Tuesday, 9 May 2017

MADAKTARI Watalii Kutoka Marekani Wajitolea Bure Matibabu ya Watoto Watatu Walionusurika Katika Ajali ya Basi.

Madaktari watalii waliotoa msaada wa awali baada ya ajali iliyowaua wanafunzi na waalimu wa Lucky Vicent Academy wameahidi kuwapatia msaada majeruhi watatu waliobaki hospitalini hata kuwapeleka nje ya nchi kama itahitajika.
 
Akiwaongoza wakazi wa Arusha kuomboleza msiba katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid, Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu amesema kwamba Madaktari hao walikuwa watalii na gari lao lilikuwa mbele ya ‘bus’ la wanafunzi na hata baada ya ajali kutokea wao ndio walikuwa watu wa kwanza kutoa msaada wa kitaalamu.
 
Katika hotuba yake Makamu wa rais amesema kuwa hata baada ya kutoa msaada watalii hao  kutoka shirika la afya nchini Marekani wameahidi kujitolea kuwapatia matibabu wanafunzi watatu ambao ni majeruhi wa ajali hiyo na hata msaada kutoka nje ya nchi  wapo tayari kututoa.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa 

0 comments:

Post a Comment