Wabunge wawili wa Chadema, Peter Msigwa wa Iringa Mjini na Godbless Lema
wa Arusha Mjini wameomba mwongozo wa Spika kuhusu ubaguzi wa kisiasa
uliotokea kwenye msiba mjini Arusha Jumatatu.
Jana Jumatatu jijini Arusha ilikuwa inaagwa miili ya wanafunzi 32,
walimu wawili na dereva wa Shule ya Lucky Vincent waliopoteza maisha
katika ajali ya gari.
Wa kwanza kusimana alikuwa Msigwa ambaye amehoji kama ni haki kutowapa
fursa Meya wa Arusha, Calist Lazaro na Mbunge wa jimbo hilo, Lema kutoa
salamu za rambirambi.
Lema kwa upande wake amesema hata magari mawili ya kubeba wagonjwa
yaliyotolewa na yeye na mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari
yaliondolewa kwa sababu yana majina yao.
Amesema ni kwa sababu walimheshimu makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, vinginevyo mambo kama hayo huwa hayatokei mbele yao.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza HapaFollow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment