Tuesday, 25 October 2016

Rais Magufuli ametajwa kuwania tuzo ya ‘Forbes Africa Person of The Year’, ingia hapa kumpigia kura.

Rais Dkt John Pombe Magufuli ametajwa kuwania tuzo ya ‘Forbes Africa Person of The Year.’

Anachuana na watu wengine wanne wakiwemo: Rais wa Mauritania, Ameenah Gulib, Mwanzilishi wa Capitec Bank, Michiel Le Roux na Thuli Madonsela wa Afrika Kusini pamoja na watu wa Rwanda.

Zimebaki siku 22 za kupiga kura. Unaweza kumpigia kura Rais Magufuli kwa kubonyeza hapa. Hadi sasa Rais Magufuli anaongoza kwa asilimia nyingi (73%).

Mwaka huu tuzo hizo zitatolewa jijini Nairobi, Kenya November 17.

Wafuatao ni washindi wa tuzo hiyo miaka ya nyuma

Mohammed Dewji (Tanzania)– 2015
Aliko Dangote (Nigeria)– 2014
Akinwumi Adesina (Nigeria) – 2013
James Mwangi (Kenya) – 2012
Sanusi Lamido Sanusi (Nigeria)- 2011

#BURUDANI>>>Rose Ndauka Aswekwa Lupango.Fahamu zaidi hapa.

Staa wa Bongo Movie Rose Donatus Ndauka anadaiwa kuswekwa lupango kwa takriban saa nne kabla ya kuchomolewa kwa dhamana.

Sosi wetu ambaye ni mtu wa karibu wa Rose alinyetisha kuwa, staa huyo alikuwa kwenye misele na gari lake maeneo ya Kawe jijini Dar ambapo alitanua barabarani hivyo akakamatwa kisha kukaibuka tafrani iliyosababisha kufikishwa kwenye Kituo cha Polisi cha Kawe alikosota kwa muda huo kabla ya kuachiwa.

Baada ya Wikienda kunyetishiwa habari hiyo, lilimtafuta Rose ambaye alifunguka kwa kifupi:
“Duh! Hii ishu mmeipata? Kweli ninyi siyo watu wa mchezomchezo, baada ya kuandika kuhusu Lebo ya Ndauka mnataka umbeya tu, sasa hivi nna lebo imeanza na msanii Casso aliyeimba Wimbo wa Kitonga.”

Rose alisema kukaa kwake lupango amejifunza kwani saa nne aliziona kama miezi na kuwakumbusha watu kuheshimu sheria za usalama barabarani.

#YALIYOJIRI>>>UJUMBE ALIOANDIKA EDWARD LOWASSA BAADA YA KUTIMIA MWAKA MMOJA TOKEA SIKU YA KUPIGA KURA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Tanzania imetimiza mwaka mmoja tangu ilipofanya uchaguzi wake mkuu ambapo watanzania walipata nafasi ya kupiga kura kuwachagua Madiwani, Wabunge na Rais wote wataoliongoza taifa kwa miaka mitano.

Uchaguzi Mkuu ulifanyika tarehe 25 Oktoba 2015 ambapo ulikuwa ni mmoja ya chaguzi zilizokuwa na ushindani mkubwa zaidi kuwahi kutokea Tanzania tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.

Ushindani mkubwa ulikwa kati ya wagombea wa Urais, Dkt John Pombe Magufuli aliyekuwa akipeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Edward Ngoyai Lowassa, aliyekuwa akipeperusha bendera ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Ikiwa leo ni mwaka mmoja tangu kufanyika kwa uchaguzi, watu wengi wameandika vitu tofauti kwenye mitandao ya  kijamii wakijikumbusha hali ilivyokuwa ambapo baadhi waliweka picha na video za matukio mbalimbali ya Oktoba 25, 2015.

Aliyekuwa mgombea wa CHADEMA, Edward Lowassa kupitia ukurasa wake wa Facebook na Twitter ameandika ujumbe huu kwa Watanzania.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilimtangaza mgombea wa CCM, Dkt John Pombe Magufuli kuwa ndiye mshindi wa uchaguzi huo na aliapishwa Novemba 2, 2015 kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

EFM RADIO YAMPELEKA MTANGAZAJI WA CLOUDS FM MAHAKAMANI…VITA YAO YAZIDI KUWA KUBWA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Mtangazaji huyo aliondoka EFM mwanzoni mwa mwezi huu na kurejea kwenye kituo chake cha zamani, Clouds FM, alichoondoka pamoja na mwenzake Gerald Hando. EFM imefungua mashtaka katika mahakama ya kazi jijini Dar es Salaam kwa madai ya kukiuka mkataba wa kazi wa kituo hicho.
Kufuatia mashtaka hayo, EFM inadai fidia ya shilingi milioni 200 kutoka kwa mtangazaji huyo.
Inadai PJ alikatisha mkataba kiholela na kurudi tena Clouds FM bila kufuata makubaliano pamoja na sheria alizokubaliana nazo katika mkataba wake pale alipojiunga nacho.

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa November 23, 2016 katika mahakama ya kazi jijini Dar es Salaam.

PICHA:Hans Van Pluijm Alivyotua Mazoezini Kuagana na Wachezaji wa Yanga.Fahamu zaidi hapa.

Baada ya kuamua kujiuzulu nafasi ya ukocha mkuu wa Yanga, Hans van Pluijm alienda kwenye mazoezi ya klabu hiyo kwa ajili ya kuagana na wachezaji wake pamoja na baadhi ya viongozi wa benchi la ufundi waliosalia kwenye klabu hiyo.

Van Pluijm aliamua kujiuzulu nafasi hiyo baada ya kupata taarifa kwamba, uongozi wa Yanga umemleta kocha kutoka Zambia George Lwandamina ili kuchukua nafasi yake.

Kwa sasa, timu itakuwa chini ya kocha Juma Mwambusi ambaye alikuwa msaidi wa Hans van Pluijm mpaka hapo klabu itakapomtangaza kocha mkuu.

HATIMAYE NYUMBA YA KIFAHARI YA ALI KIBA YAWEKWA HADHARANI…JIKO TU LAGHARIMU MILIONI 19.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Alikiba hajawahi kusema kuwa yupo kwenye ujenzi wa ile inayoweza kuwa nyumba ya kifahari zaidi inayomilikiwa na msanii wa Bongo.
Nyumba ya Alikiba yenye ghorofa mbili
Na sasa nyumba yake yenye ghorofa mbili imewekwa hadharani.
 Ipo maeneo ya Tabata, jijini Dar es Salaam. Picha na video za nyumba hiyo zimewekwa kwenye ukurasa mmoja wa Instagram wa shabiki wake mkubwa.
 Alikiba bado hajahamia kwenye nyumba hiyo na mafundi wanamalizia décor.
 Haijajulikana mara moja gharama ya nyumba hiyo lakini shabiki wake anadai kuwa jiko pekee limegharimu takriban shilingi milioni 19.


#YALIYOJIRI>>>>Vigogo Bandari Kizimbani kwa Rushwa ya Bilioni 8.Fahamu zaidi hapa.

Vigogo  watatu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Ephraim Mgawe (62) wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka ya kujihusisha na rushwa ya Sh bilioni nane.

Mbali na Mgawe, vigogo wengine katika kesi hiyo ni Mkurugenzi wa zamani wa Uhandisi wa TPA, Bakari Kilo (59) na aliyekuwa Meneja wa Mazingira wa TPA, Theophil Kimaro (54) pamoja na Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya DB Shapriya, Kishor Shapriya (60).

Washtakiwa hao walifikishwa mahakamani jana na kusomewa mashtaka mawili na Wakili wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba. 
Wakili Kishenyi alidai katika tarehe tofauti kati ya mwaka 2009 na 2012, Mgawe, Kilo na Kimaro kwa kutumia nafasi zao, waliomba rushwa ya Dola za Marekani milioni nne ikiwa ni zaidi ya Sh bilioni nane.

Inadaiwa waliomba rushwa hiyo kutoka kwa Shapriya ili kumuwezesha ashinde zabuni iliyokuwa ikishindaniwa yenye namba AE/0116/2008-2009/10/59 kwa ajili ya ujenzi wa bomba la TPA katika RAS ya Mjimwema.

Aidha, inadaiwa katika tarehe tofauti kati mwaka 2008 na 2009 akiwa kama Mkurugenzi wa DB Shapriya alitoa rushwa ya Dola za Marekani milioni nne kwa vigogo hao, kwa ajili ya kuiwezesha kampuni yake ishinde zabuni. Baada ya kusomewa mashtaka hayo, washtakiwa walikana kuhusika na kutenda makosa hayo.

Wakili Kishenyi alisema upelelezi wa kesi bado unaendelea, pia hawana pingamizi la dhamana endapo washtakiwa watatimiza masharti ya dhamana yatakayotolewa na mahakama.

Vigogo hao waliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana yaliyowataka kuwa na wadhamini wawili waaminifu watakaosaini hati ya dhamana ya Sh milioni 500 kwa kila mmoja.

#YALIYOJIRI>>>Serikali Yakanusha Taarifa Iliyosambaa Katika Mitandao Ya Kijamii Kuwa Itaanza Kutoa Ajira.Fahamu zaidi hapa.

1.Ipo taarifa inayosambaa katika mitandao ya kijamii ikimnukuu Waziri wa Nchi -Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb), kuwa Serikali itaanza kutoa ajira, kupandisha Vyeo na kulipa Stahiki mbalimbali za Watumishi wa Umma mwezi Februari, 2017. Chanzo cha habari hiyo ni mtandao wa Jamii Forum kupitia mjadala ulioanzishwa na nkanga chief (JF-Expert Member) na baadaye kusambazwa katika mitandao mingine.

2. Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora inapenda kuwafahamisha Watumishi wa Umma na Umma kwa ujumla kuwa, taarifa hiyo haina ukweli wowote na ina lengo la kuupotosha

Umma. Hivyo watumishi wa umma na wananchi kwa ujumla wanaombwa kuipuuza taarifa hiyo na kuendelea na majukumu yao kama kawaida.


3.Serikali inasisitiza kuwa, suala la Ajira mpya na upandishaji Vyeo litafanyika kwa kuzingatia Bajeti ya Serikali ya Mwaka wa Fedha 2016/17. Malipo ya stahili za watumishi wa umma yatafanywa na Serikali kwa kuzingatia, Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo.

4. Ikumbukwe, Serikali ina utaratibu maalum wa kutoa taarifa kwa Umma, hivyo Serikali itatoa taarifa rasmi kwa Umma kupitia mamlaka husika.

