Sunday, 7 May 2017

WAZIRI Muhongo: Mikataba Yote ya Umeme Nchini ni Mibaya.

Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo amewataka watanzania kukubaliana na ukweli kuwa mikataba yote ya umeme iliyopo hapa nchini ni mibaya. Waziri Muhongo ameyasema hayo alipokuwa akijibu changamoto zilizoelekezwa katika Wizara yake katika Mkutano wa Baraza la Taifa la Biashahara, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Hatahivyo,Waziri Muhongo hakufafanua kuhusu wahusika wa mikataba hiyo;mikataba husika na namna ya kuifanya iwe mizuri. Mtakubaliana nami kuwa mikataba ya umeme kati ya TANESCO na Makampuni ya kuzalisha umeme imekuwa ikizalisha kashfa za kifisadi pamoja na kesi mbalimbali za jinai na madai kwa miaka mingi sasa.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa 

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment