Home »
Michezo
» #MICHEZO>>>AZAM WAKUBALI YAISHE, KUKOMAA NA KOMBE LA FA.Fahamu zaidi hapa.

SIKU moja baada ya
Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) kuipokonya pointi tatu timu ya
Azam kwa kosa la kumchezesha beki wao Erasto Nyoni aliyekuwa na kadi
tatu za njano, Uongozi wa timu hiyo umelijia juu shirikisho hilo na
kusema linaongozwa kwa majungu.
Azam ilimchezesha Nyoni
katika mchezo namba 156 dhidi ya Mbeya city uliochezwa Uwanja wa Sokoine
jijini Mbeya na kukiuka kanuni ya 37(4) ya ligi kuu toleo la mwaka 2015
na kanuni ya 14(37) ya mwaka jana.
Mtendaji Mkuu wa timu
hiyo Saady Kawemba ameiambia BOIPLUS kuwa: ''Kwa uongozi huu wa
shirikisho hilo tutaendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu kwa kuwa kuna
maamuzi yanafanywa ili kuwapa faida timu fulani. Tuliisajili Azam kama
timu ya mpira hivyo tutaendelea kucheza ila utaratibu unaofanywa na TFF
ndiyo unaodumaza soka na tumefunga mjadala sasa tunaangalia fainali za
Kombe la FA,''
Azam imeshuka hadi
nafasi ya tatu baada ya kubakiwa na alama 57 wakiwa nyuma kwa pointi
moja dhidi ya Simba ambao wana mchezo mmoja mkononi huku Yanga
ikiendelea kubaki kileleni mwa ligi ikiwa na pointi 68.
Azam watashuka dimbani
kesho Jumamosi kuwakabili Kagera Sugar mechi itakayochezwa Uwanja wa
Kambarage mkoani Shinyanga huku wenyeji wakihitaji pointi tatu ili
kujinusuru kushuka daraja.
UNAWEZA COMMENT HAPA.
Related Posts:
#MICHEZO>>>>WAPINZANI WA YANGA CAF WAANZA KUTOA SABABU.Fahamu zaidi hapa.
TIMU ya soka ya Medeama ya Ghana,
imesema itakuwa shughuli pevu kukutana Yanga SC ya Tanzania katika hatua
ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, kwa sababu sasa inafundishwa
na kocha wao wa zamani, Mholanzi Hans van d… Read More
#MICHEZO>>>FARID MUSSA APATA RUHUSA YA BOSS WA AZAM KWENDA HISPANIA.Fahamu zaidi hapa.
Maendeleo ya soka katika nchi zinazoendelea hususani nchi za Ukanda wa
Afrika Mashariki linahitaji watu wenye kujua thamani ya vipaji na namna
ya kuviendeleza tofauti na watu wenye kutaka faida kubwa kabla y… Read More
#MICHEZO>>>>UWEPO GUARDIOLA, KLOPP, WENGER, MOURINHO, CONTE, NI KUREJEA KWA UBORA WA EPL ULAYA?.Fahamu zaidi hapa.
Na Mahmoud Rajab
Hatimaye Jose Mourinho anarudi tena kundini na kukutana na mahasimu
wake wakubwa katika soka ambao ni Pep Guardiola, Wenger na Klopp (ambaye
vilevile ana historia na Pep Guardiola pia) bila kusahau Conte… Read More
#MICHEZO>>> WAMBURA AULA KWA CAF.Fahamu zaidi hapa.
Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), limemteua
Michael Richard Wambura kuwa Kamishina wa mchezo wa kuwania kufuzu
fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Rwanda na Msumbiji
unaotarajiwa kufanyika jijini Ki… Read More
#MICHEZO>>>>Video#INTERVIEW YA KWANZA YA MOURINHO AKIWA KOCHA WA MANCHESTER UNITED.
Jose Mourinho amewaasa mashabiki wa Manchester United kusahau yote
yaliyotokea miaka mitatu iliyopita wakati timu hiyo ilipokuwa chini ya
David Moyes na Louis van Gaal na kuangalia namna ya kuirudisha upya
katika zama za… Read More
Safi sana
ReplyDelete