Home »
Burudani
» #YALIYOJIRI>>>>GADNER SIJUTIA KUMTUSI KOMANDO JIDE,MAMBO MAZITO YAIBUKA.Fahamu zaidi hapa.
SIKU chache baada ya kipande cha video kuonekana katika mitandao
ya kijamii, ikimuonesha mtangazaji maarufu, Gardner G Habash akitoa
maneno ya matusi kwa mkewe wa zamani, Judith Wambura ‘Jide’, ameonekana
kujutia kitendo chake hicho. Katika eneo ambalo linalotajwa kuwa ni
katika Ukumbi wa TCC Chang’ombe, Ijumaa ya wiki iliyopita, Gardner,
aliyejitambulisha kuwa ni Mtangazaji wa Clouds FM, alitoa maneno ya
kidhalilishaji kwa msanii huyo wa Muziki wa Kizazi Kipya, baada ya
kuulizwa na mashabiki kama alikuwa na matatizo na mtalaka wake. “Mimi
sina neno na yule mtoto wa kike, nime… (tusi) kwa miaka 15,” alisema
mtangazaji huyo, ambaye aliishi katika maisha ya ndoa na Jide kwa zaidi
ya miaka kumi, kabla ya kutengana miaka miwili iliyopita Akizungumza na
Risasi Mchanganyiko lililotaka kufahamu kisa na mkasa wa kutoa maneno
hayo, Gardner alishindwa kuongea akidai alikuwa katika kikao, lakini
alituma ujumbe mfupi wa maneno akisema;
Gardner, aliyejitambulisha kuwa ni Mtangazaji wa Clouds FM.
“Kaka pole kwa usumbufu, sitakuwa na cha kusema kwa sasa ili kuepusha
tafsiri isiyo sahihi, naomba nielewe mkuu. Asante.” Gazeti hili pia
lilimtafuta kupitia simu yake ya mkononi mwimbaji huyo wa kibao cha Ndi
Ndi Ndi, Jide lakini hakupokea.
Hata Meneja wake, Severin Mosha maarufu kama Seven, alipoulizwa kama
wana taarifa na kipande hicho cha video na mpango wao kuhusiana na
jambo hili, alisema wameiona lakini hawana la kusema kwa sasa. Katika
hali nyingine, Naibu Waziri wa Afya, Jinsia na Watoto, Dk. Khamis
Kigwangalla amekitaka Kituo cha Redio cha Clouds na Gardner kumuomba
radhi Jide.
Chanzo: Risasi Jumatano/GPL
Related Posts:
Team Wema Wamfanyia Wema 'Suprise' Kubwa Kwenye Siku Yake ya Kuzaliwa.
Ikiwa leo Septemba 28, 2017, mwigizaji mahiri Bongo, Wema Isaac Sepetu
almaarufu Keki ya Taifa, anasheherekea birthday yake, mashabiki wake
wameungana kwa pamoja na kumfanyia surprise akiwa saluni kwa kumpelekea
keki n… Read More
TID Atangaza Nia ya Kugombea Ubunge wa Kinondoni 2020 Je Atamng'oa Mtuli?
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Khalid Mohamed maarufu kama T.I.D,
ametangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Kinondoni, kwenye uchaguzi
ujao unaotarajiwa kufanyika mwaka 2020, na kumng'oa mbunge wa sasa wa
jimbo hilo M… Read More
Shilole Hausiki Kuvunja Ndoa Yangu Bali ni Wazazi wa Nawal- Nuhu Mziwanda.
Mwanamuziki Nuh Mziwanda amekanusha suala linaloongelewa na watu kuwa
kuvunjika kwa mapenzi kati yake na mzazi mwenzie chanzo chake siyo
Shilole bali ni wazazi wa binti huyo.
“Unajua watanzania ukiwapa picha tu, basi wao… Read More
Shamsa Ford Apambana na Ndoa Yake Asema Hawezi Kumuacha Mumewe Kwa Sababu ya Amemsaliti.
Mwigizaji wa Filamu Shamsa Ford amesema hawezi kumuacha mumewe kwa sababu amemsaliti na mwanamke mwingine.
Shamsa amejilinganisha na Hillary Clinton aliyekuwa mke wa Rais wa 42 wa
Marekani, Bill Clinton aliyewahi kuingia … Read More
Nyota ya Zari Yazidi Kung'aa Apata Shavu Nono Mercedez- Benz.
Mwanadada Zarina Hassan maarufu kwa jina la Zarithebosslady amepata dili
la kuonyesha magari aina ya Mercedez-Benz ya kampuni ya AMG Performance
Centre iliyoko nchini Afrika ya Kusini.
Hayo yameonekana baada ya mwanadada… Read More
0 comments:
Post a Comment