5. Serikali kupitia taarifa hii inawaasa wananchi kuacha tabia ya kusambaza habari za uongo au zisizothibitishwa dhidi yake. Serikali haitasita kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika kuzusha na kusambaza habari za upotoshaji kuhusu shughuli za Serikali. 

Imetolewa na:

#YALIYOJIRI>>>Morocco na Tanzania zasaini mikataba 21 ya ushirikiano Ikulu jijini Dar.Fahamu zaidi hapa.

Mfalme  Mohammed VI wa Morocco amekubali maombi ya Rais John Magufuli ya kujenga uwanja wa mpira mjini Dodoma ambao utakuwa mkubwa kuliko ule wa Taifa jijini Dar es Salaam sambamba na kujenga msikiti mkubwa jijini humo. 

Rais Magufuli aliyasema hayo Ikulu Dar es Salaam jana wakati akitoa shukrani baada ya kukutana na kiongozi huyo, aliyeambatana na wajumbe 150 ambao pamoja na mambo mengine, nchi hizo mbili zilisaini Mikataba ya Makubaliano (MoU) 21.

Akitoa taarifa fupi ya mazungumzo baina yao, Rais Magufuli alisema Mfalme Mohammed VI amekubali kujenga msikiti mkubwa jijini Dar es Salaam sambamba na kujenga uwanja wa mpira mjini Dodoma wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 80 (zaidi ya Sh bilioni 160).

“Katika mazungumzo yetu, nimshukuru Mfalme Mohammed wa Morocco amekubali ombi langu la kujenga msikiti mkubwa hapa Dar es Salaam, na amekubali kwenye mji mkuu Dodoma, atajenga uwanja wa mpira utakaokuwa mkubwa kuliko wa Dar, na thamani yake ni zaidi ya Dola milioni 80,” alieleza Dk Magufuli.

Uwanja wa Taifa umejengwa na Wachina kwa gharama ya Sh bilioni 60 na una uwezo wa kuchukua watu 60,000 waliokaa. Dodoma ambayo ni Makao Makuu ya nchi na Serikali ya Awamu ya Tano imepanga yote kuhamia huko ifikapo mwaka 2020, inao Uwanja wa Jamhuri ambao unamilikiwa na CCM na unachukua watu 8,000.

Mbali na hayo, katika kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo mbili kwenye nyanja ya usalama na ulinzi, Mfalme huyo amekubali kuanzisha programu ya kubadilishana mafunzo baina ya askari wa Tanzania na Morocco na kwa kuanza wiki ijayo askari 150 wa Tanzania watakwenda mafunzoni nchini Morocco.

Katika ziara ya siku tatu ya kikazi ya Mfalme Mohammed VI aliyewasili nchini juzi, akiwa na ujumbe wa wafanyabiashara pamoja na viongozi wengine, wamefanikiwa kufanya makubaliano ya mikataba 21 katika nyanja mbalimbali zikiwamo za kilimo, gesi, madini na na usafiri wa anga.

Mikataba hiyo ni pamoja na Makubaliano ya Jumla katika Ushirikiano wa Uchumi, Sayansi, Ufundi na Utamaduni baina ya Serikali ya Morocco na Tanzania yaliyosainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk Augustine Mahiga na Waziri wa wizara hiyo wa Morocco, Salahddine Mezouar.

Mwingine ni ule wa kuanzishwa kwa Jukwaa la Mashauriano ya kisiasa baina ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na wizara hiyo nchini Morocco, mkataba wa ushirikiano kwenye sekta ya gesi, nishati, madini na sayansi ya miamba, mkataba wa ushirikiano wa usafiri wa anga, mkataba wa ushirikiano kwenye mradi wa mtangamano wa kuwasaidia wakulima wadogo nchini.

Pia mkataba wa makubaliano kwenye sekta ya uvuvi, mkataba wa makubaliano baina na MASEN-Morocco na Wizara ya Nishati na Madini kwa ajili ya maendeleo ya nishati mbadala, mkataba wa ushirikiano baina ya Shirika la Mbolea la Morocco (OCP) na Shirika la Mbolea la Tanzania katika kuendeleza soko la mbolea na kilimo nchini.

Pia mkataba baina ya Bodi ya Utalii Tanzania na Kamisheni ya Utalii Zanzibar na Ofisi ya Utalii ya Taifa nchini Morocco, Mkataba wa Kundi la Utoaji Mikopo la Morocco na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, Mkataba baina ya Shirika la Bima la Taifa (NIC) na Shirika la Bima la Morocco.

Mingine ni Mkataba wa Maeneo Maalumu ya Uwekezaji (EPZA) na Kundi la SNTL la Morocco katika ubia wa uendelezaji na utangazaji wa viwanda, mkataba wa usafirishiaji kwenye reli kupitia Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli Tanzania (RACO) kwa ajili ya ubia kuendeleza reli ya Mtwara-Mchuchuma/Liganga.

Aidha, mkataba mwingine ni ule wa kuanzishwa kwa Baraza la Biashara baina ya Shirikisho la Wafanyabiashara wa Morocco (CGEM) na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Mkataba wa Mkopo baina ya Benki ya Afrika (BOA) na Hospitali ya CCBRT na mkataba wa mkopo wa BOA na Kampuni ya gesi ya Lake.

