiyo Abdul-Razaq Badru amesema kuwa hadi sasa kuna jumla ya
wadaiwa sugu 142,470 wenye mikopo ya shilingi 239,353,750,170.27
iliy… Read More
0 comments:
Post a Comment