KATIKA kile kinachoweza kusemwa kama KUMKUBALI KIANA Rais Dr
Magufuli,Mbunge wa Iringa Mjini kupitia CHADEMA,Mch Peter Msingwa leo
hii amekutana na kusalimiana na Rais Magufuli wakati wa kukabidhi
madawati.
Kwa tukio hilo,Mbunge huyo ambaye ni miongoni mwa wabunge waliowahi
kumkosoa hadharani Rais Magufuli pamoja na Serikali yake,alionekana
kuwa na bashasha na furaha wakati akisalimiana na Mhe Rais.
Ikumbukwe kuwa wabunge na viongozi wanaounda umoja wa katiba ya
wananchi UKAWA kwa nyakati tofauti walinukuliwa wakisema kuwa
hawamtambui Rais Magufuli,huku wengine wakidiriki kumuita ni Dikteta.
0 comments:
Post a Comment