Tuesday, 9 May 2017

Basi la Ally's na Isanzu Coaster Yagongana Uso Kwa Uso.

Basi la Ally's lililokuwa likitokea Mwanza kuelekea Tabora limegongana na Coaster ya Isanzu uso kwa uso iliyokuwa linaelekea Mwanza kutoka Kahama

Ajali imetokea saa mbili asubuhi eneo la Samuye barabara ya Shinyanga.Hali ya dereva wa Coaster ya  Isanzu si nzuri.
 
Kamanda wa polisi mkoani hapa, Muliro Jumanne amesema  chanzo cha ajali hiyo ni basi la kampuni ya Ally's kuwa kwenye mwendo kasi.

Jumanne amesema kuwa abiria waliokuwa kwenye magari hayo ni zaidi ya 70 lakini waliojeruhiwa ni 35 ambao ndiyo wamelazwa hospitali ya mkoa wa Shinyanga.

Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga,  Dk Rashid  Mfaume  amesema amepokea majeruhi  35 wa ajali hiyo wakiwemo watoto wawili na kwamba kati ya majeruhi hao wenye hali mbaya ni wawili.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa 

0 comments:

Post a Comment