Friday, 5 May 2017

‘Wapo' ni baba lao katika nyimbo zangu zote - Nay wa Mitego.

Msanii wa muziki wa hip hop, Nay wa Mitego amedai wimbo wake ‘Wapo’ ni wimbo ambao umefanya vizuri kwa muda mchache kuliko nyimbo zake zote alizowahi kuziachia katika maisha yake ya muziki.

Rapa Nay wa Mitego akiwa kwenye moja kati ya shows zake za hivi karibuni.

Akiongea na Bongo5 Alhamisi hii, Nay wa Mitego amesema hata show zake zinajaza zaidi kuliko kipindi cha nyuma kutokana na wimbo huo.

“Nimeshatoa nyimbo zikawa kubwa, nimeshatoa nyimbo watu wakawa wanaimba, nimeshotoa nyimbo zikawa gumzo lakini ‘Wapo’ ni kiboko,” alisema Nay wa Mitego.

Aliongeza, “Ni wimbo ambao umefanya vizuri kila sehemu hata kwenye show mikoa yote niliyozunguka mambo yamekuwa ni mazuri sana. Kwahiyo naweza kuthubutu kusema Wapo ni kazi kubwa kuliko hata kazi zangu zote,”

Rapa huyo ambaye anatarajia kufanya show ya ‘Wapo Night’ mwezi huu katika ukumbi Dar Live jijini Dar es salaam, amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwaajili ya remix ya wimbo huo.

Katika hatua nyingine, rapa huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kuendelea kumsupport msanii wake mpya B-Gway ambaye anafanya vizuri na wimbo wake mpya uitwao ‘Sijachukua’.
Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa 

0 comments:

Post a Comment