Mkataba wa Mkopo wa BOA na Kampuni ya Superstar Forwarders, Mkataba wa Ushirikiano baina ya Kampuni ya OLAM Tanzania na Benki ya Attijariwafa, mkataba wa ubia baina ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)na Benki ya Centrale Populaire ya Morocco, mkataba wa Kitaalamu baina ya Shirikisho la Bima la Morocco na kampuni za bima Tanzania.

Pia mkataba wa ushirikiano baina ya kampuni ya kuchanganya chai ya Morocco na Kampuni ya Afri Tea and Coffee ya Tanzania.

Akizungumzia MoU kwenye usafiri wa anga, Rais Magufuli alisema wamekubaliana nchi hizo mbili kuanzisha safari za ndege za moja kwa moja kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kwenda Rabat, mji mkuu wa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

“Na sisi tumeanzisha shirika letu kidodokidogo linasuasua, lakini tutakuwa na ushirikiano mzuri na Shirika la Ndege la Morocco, na makubaliano haya yote ni mwelekeo nzuri wa kuijenga Tanzania na kuwa na uchumi unaokua kwa asilimia 7.2,” alisema Rais Magufuli.

Rais Magufuli alisema Morocco imepiga hatua kubwa kwenye utalii na kwamba mwaka 2015 ilipokea watalii milioni 10.5 na mwakani wanategemea kupokea watalii zaidi ya milioni 14 na kwamba Tanzania imeshaini makubaliano kwenye sekta hiyo kwa lengo la kuendeleza hifadhi za nchi na kuutangaza utalii.

Aidha, alisema makubaliano yote hayo yamelenga kuijenga Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati wa viwanda na kwamba hilo linawezekana kwa kuwa hata sasa hali ya uchumi wa nchi ni nzuri kwa kuwa unakua kwa asilimia 7.2; na taarifa za uchumi zinaonesha kwenye robo ya pili ya mwaka uchumi umekua kwa asilimia 7.9.

“Tuko kwa ajili ya kuujenga uchumi na niwakaribisheni wageni wetu kutoka Morocco, niwahakikishieni kuwa mko salama na karibuni kuwekeza kwa faida ya nchi hizo mbili ambazo uhusiano wake ulianza tangu enzi za Iban Batutu wa Morocco aliyetembelea Kilwa miaka mingi iliyopita,” alieleza Rais Magufuli.

Monday, 24 October 2016

PLUIJM AKABIDHI BARUA YA KUJIUZULU YANGA, WAMKUBALIA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Kocha Hans van der Pluijm ameachia ngazi rasmi kuinoa Yanga.

Pluijm ameamua kuachana na Yanga na barua yake ameikabidhi na uongozi wa Yanga tayari umemjibu.


Hii ni baada ya kamati ya Mashindano ya Yanga kuamua kumleta Kocha George Lwandamina raia Zambia.

Tayari Mzambia huyo yupo jijini Dar es Salaam akiendelea na mazungumzo na uongozi wa Yanga.

Kumekuwa na taarifa wameishamalizana lakini uongozi wa Yanga umeendelea kusema ni mazungumzo tu.

MWAMBUSI ATAIONGOZA YANGA KWA MUDA, LWANDAMINA ATAANZA KAZI MWEZI UJAO.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi atakiongoza kikosi cha Yanga katika mechi zilizobaki hadi hapo kocha mkuu mpya atakapoanza kazi.

Taarifa za ndani kutoka Yanga zinasema George Lwandamina raia wa Zambia ataanza kazi rasmi Novemba Mosi.

Tayari Lwandamina yuko jijini Dar es Salaam na Kocha Hans van der Pluijm ameachia ngazi rasmi kuinoa Yang.
“Mwambusi ndiye ataendelea na kikosi, mambo mengine yakikamilika Lwandamina ataanza kazi,” alisema.

Awali ilielezwa kwamba Pluijm atakuwa ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Yanga kabla ya mwenyewe kuamua kujiuzulu.

BAO LA NGASSA KIVUTIO, AANZA KUONYESHA CHECHE ZAKE OMAN.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Mshambuliaji mpya wa Fanja ya Oman, Mrisho Ngassa ameanza kuonyesha makali yake baada ya kuifungia timu yake bao katika mechi iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Ngassa aliyewahi kuzichezea Yanga na Simba kwa vipindi tofauti, alifunga bao hilo akisawazisha baada ya Fanja kuwa nyuma dhidi ya Al Nah kwa bao moja, hivyo kufanya matokeo kuwa.

Hata hivyo mechi hiyo ilisha kwa sare ya mabao 2-2 lakini Ngassa akawa ameonyesha uhai mkubwa katika kikosi hicho.


Mtanzania huyo amejiunga na Fanja akitokea Free State Star ya Afrika Kusini aliyoamua kuvunja mkataba.

BAADA YA KUJIUZULU YANGA,HANS VAN DER PLUIJM ANUKIA AZAM FC.FAHAMU ZAIDI HAPA.

PLUIJM

Kocha Hans van der Pluijm ananukia Azam FC ambayo imeonyesha nia ya kumpa nafasi ya kuinoa.

Bado hakujawa na mwafaka kocha huyo raia wa Uholanzi, achukue nafasi ya kocha mkuu au mkurugenzi wa Ufundi.

