Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva kutoka lebo ya WCB, Harmonize ameweka
wazi kiasi cha pesa anachoingiza kupitia mtandao wa Youtube kwa Mwezi .
Harmonize amesema watu wanashangaa kuona anatembelea magari ya kifahari
ila hawajui tu kuwa muziki unampa Connections nyingi kwani mbali na show
pia anaingiza mkwanja mrefu kupitia mtandao wa Youtube ambapo
amefunguka kuwa anaingiza kiasi cha Dola za Kimarekani 3,500 kwa mwezi.
“Namshukuru Mwenyezi Mungu Kupitia muziki umenikutanisha na watu
wengi,Umenipa Dili napata riziki kwenye njia tofauti tofauti,sio tu
kwenye show,licha ya kufanya show nauza nyimbo zangu kwenye
Platform,Mimi akaunti yangu ya Youtube kila mwezi nalipwa Dola
3,500“Amesema Harmonize kwenye mahojiano yake na kipindi cha leo tena
cha Clouds FM.
Harmonize kwa sasa ambae anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Niambie’
anatarajia kuanza Tour yake ya muziki wikiendi hii mkoani Mtwara.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment