Kamati
Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) imewateua washiriki
sita kugombea ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala).
Katika
kikao kilichofanyika jana mjini Zanzibar walioteuliwa ni Profesa
Abdalla Safari, Salum Mwalimu, Ezekiel Wenje, Josephine Lemoyan,
Lawrence Masha na Pamela Massay.
Taarifa
ya leo iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya
Chadema, Tumaini Makene imesema wateule hao watakamilisha hatua zingine
za uteuzi kwa mujibu wa utaratibu, Kanuni za Bunge na Uchaguzi wa Bunge
la Afrika Mashariki.
Masha
na Wenje, walishiriki uchaguzi uliofanyika Aprili 4 ambao Chadema
ilipeleka majina yao pekee jambo lililozua mjadala bungeni na
kuhitimishwa kwa wao kupigiwa kura za Hapana.
Katika uchaguzi huo, wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano waliwachagua wajumbe saba wa Eala.
Kwa
upande wa CCM, walioshinda ni Fancy Nkuhi, Happiness Legiko, Maryam
Ussi Yahya, Dk Abdullah Makame, Dk Ngwaru Maghembe na Adam Kimbisa na
kutoka CUF iliyokuwa na wagombea watatu kwa ajili ya nafasi moja,
aliyeshinda ni Mohamed Habib Mnyaa akiwashinda Twaha Taslima na Sonia
Magogo.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment