Saturday, 6 May 2017

#YALIYOJIRI HIVI PUNDE AJALI MBAYA YATOKEA ARUSHA,WANAFUNZI NA WALIMU WAPOTEZA MAISHA

Wanafunzi zaidi ya 20 wapoteza maisha huko Arusha, kufuatia ajali ya gari wakati wakielekea Karatu katika kufanya mitihani.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo MsindiForums imezipata  muda huu inaeleza kuwa,  ajali hiyo mbaya kabisa katika mkoa huo wa Arusha  imetokea eneo  la Kata ya Rhotia Wilaya ya  Karatu. Basi la wanafunzi wa St Lucky ya Arusha walikuwa wanaenda karatu kufanya mtihani na wanafunzi wenzao wa Tumaini English Medium School ya Karatu ndipo walipopata ajali hiyo.

Kwa mujibu wa mashuhuda waliopo eneo la tukio wanaeleza kuwa mpaka sasa taarifa za vifo ni watoto zaidi ya 20 wamepoteza maisha na waalimu wao.

MSINDIFORUMS inaendelea kuwasiliana na vyanzo mbalimbali vya habari, na tutakuhabarisha hapahapa kujua idadi kamili pamoja na majina yao. Endelea kuperuzi mtandao wako ulio bora zaidi.
Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa 

0 comments:

Post a Comment