Pluijm ametangaza kujiuzulu Yanga baada ya Kocha George Lwandamina kutua nchini na kumalizana na Yanga.

Lwandamina amemalizana na Yanga na anatarajia kuondoka na kurejea kwao Zambia kabla ya kurudi tena.

Lakini Azam FC imeonyesha nia ya kumnasa Pluijm ambaye iliwahi kumuwania hapo awali.

“Kuna mazungumzo ingawa inafanywa siri kubwa, sijajua sahihi ni mkurugenzi wa ufundi au kocha mkuu.

“Nafikiri ni suala ambalo linaendelea kushughulikiwa,” kilieleza chanzo.

Kumekuwa na ugumu kuwapata viongozi wa Azam FC lakini juhudi zinaendelea ili kupata kauli yao kuhusiana na Pluijm pia Kocha Zeben Hernandez raia wa Hispania ambaye anakinoa kikosi chao.

#MICHEZO>>>>Thomas Ulimwengu Aondoka TP Mazembe, Afuata Ndoto zake Kucheza Ulaya.Fahamu zaidi hapa.

Baada ya kucheza misimu mitano kwenye klabu ya TP Mazembe, mchezaji wa Taifa Stars, Thomas Ulimwengu ameondoka kufuata ndoto zake kucheza Ulaya.

Mchezaji huyo aliyekuwa akivaa jezi namba 28 na aliyepewa jina la utani ‘Rambo’ alichukuliwa na klabu hiyo akiwa na umri 18 kutoka AFC Academy ya Stockholm, Sweden. Akiwa na TP Mazembe, Ulimwengu amecheza mechi 130 na kufunga mabao 35.

Wakati anachezea klabu hiyo klabu nyingi zilitaka kumchukua lakini aliamua kumaliza kwanza mkataba wake na Mazembe. Aliamua kutoongeza tena mkataba na TPM. Na sasa Ulimwengu anataka kufuata nyayo za Mtanzania mwenzake Mbwana Samatta wa Genk ya Ubelgiji.

Kabla ya kuondoka Lubumbashi, Ulimwengu alisema kupitia taarifa kwenye tovuti ya klabu hiyo, “Kwa miaka mitano Mazembe imeniruhusu kuendelea kukua kisoka na nataka kuwashukuru wote walioniunga mkono na kusaidia kushinda vikombe wakiongozwa na Rais Katumbi na Mrs Carine, viongozi na makocha.”

Vyakula Vinavyoongeza Hamu na Nguvu ya Kufanya Tendo la Ndoa.Fahamu zaidi hapa.

Tatizo la uwezo wa kufanya tendo la ndoa linazidi kukua miongoni wa wanandoa na wapenzi wengi. Takwimu za kitafiti zinaonyesha kuwa karibu ndoa 4 kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliana na tatizo hili. Aidha wanaume 6 kati ya 10 wanatajwa kulalamikia upungufu wa nguvu za kiume.

Pamoja na matatizo mengine kutajwa kuchangia upungufu wa nguvu za kiume na kushuka kwa msisimko wa tendo miongoni mwa wanandoa, uchunguzi umeonesha kuwa utumiaji holela wa vyakula hasa vyenye mafuta ni moja kati ya sababu zinazochangia kwa kasi tatizo hili.

Kwa kuzingatia hilo, watafiti wa masuala ya uhusiano wa kimapenzi wamebaini aina mbalimbali ya vyakula ambavyo vina uwezo wa kumuongezea mtu nguvu ya kufanya tendo la ndoa.  Vyakula hivyo ni hivi vifuatavyo:

1. PILIPILI
Kama tunavyojua wote mara nyingi chakula ambacho kimeungwa pilipili hufanya hata mapigo ya moyo kuwa tofauti na wakati mwingine hata jasho au kamasi hutoka. Ndani ya pilipili kuna kitu kinaitwa capsaicin ambacho hufanya pilipili iwe na hali ya ukali. Capsaicin huwezesha ubongo kutoa homoni ya endorphins ambayo huleta mgusu wa hisia za raha wakati wa kufanya tendo la ndoa.
Pia pilipili husisimua mfumo wa fahamu (nerves) wa ubongo na katika kufanya hivyo huwezesha kuamshwa haraka kimapenzi (kunyegeka) wakati wa tendo la ndoa na pia ukiguswa au kubusiwa au kunyonywa au kupapaswa unapata hisia kila sehemu ya mwili.

2. MATUNDA NA MBOGA ZA MAJANI
Ulaji wa matunda na mboga za majani una matokeo makubwa sana katika hamu ya tendo la ndoa kwa njia nyingi. Kwanza matunda na mboga za majani hupunguza kiwango cha mafuta na unene (cholesterol).  Kuongezeka kwa mafuta mwilini huzuia mzunguko wa damu kwa kubana mishipa ya damu.

Pia kula matunda na mboga za majani huhakikisha balance ya uzito kwani unene (obesity) kwa wanaume kuna matokeo mabaya katika kuzalisha homeni za testoeterone na hatimaye jogoo kushindwa kuwika na kuwa na pia mwanaume anakuwa na hisia za mapenzi (libido) kidogo.
Na pia wanandoa wanapozidi kunenepeana ndipo na hali ya kufurahia au kuwa na hamu ya tendo la ndoa huzidi kupungua. Kitalaam inashauriwa kula milo (potions) 3-5 za matunda kwa siku.

