Wednesday, 3 May 2017

Meneja wa AS Monaco anena na vyombo vya Habari hivi punde.

Meneja wa AS Monaco Leonardo Jardi amesema kwamba, ni lazima washinde katika mchezo wetu wa kwanza wa nusu fainali ya Klabu Bingwa Barani Ulaya dhidi ya Juventus ili tupate nafasi ya kuingia hatua ya fainali.

Monaco itawakaribisha Juve katika dimba la Stade Louis II usiku wa jumatano hii kabla ya kucheza tena mchezo wa marudiano Turin juma lijalo.

Bosi huyo amesisitiza ushindi siku zote unaanzia nyumbani.

“Huu utakuwa mchezo muhimu kwetu. Lakini mamuzi ya mwisho ya nani amepita katika hatua hii yatatoka huko Turin. Ni lazima tufunge hata goli moja pale Bayern Munich.
“Nilazima tufanye hivyo. Tuliwafunga magoli matatu Manchester City, magoli matatu Dortmund na magoli matatu pia dhidi ya Tottenham. Hizi zote zilikuwa ni timu kubwa . “Ndio maana ni lazima tushide Jumatano hii.”

Monaco ameingiza kimyani Magoli 11 mpaka sasa katika michezo yake minne iliyocheza kunako Klabu bingwa barani ulaya.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa 

0 comments:

Post a Comment