Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO)
akikanusha kuhusu Chadema kutumia Uwanja wa Taifa kuzindua kampeni
zake siku ya tarehe 22 Agosti, 2015 jijini Dar es Salaam. Kanusho
hilo lilitolewa katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) uliopo jijini Dar es
Salaam.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia
taarifa kutoka Serikalini kuhusu Chadema kutumia Uwanja wa Taifa kuzindua
kampeni zake siku ya tarehe 22 Agosti, 2015 jijini Dar es Salaam.
Kanusho hilo lilitolewa katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) uliopo
jijini Dar es Salaam.
SERIKALI imekanusha taarifa zilizojitokeza
kwenye Vyombo vya habari yakiwemo magazeti na mitandao ya kijamii kwamba Chama
Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kitafanya mkutano hadhara Uwanja wa Taifa
Dar es Salaam tarehe 22 Agosti, 2015. Akizungumza na vyombo vya habari jana,
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene alisema serikali
haijatoa ruhusa kwa chama chochote cha siasa kutumia uwanja wa taifa kwa ajili
ya shughuli za kisiasa. Alikiri kwamba ni kweli kwamba CHADEMA waliiandikia
Wizara tarehe 12 Agosti, 2015 kutaka kutumia uwanja wa taifa katika uzinduzi wa
kampeni lakini ombi lao lilikataliwa kwa maelezo kwamba uwanja ule kwa
mazingira ya sasa hauruhusiwi kutumika kwa ajili ya mihadhara ya vyama vya
siasa. “kwa kipindi haturuhusu uwanja wa taifa kutumika kwa mihadhara ya
kampeni za vyama vya siasa. Uamuzi huu unalenga kuweka uwanja katika mazingira
rafiki ya michezo na kuepuka athari zozote zinazoweza kujitokeza kutokana na
mihemuko ya kisiasa” alisema Bwana Mwambene. Mwambene ameeleza kuwa, Serikali
imeamua uwanja huo ubaki kwa ajili ya kufanyia shughuli zake za msingi za
kimichezo ili kuepuka mihemuko na athari yoyote inayoweza kujitokeza kutokana
na hamasa za kisiasa. “Ni kweli kwamba tulipata barua ya Chadema kuomba Uwanja
kutumika kwa ajili ya mhadhara ya kisiasa wa CHADEMA hasa kuzindua Kampeni zao
kwenye Uwanja tayari tumeshawaandikia kuwaarifu kuwa Uwanja ule hauwezi
kutumika kwa ajili ya shughuli zozote za kisiasa” alisema Bwana Mwambene.
0 comments:
Post a Comment