3. NAFAKA ZISIZOKOBOLEWA
Nafaka hasa zisizokobolewa kama mahindi, ngano, uwele, nk zina nyuzinyuzi (fibre) na sukari ngumu (complex sugar) ambazo kusaidia kutunza uzito wa mwili. Nafaka husaidia katika kuzalisha homoni za testosterone kwenye damu. Na pia nafaka huwezesha mtu kuwa na nguvu hatimaye kwenda masafa marefu wakati wa tendo.

Kula nafaka nzima kama vile brown bread badala ya white bread, pia kula nafaka halisi badala ya cornflakes ni jambo zuri linalokuhakikisha afya nejama na mahusiano mazuri ya ndoa yako.

4. TANGAWIZI
Tangawizi ni kiungo cha mboga ambacho husisimua sana na kusaidia mfumo wa mzunguko wa damu mwilini. Tangawizi zinajulikana sana kwa kusukuma damu kwenda sehemu za viungo vya uzazi yaani uke na uume hivyo kuwa na umuhimu sana katika kuboresha ufanyaji wa tendo la ndoa. Inaweza kuliwa mbichi, au kuliwa ikiwa imeungwa kwenye chakula au kusagwa na kuwa kama unga na kutumiwa kama chai.

5. ASALI
Asali ina madini yanayoitwa boron, ambayo husaidia mwili kutumia homoni ya estrogen ambayo ni homoni inayohusika na viungo ya uzazi na mapenzi kwa mwanamke.
Pia kuna utafiti unaoonesha kwamba asali huongeza nguvu, kitendo ambacho kitapelekea mwanamke kuwa uwezo na hamu ya tendo la ndoa au libido.

6. KARANGA
Karanga huhusika katika kuchochea mfumo wa mzunguko wa damu (vascular system). Mzunguko wa damu ulio sawasawa katika uke na uume huwezesha mwanaume na mwanamke kupata msisimko wa mapenzi haraka hatimaye tendo la ndoa kuwa murua. Pia karanga zina madini muhimu kama vile magnesium, asidi ya folic na zinc ambayo ni muhimu sana katika usalishaji wa mbegu za mwanaume.

7. CHAZA (OYSTERS) NA PWEZA
Hawa ni aina ya samaki ambao hupatikana katika maji chumvi. Huwa na kiasi kikubwa sana cha madini ya zinc na haya madini ndiyo huhusika zaidi na uzalishaji wa homoni ya testosterone kwa wanaume.
Pia imethibitika kwamba wanaume wenye ukosefu wa madini ya zinc huwa na matatizo ya nguvu za kiume.  Pia madini mengi ya zinc mwilini huongeza kiwango cha shahawa kwa wanaume.

8. SOYA
Pamoja na kuwa na kiwango kidogo sana cha mafuta (fat) na pia kuwa na kiwango kizuri cha protein, soya zina phytoestrogens ambayo husaidia sana wanawake ambao wamefikia menopause kutengeneza homoni estrogen ya ziada.
Husaidia uke kuwa laini (wet, lubricated) mwanamke akisisimuliwa wakati wa tendo la ndoa.

9. CHOKOLETI
Chocolate ina phenylethylamine, kemikali ambayo husababisha hisia (feelings) za furaha wakati wa mwanamke au mwanaume kufika kileleni (orgasm). Inasaidia sana kula chocolate masaa machache kabla ya kuanza kufanya tendo la ndoa.

10. PARACHICHI
Aina nyingine ya chakula ambacho husaidia kuongeza uwezo wa mtu kufanya tendo la ndoa ni Parachichi. Tunda hili linauwezo mkubwa wa kuzalisha vitamini E ambayo husaidia katika uzalishaji wa homoni. Inatajwa kuwa watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwana msisimko mkali wa kimapenzi na kwa upande wa wanawake husaidia kuongeza majimaji yenye utelezi sehemu za siri na hivyo kuzuia uwezekano wa kuchubuka wakati wa kujamiiana.

#YALIYOJIRI>>>>Serikali Kuwabana Wanafunzi Wanaopewa Mikopo Kwa Kipaumbele.Fahamu zaidi hapa.

Serikali ipo katika mkakati wa kuwabana wanafunzi wanaopewa mikopo katika fani za kipaumbele, kutumikia katika utumishi wa umma nchini kwa muda fulani ili kuhakikisha dhamira ya serikali ya inatimia.

Fani hizo ni sayansi za tiba na afya, ualimu wa sayansi na hisabati, uhandisi wa viwanda, kilimo, mifugo, mafuta, gesi asilia, sayansi asilia, mabadiliko ya tabia nchi, sayansi za ardhi, usanifu majengo na miundombinu.

Serikali inachukua uamuzi huo, baada ya kubaini kuwapo wanafunzi wanaosomea fani hizo ili kupata mikopo, lakini baada ya kumaliza hukimbilia kufanya kazi nyingine au nje ya nchi na hivyo kuendelea kuwepo upungufu wa wataalamu waliowakusudia kubaki.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na mafunzo ya ufundi, Stella Manyanya aliyasema hayo hivi karibuni, alipozungumzia utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Alieleza kuwa serikali inafikiria kuwe na utaratibu kwa wanaonufaika na mikopo ya kipaumbele kuingia makubaliano na serikali.

