Genk walipata bao la kwanza kwenye dimba lao la nyumbani, Cristal Arena kupitia kwa Neeskens Kebano aliyefunga kwa kichwa katika dakika ya 47 baada ya kushushudia timu hizo zikienda mapumziko bila magoli.
Genk ambayo inapamba kumaliza ligi katika nafasi za juu ili ishiriki michuano ya Ulaya, ilipata bao la pili dakika ya 63 lililofungwa na Onyinye Ndidi huku michomo kadhaa ya Zulte ikiokolewa na kipa wa Genk, Marco Bizot.
Samatta ambaye amerejea uwanjani baada ya kukosekana kwa wiki mbili akiuguza jeraha la pua nusura aipatie Genk bao la tatu lakini chenga yake ya kudokoa ilinaswa na kipa wa Zulte, Sammy Bossuyt.
Kwa ushindi huyo Genk imefikisha pointi 36 ikibakia katika nafasi yake ya nne nyuma ya Club Brugge inayoongoza ligi kwa pointi 44, Anderlecht yenye 41 na Gent iliyojikusanyia alama 38.
Kikosi cha Genk kilikuwa hivi;
0 comments:
Post a Comment