Alisema suala hilo halitakuwa jipya kwani hapo nyuma walikuwa wakibanwa kuwa lazima kufanya kazi angalau kwa miaka mitano serikalini na baadaye ni ruhusa kwenda popote, lakini kwa sasa hawawezi kuwabana wote, lakini lazima kufanya hivyo kwa hao wa kipaumbele.

Aidha Manyanya alizungumzia ulipaji mikopo hiyo na kudai wanaboresha sheria ya kukusanya madeni kwa kushirikiana na waajiri.

“Serikali itakusanya madeni hata kwa wakopaji ambao wamejiajiri kwa sababu wengi wakimaliza masomo hawafikirii kulipa,” alisema.”Sasa lazima walipe, wakopaji watambue fedha hizo ni mikopo na lazima kulipa.”

Alisema kwa wakopaji watakaoajiriwa, wizara inataka mkopo huo kuwa wa kwanza kukatwa kabla ya mingine ili kuepuka kuingiliana na sheria za kazi, zinazotaka mkopaji kuachiwa fedha fulani katika mshahara wake.

Huyu Hapa Mpenzi Mpya wa Idriss Sultan....Wagandana Kama Ruba Huko MTV Awards.Fahamu zaidi hapa.

Inasemekana eti Idriss na Mrembo ajulikanaye kama Sanchoka kwa sasa ni wapenzi baada ya kuonekana pamoja huko Afrika Kusini walipoenda kwa ajili ya MTV awards...
Picha na Video mbali mbali wakiwa pamoja zainazagaa huku instagram

Sunday, 23 October 2016

Ukweli Unauma, Hizi Ndio Sababu Zilizotufanya Watanzania Tukakosa Tuzo MTV Awards.Fahamu zaidi hapa.

Ngoja Niongee Leo Hii.
Watu Wengi Wamekuwa Wakijiuliza Why Tumeshindwa Huku Wakipeleka Lawama Zote Kwa Teams Bila Hata Kuchambua KwA Kina.

KwA Upande Wangu Na Akili Zangu Hizi Hizi Za Insta Ni Wengi Mno AmbaO Wanaingia Katika Kusababisha Hili KwA Namna Moja Ama Nyingine.

1. Watu Wa Kwanza Kabisa Kuchangia Kukosa KwA Tuzo Ni Wasanii Wenyewe. Wasanii Wamekuwa Wanafiki Sana Sana. Naomba Nihakikishie Direct Hii, Hivi Bongo Kuna Wasanii Wawili Tu? Au Ndio Ile Hawana Management Nzuri?? Ifike Time Muache Ubinafsi, If Unaamini Mungu Anampa Kila Mtu Ridhiki Yake Then Acheni Uchoyo WA Kuwaambia NA Wenzenu Process Za Kuwafikisha Katika Mashindano, Tell Them What They Suppose To Do, Wingi Wenu Katika Categories Utasaidia Pia Kuwanyanyua, Usiniambie Bongo Kiba Na Mondi Tu Ndio Very Best Artist, Narudia Kama Unajiamini Ridhiki Yako Ipo Just Tell Na Wengine Nini Wanatakiwa Kufanya Wafike Hapo. Rayvanny Kama Asingekuwa WCB Am Not Sure Kama Angekuwa Katika Kipengele Chochote, Too Bad Namshangaa Kiba Why Abdu Kiba Bado Yupo Nyuma Tu Hafiki Popote. Hebu Mjifunze Kubebana Sana.

2. Teams ,This Is The Worse Part Dah!! Sitaki Hata Kufikiria Mara Mbili, But Mmeshawahi Hata Kujiuliza Wanapata Wapi Nguvu Zote Hizo?? KamA Utajiuliza Hili Swali KwA Kina Utajua Kuwa Wasanii Wenyewe Hapa Wanarudi Tena Humu Humu Katika Teams, Wao Ndio Vichocheo Vikubwa Vya Jeuri KwA Hizi Teams, We Know Kila Mtu Ana Njia Yake Ya Kutafuta Ugali Mezani, Ila Ifike Muda Kama Kweli Mnataka Uzalendo Make Sure Mnavunja Team Za Kibaguzi, Unajua Hata Wasanii Wakubwa Nje Wana Teams Zao (Tena Kuna Tuzo Wana Mpaka Category Team Ya Nani Ni Strong Team) Rihanna Navy Ya Rihanna, Beyhive Ya Beyonce, Swifties Ya Taylor Swift, Arianators For Ariana Grande, Selenators Hawa WA Selena Gomez, Dah Guys Wako Wengi Tu, Ila Hawa Wanaongoza Kununua Kazi Zao, KutoA Support Za Shows, Bidhaa Zao NA Kadhalika, Sisi Ni Mitusi Tu Mwanzo Mwisho, Mitusi Tu.

3. Media Hawa Unaweza Kuwaona Hawamo Ila Trust Me Hawa Watu Nao Kwa Namna Moja Ama Nyingine Wanachangia, Wanachangia Sana, Ifike Time Na Wasanii Wengine Wapewe Support,

Pamoja Na Kulalamika Kooote Wabongo Turudi Kwenye Ukweli Hivi Kweli Diamond Angemshinda Wizkid?Vanessa Amzidi Yemi Alade Na Rayvan Ampite Tecno. Nah Hapana Tuwe Wakweli At Once.

Tunajiliwaza Lakini Ukweli Ni Kwamba This Time Tulibanwa Mno, Vanessa Ana Ngoma Gani Ya Kumpita Yemi?? Nyimbo Mbili Za Rayvanny Ampite Techno Na Ma Wash Yake Sijui Maduro?? Diamond Tuzo Zilizopita My #1 iliweza Kumbeba, Mwaka Huu Alikuwa Na Kipi Cha Kumpita Wizkid?? Pamoja Na Kura Zote Na Yote Tunatakiwa Kukubali Mwaka Huu Tulibanwa. Who Knows YaMoto Band?? Where In Africa Wamefanya Hata Show, Kiukweli This Time Hatukuwa Na Lolote. (Najua Tutakataa Kuukubali Huu Ukweli)
Tatizo Wabongo Tunajiona Sisi Ni Wakubwa, Kiukweli Bado Tuna Safari Ndefu, Wizkid Sio Mwenzetu, Kiba Na Diamond Hawamgusi Hata Robo Ana Mashabiki Africa Nzima Na Nje Ya Africa.

Diamond Asubiri Mwakani Wimbo Wake Na P Square Una Nafasi Kubwa Sana YA Kumpa Tuzo, My #1 Na Nana Zilimbeba Sana, Ila Baada Ya Hapo Kiukweli Alikuwa Na Nyimbo Za Kawaida Za Wabongo Na Sio Nyimbo Za Tuzo Kubwa.

Kiba Japo Hakuwepo Direct Katika Nominee, Ila Kajitahidi As An Artist Kwa Show Yake, Amefanya Poa Performance Japo NAe Pia Anabezwa. For Now Sasa Ndio Tuonyeshe Huo Uzalendo, Kumuombea NA Kupiga Kura Ile Tuzo Ile MtvEMA Ije Home.

NINI KIFANYIKE
Wasanii Wetu Needs To Go Outside, Wanatakiwa Waanze Kupiga Shows Across Africa Countries, Isiwe Tu Shows Wanazoalikwa Ulaya. Leo Hii Wizkid Anakuja Tz Kupiga Show Coz Hapa Tz Ana Mashabiki, Plus Nchi Mbalimbali Za Africa Anazokwenda. Nina Hakika Katika Hizo Tuzo Wapo WaTz Kibao Waliompigia Kura, Tukiacha Hizo Mateam But As Fans Wake From Tz.
Mziki Wetu Unakuwa Yes, Lakini Tutoke Pia, Tupige Shows Africa Na Itasaidia Kukuza Jina, Soko Na Kujitangaza.

Hayo Yoooote Yakishafanyika Sasa Ndio Tuje Katika Kura, Na Narudia Teams Sio Shida Kama Tutajua Jinsi Ya Kuzitumia NA Sio Kusambaza Chuki, Hata Ulaya Wana Teams (As Mentioned Mwanzo) Team Zetu Zinakosa Uzalendo, ZinaendekezA Chuki Hata Katika Mambo Ya Msingi.
Tunashukuru 5 nominations, Ni Jambo La Khery, Hata Appearance Ya Idris NA Navy Kenzo. Tupo Pazuri, Next Year Tuwe Na 10 Nominations

#YALIYOJIRI>>>>Kutana na Mwanamke Mnene Kuliko Wote Duniani… Ana Uzito wa Kilo 500.Fahamu zaidi hapa.

 Kwa mujibu wa jarida la Daily Mail, inaelezwa kuwa mwanamke huyo aitwaye Iman Ahmad Abdulati mwenye miaka 36 hajawahi kutoka ndani kwa miaka 25 na amekua akiongezeka uzito wake kwa haraka mpaka kufikia kilo 500 zinazompa shida ya kujifanyia usafi na hata kula. Ripoti ya madaktari inaonesha kuwa mwanamke huyu anasumbuliwa na maambukizi ya bakteria wanaoshambulia ukuaji wa mwili.

Akiwa na miaka 11 alianza kusumbuliwa na tatizo hilo ingawa wazazi wake wanakiri kuwa hawakudhani kuwa ni tatizo lakini siku zilivyozidi kwenda ndipo wakabaini kuwa halikua jambo la kawaida hivyo wakaamua kutafuta wataalamu ambao walitoa ripoti kuwa ana matatizo ya mwili wake kukaa na maji mengi bila kuyatoa nje kitu ambacho sio cha kawaida kwa binadamu.

#BURUDANI>>>>Muonekano wa Shilole Red Capet ya MTV Awards Wazua Gumzo Mitandaoni.Fahamu zaidi hapa.

 Mrembo Shilole aka Shishi Baby amezua gumzo mitandaoni kwa vazi alilovaa kwenye red kapeti ya MTV Mama Awards zilizofanyika jumamosi iliyopita...

Baada ya kutupia hiyo picha kwenye page yake hivi ndivyo watu walivyofunguka...

suzan.ndama
Kikwell mim huyu dada toka kaanzakufahamika sana cjawah kupendezewa na mavaz yake

sofia_omary78 
Kajifanya mjuaji kaharibu sasa ivyo ndo nini seemu yenye heshima Zake watu na misuti yao wewe unatuvalia kibkita kama uko kwenye singeli anawezekana hii safari ya kushitukiza hajajipanga igweeeeeee